Super Najimunisa.....Majini 7
Enzi hizo Dodoma Shinyanga ni Vumbi tupu.
Basi Bwana,
Ilikuwa ni Mwaka 1999 natika Zangu Mwanza naenda Shule Morogoro nikaoanda Super najmunisa....Hahahah Acha Kabisa hili basi Sio Basi tuu ni Dereva Anaitwa “Rama Mtoto”
Alikuwa akiendesha Scania.93 ile nadhani!
Unaambiwa Kwanza Mpaka Matrafic walikuwa wanampenda...dogo alikuwa na control ajabu duu!
Basi Nimetoka mwanza tuko na Ligi ya Zuberi,Amit,
Tukaingia Shy chaaap,Hatukukaa sana Chombo Kikaoshwa....Hapo Zuberi na Amit wako mbele yetu[emoji3516][emoji41][emoji851][emoji30][emoji30]
Barabara ni vumbi tuu,Tukaanza Kumtafuta Mmoja baada ya Mwingine,Tunafika Tinde Amit huyu hapa...Chapa Rubber... tukaingia Nzega,Bado Zuberi haonekani...
Dogo anatembea anakuka Karanga tuu!
Mzee niko siti ya Mbele kabisa Nyuma yake,Tena yeye aliniambia Usilipe Nauli hela nipe Mimi! Nikampa.
Tunaingia Igunga...Zuberi huyu hapa nae anatoa Chombo...Sisi tukapaki kwanza...
Dereva Rama mtoto akasema tuondoke jamani,ngoma ikaanza...ni vumbi lakini Imechongwa....Piga piga Mara shelui Zeberi hiyu hapa....Akaombwa site,Overtake akakataa...[emoji3516][emoji3][emoji3][emoji3]Rama katulia tuu na Kitu Scania...
Ngoma Sekenke mlimani pale Rama akaomba tena Kwenye Mlima...[emoji30][emoji30][emoji30]Jamaa kambania kambania ile tunamaliza tuu ile S Rama akaingia kwenye tuta za Viazi[emoji23] Ngoma Imekubali mpaka watu wanashangilia Ile Overtake ya Kibabe! Jamaa Zeberi anachanganya wapi...Rama anatembea na Gia No.5 tuu Break ya Kwanza Singida tumekaa Pale Saa nzima Jamaa wooote mabadi yooote hayajatokea tuu Tukang’o chombo.
No.2 nyingine
Kama Kawaida dogo Rama Mtoto yupo Kwenye Super Najmunisa Tumekwama Manyoni kwenye Tope balaa!Sisi Tunaenda Dar,Tukakutana na Super najmunisa C.I.A ikiendeshwa na George
Wakati sisi tukiwa na NATO chini ya Dereva Mtoto Rama acha Kabisa!
Mlangoni yupo Mhindi Tajiri.
Baada ya Kushindikana Kupita na Magari yote yapo pale...Na Kamvua Kananyesha...Tukaambiwa tushuke tutembee...
Sawa tukashuka...Akabaki Rama peke yake kwenye Usukani....[emoji41][emoji851]
Akaanza Kuitoa Mashine...Kama Unavyojua Mlio wa Scania Mpaka Yule Tajiri Muhindi Akaanza Kutukana Kuionea Huruma Gari yake...[emoji51]
Ngoma Mpaka Imelala....
Rama Akairudisha nyuma eee bwanaeee...
Alipita nayo pale mkukuu inalala Kulia Na Kushoto jamaa yumoo tuu mpaka akaileta Upande wa Pili...
Halafu hao tukapanda tukaenda zetu[emoji851][emoji3516][emoji123][emoji91][emoji91]
Rama mtoto Super Najmunisa...Baadae Zuberi,Baadae nimesahau jina La Basi Alilokuwepo tena...
Alikuwa akishindana na Muhando(Marehemu kwa sasa)
Na Ukitaka Kumjua Ulikuwa unawnda Pale Ubungo Stendi Sehemu Inaitwa madereva Mashuhuru Utampata[emoji119]