TCRA, BASATA zafungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft Zuchu - "Watasubiri Sana"

TCRA, BASATA zafungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft Zuchu - "Watasubiri Sana"

Mtoto wa juzi Tanzania imefahamika kimuziki tangu zamani. Domo janja janja nyingi ndo maana mnamuabudu. Huko kenya hata Mr Nice walimtaka,Rose muhando nae. Kila kitu kenya kenya kenya ndo maana wanatudharau
Hata Kenya tu wanamhitaji kwa sana awe Kenya. Hata huko Africa magharibi,hususani Nigeria wanathamini sana vya kwao kwanza. Hata mziki wao wanausapot kwa nguvu.

Tuthamini vya kwetu na tuwe na ya kuvisapo. Tupende tusipende,tukatae tukubali Diamond kaupeleka mbali sana mziki wa bongo. Kaitangaza sana Tanzania nje ya mipaka. Lakini humu kwetu wachawi ni wengi. Hata serikalini wapo wengi tu wachawi wake. Shida ya wengi umasikini unawasumbua. Wana wivu. Kweli nimeamini UMASIKINI NA UCHAWI WANAISHI NYUMBA MOJA.

Pamoja na yote kiukweli nimeshindwa kabisa kuisaport bongo movie,wanacheza mdunguano tu wale kenge. Ndio ujue bongo fever iko vizuri mpaka nimeisapot
 
Mtoto wa juzi Tanzania imefahamika kimuziki tangu zamani. Domo janja janja nyingi ndo maana mnamuabudu. Huko kenya hata Mr Nice walimtaka,Rose muhando nae. Kila kitu kenya kenya kenya ndo maana wanatudharau
Duuh...! Sijui Diamond alikufanya nini wewe mama?. Maana sio kumdis kwa hivyo. Hebu weka wazi hapa kuna nini kati yako na huyu dogo?. Au ndio yale yale?
 
Sababu yakufungiwa ni kutokana na maudhui ya kuudhi dhini ya dini ya kikristo,sehemu ambayo inamuonyesha Zuchu akiiacha kwaya na kukimbilia nje kuongea na simu kitu ambacho hakina uhalisia kwa madhehebu ya dini hiyo.

Hapa najiuliza tu hivi inakuaje Nabii Tito anaendelea kutamba mitaani,na hata clip za sheikh Mazinge zinatamba lakini hakuna tamko lolote la kulaani haya mambo,iweje tu kwa kipande cha wimbo wa domo kilete shida?
Mbona miaka nenda rudi watu wanaact mashehe mbwabwa nk
Na hakuna shida
 
Kama mkristo hainisumbui, sijali kuhusu hayo.
Lakini Tuulizane maswali haya
Je kilichofanyika kinaleta picha gani kuhusu wakristo?
Vipi wangefanya kuhusu dini zao wenyewe yaani uislam, waislam wangechukuliaje?
Kama Ungekuwa wewe ni TCRA, hii ni content inayofaa?
Kuna maswali mengi ya kujiuluza kuhusu hiyo video na hilo katazo lenyewe mkuu

1. Nini chanzo? Kwa maana nani aliwasilisha lalamiko BASATA?

2. Nani wa kulaumiwa kuhusu video production and location?

3. Ilikuaje hiyo video ikarekodiwa kwenye hiyo location?

4. Nani anakagua kazi ya msanii, wakati gani, kwa lengo gani, wapi? Kabla ya kumfikia mtazamaji?

Na mengine mengii

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nisamehewe!!!

But in short,imani uliyoitaja hapa msingi wake mkuu ni unafiki,nazini lakini nguruwe haramu,naiba ila kunywa pombe haramu,nasali lakini kutukana na kuita majina ya kuudhi asiyefanana na mimi siyo haramu.
Uwezo wako wa ku reason ni mdogo sana, unahusisha matendo ya uisalam na misingi ya uislam, bahati nzuri hayo yote uloyataka kama

1. zinaa imekatazwa wazi na hujumu yake kwa alieona ni kupigwa mawe hadi kufa na asieona ni mijeledi 100,lipo katazo la moja kwa moja kua "usiikaribie zinaa" yani si kufanya tu hata vile vitakavyoshawishi

2. Kuhusu uizi, sheria inasema muizi akiiba mara ya kwanza anakatwa kinganya cha mkono wa kushoto nk.

Husu unafiki, katika uislam unasema wanafiki watakua tabaka la chini kabisa la moto, na kama unafahamu hadithi maarufu ya alama za unafiki ni tatu
A. Ukitoa ahadi hutekelezi
B. Ukiaminiwa unaleta uhaini mf umekopeshwa af usilipe
C. Ukizungumza huongea uongo

Yote haya ni mafundisho ya uislam, unapitaka kuujua uislam, usome uislam na sio wanaojiita waislam unaoshinda nao baa, ni sawa na leo nikitaka kujifunza ukiristo niende nikachukue Nabii Tito kama reference.
You have to learn principles not those given principles
 
