TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Kwani ile bambo ya songea mbambabay imeacha routes au
 
Huu uzi mzuri kweli kwa kumbukumbu. Umetukumbusha mbali mkuu, baada ya kupitia uzi kuna visa vimenivutia.
1. Kupata kiini cha kufa kwa kampuni ya Hood
2. Dereva aliyetoka Dar na kufika Mbeya saa 7, hii ni balaa.
3. Ajali iliyokula 70 dah! Bado natamani kupata mwendelezo wake, 70 kwenye bus moja ni kisanga hiki. Halafu kwanini ajali za miaka ya nyuma ziliua sana watu wengi kwa mpigo? Nakumbuka bus jingne sijui (air msae) lilipata ajali kilimanjaro likaua sana wanafunzi.
4. Simon Sirro RPC Tanga [emoji1]
5. Nami niongeze yangu nnayokumbuka ambayo sijayaona huko juu
  • Air Shengena
  • Kizota
  • Fresh ya Shamba
  • Bembea
  • Royal
 
Kweli mkuu nimeiona Hadi miaka ya hivi karibu pale songea na Lina abiria nyomi bila kujali mabasi ya kisiasa yaliyopo barabarani
 
Kwani ile bambo ya songea mbambabay imeacha routes au
Hii bamboo imefilisika Ina maari mawili tu yote hunzia Mbinga kwenda tunduru. Songea mbambabay imekamatwa na kampuni za wazawa kisumapai na kangaulaya na Zina magari high class
 

Zilikua zinabebq abiria wengi kulingana na wingi wa siti. Huduma za abiria wakati wa tahadhari kama mikanda hazikuwapo.

Sema zilikua zinafukia sio rami uchwara au vumbi
 
Tuwekee MAPANDE na FRESH YA SHAMBA iliyokua inapiga Dar Arusha
 
Scandinavia gari ya kwanza kwangu kupanda ina choo ndani, tunapewa biskuti na soda.. nimetumiwa sana hela kupitia basi hili
Ni kweli kabisa mpaka sasa sijaona kampuni iliyofikia viwango vya juu kama hawa jamaa. Pale head office yao Kamata ukifika utadhani umeingia airport ndogo [emoji12][emoji12]
 
Huyo mwenye Bus za Kiswele nikiwa Lindi wilaya ya Kilwa niliwahi kufika kijiji kinaitwa Kiswele baada ya kudadisi wenyeji kwamba kuna kampuni ya Bus zinaitwa Kiswele wakaniambia aaaah huyo ni mzaliwa wa hapa Kijijini na nyumbani kwake paleee. Kiukweli watu wanahangaika kutafuta maisha maana hicho kijiji miaka hiyo ilikuwa hata gari halifiki, mnaishia njiani mnaacha gari halafu mnatembea kwa miguu.
 
Yaani hapo kwa Sirro daah..
kumbe watu wametoka mbali.
Imagine 2009 jamaa tayari RPC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…