TCRA, BASATA zafungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft Zuchu - "Watasubiri Sana"

TCRA, BASATA zafungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft Zuchu - "Watasubiri Sana"

Mamlaka ya wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeufungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz na Zuchu unaoitwa "Watasubiri Sana' baada ya kupata taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa wimbo na video hiyo inaleta ukakasi kwa waumini wa dini na dhehebu fulani.

Wimbo huo unafungiwa licha ya kuwa una mwezi mmoja tangu ulipowekwa YouTube, ukiwa umetamzwa zaidi ya mara milioni 10.2.

Video ilishatapakaa utube kila kona unaufungiaje!??

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Sababu yakufungiwa ni kutokana na maudhui ya kuudhi dhini ya dini ya kikristo,sehemu ambayo inamuonyesha Zuchu akiiacha kwaya na kukimbilia nje kuongea na simu kitu ambacho hakina uhalisia kwa madhehebu ya dini hiyo.

Hapa najiuliza tu hivi inakuaje Nabii Tito anaendelea kutamba mitaani,na hata clip za sheikh Mazinge zinatamba lakini hakuna tamko lolote la kulaani haya mambo,iweje tu kwa kipande cha wimbo wa domo kilete shida?
 
Dharau kwa ukristo huku wote wakiwa ni Muslim..

Wangefanya hivyo kwa imani yao wangelaaniwa na kuombewa hata kifo....

Hii ndio tofaut ya saba mara sabini na jino kwa jino....

Dini Tumeletewa/Mungu hana dini..

Wala gharama za maisha hazichagui mwenye dini au mwenye Mungu[emoji3508]...

Turudi kwenye hoja za msingi kuhusu bei ya mafuta na mfumuko wa bei kwa kila kitu tusitolewe relini na haya mambo ya maigizo ya kizungu pita..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hivi Yale si yalikua mazoezi ya kwaya?..wanauhakika Kama wana kwaya hua hawapokei simu au kutoka nje wakati wa mazoezi ya kwaya!!..kazi kweli kweli
Wangeigiza madrasa imefanya hivo tuone kama ingefaa si wao waisilam na wanaijua dini yao why wawafedheeshe wakristo?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Dharau kwa ukristo huku wote wakiwa ni Muslim..

Wangefanya hivyo kwa imani yao wangelaaniwa na kuombewa hata kifo....

Hii ndio tofaut ya saba mara sabini na jino kwa jino....

Dini Tumeletewa/Mungu hana dini..

Wala gharama za maisha hazichagui mwenye dini au mwenye Mungu[emoji3508]...

Turudi kwenye hoja za msingi kuhusu bei ya mafuta na mfumuko wa bei kwa kila kitu tusitolewe relini na haya mambo ya maigizo ya kizungu pita..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Waliotuletea ukristo wenyewe wanatuona mafa.la
 
Mimi sijaona ukakasi 'wowote' kwenye video hii. Sana sana nimeona transformation 'kubwa sana' kuwa sasa kumbe hata ambao sio wakristo wanajua umuhimu wa kufuata maadili na misingi ya dini hasa kipindi cha uchumba!

So far, video 'iko poa saana' hasa ukichukulia kuwa imefanywa na watu ambao ni 'wachanga kiroho'.
Safari ya kiroho iko na ngazi zake. Kuna watoto wanaonyweshwa maziwa, kuna wanaopewa uji na kuna wazima wanaolishwa kande.
Sasa wale waliofikia steji ya kula kande wasiwazamishe wale wadogo ambao bado wanatambaa.
Kwa kusema haya, sioni sababu ya video ya 'mtasubiri sana' kufungiwa kwa grounds hizo zilizotumika.
Wale wanao ona ina ukakasi wasiitizame! (Wasikilize audio au watazame video nyingine ambazo hazina ukakasi).

Bwana wetu Yesu Kristo alisha sema, 'nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi'.
Msiwabebeshe mzigo mzito wasanii wetu na wakati Yesu mwenyewe alishasema kuwa mzigo huu utakuwa ni mwepesi kwa wale wote watakao mpokea na kufanyika kuwa wana wake!
 
Labda wanatulazimisha kuangalia royo tua yenye maadili ya Kitanzania
 
Basata ni wapuuzi sana wanamuwinda Diamond kila wakati. Lakini wajue hawawezi kumshusha na hawezi wapigia magoti najua hizi ni hasira za kususiwa tuzo zao zikakosa msisimko.

Wanamuziki kibao na filamu zinafanyiwa makanisani lakini miaka yote leo wamekuja kuona la Diamond.

Cha ajabu wakristo nao wanashangaa tatizo lipo wapi
 
Ka ni habari ya kweli, na kama sababu ni hiyo iliyoainishwa hapo juu... basi BASATA wako na tatizo pahala

Sidhani kama tatizo ni la Diamond ikiwa kanisa husika limetoa kibali na mibaraka tosha ya kufanya video hiyo ndani ya kanisa

Wenye imani yao wameruhusu imani yao kutumika, BASATA anaingilia vipi ikiwa yeye si msimamizi wa imani hiyo
 
Back
Top Bottom