Ulitaka wafungie kanisa?
Unaelewa maana ya kanisa? Unadhani lile Jengo ndio kanisa?
Hili hi jambo la kanisa/wakristo kujitafakari

Hata tu kutoa kibali kwa ajili ya ku_shoot nyimbo za kidunia ni fedheha... jambo kama hilo huwezi kulikuta upande wa pili... hivyo tatizo kipo kwa kanisa lenyewe

Hata Yesu alipokuta kanisa limegeuzwa sehemu ya biashara alimaindi sana
 
Wimbo imegungiwa?
Mtoa mada unajua maana ya kugunga?
kugunga Ni kutoshiriki tendo la ndoa mpaka ndoa
 
Hili hi jambo la kanisa/wakristo kujitafakari

Hata tu kutoa kibali kwa ajili ya ku_shoot nyimbo za kidunia ni fedheha... jambo kama hilo huwezi kulikuta upande wa pili... hivyo tatizo kipo kwa kanisa lenyewe

Hata Yesu alipokuta kanisa limegeuzwa sehemu ya biashara alimaindi sana
Kosa likiwa kwa kanisa halizuii mamlaka kufanya kazi zinapoona mambo hayaendi sawa.
 
Nenda Msikitini Leo omba kibali Cha kushoot wimbo then hiyo video ioneshe watu wanaiba kaswida alafu ikatishwe ili mtu apokee simu,
Mkuu utaona matokeo yake
Kwanza sidhani kama unaweza kupewa kibali cha ku_shoot nyimbo zisizo na mlengo wa imani yao

Sijawahi kuona wimbo wowote wa bongofleva umeshutiwa msikitini... uwe ni wenye content mbaya ama nzuri. NEVER!!

Huku Ukristoni ndo kurahisi... si bongo movie wala bongofleva ni mwendo wa cut and action kila siku
 
Kuna maswali mengi ya kujiuluza kuhusu hiyo video na hilo katazo lenyewe mkuu

1. Nini chanzo? Kwa maana nani aliwasilisha lalamiko BASATA?

2. Nani wa kulaumiwa kuhusu video production and location?

3. Ilikuaje hiyo video ikarekodiwa kwenye hiyo location?

4. Nani anakagua kazi ya msanii, wakati gani, kwa lengo gani, wapi? Kabla ya kumfikia mtazamaji?

Na mengine mengii

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
1.Kufungiwa sidhani ni kuwa mpaka kuwe na mlalamikaji.
2. Mamlaka hazideal na Directors zitadeal na mtu aliyeleta kazi kwa Umma.
3. Ni kwa sababu walikusudia kuonesha kitu ka hicho na si bahati mbaya.
4.Sidhani kama ilipelekwa kukaguliwa, ingefungiwa huko huko.
 
Kosa likiwa kwa kanisa halizuii mamlaka kufanya kazi zinapoona mambo hayaendi sawa.
Mambo hayaendi sawa kwa muktadha gani mkuu??

Ile misalaba na mabenchi yanayoonekana mule?? Au ile kwaya inayoimba mule?

Kwa mtazamo lile ni kanisa... yes sina pingamizi ila tunatumia hisia kuamini kuwa ni la kikristo, jambo ambalo yawezekana tusiwe sahihi
 
Daaah Kwa mtazamo wa dini hcho kipande walikiigiza isivyo , script ipo Sawa Ila action zilizingua , kulikuwa na viashiria vya dharau kimtindo...na hawakuonyesha heshima Kwa action mle ndani ya kanisa .....!!
Wasipokuelewa hapa, hawatakuelewa tena.
 
Mambo hayaendi sawa kwa muktadha gani mkuu??

Ile misalaba na mabenchi yanayoonekana mule?? Au ile kwaya inayoimba mule?

Kwa mtazamo lile ni kanisa... yes sina pingamizi ila tunatumia hisia kuamini kuwa ni la kikristo, jambo ambalo yawezekana tusiwe sahihi
Unadhani ni dini gani basi?
 
Unadhani ni dini gani basi?
Hata kwa kudhani bado sitoweza kuwa na jibu...!!

Tunazo dini nyingi zenye makanisa mengi na yenye taratibu/kanuni/tamaduni tofauti ILA kama ni dini ya kikristo ndiyo imetoa kibali kwa ajili ya hiyo scene basi automatically imenajisi kanisa takatifu la Mungu
 
Inawezekana wewe sio mkristo, prove me wrong.
Ila haijalishi nani alikupa kibali, Ukileta kazi yenye walakini mamlaka zitafungia.
Na ndicho kilichotokea.
 
Ni kukwamisha tu Juhudi na kutaka watanzania waachane na kelele za mafuta upepo uende wa mondi.

Nchi ya hovyo sana na wanaonekana kufanikisha mkakati wao
 
Inawezekana wewe sio mkristo, prove me wrong.
Ila haijalishi nani alikupa kibali, Ukileta kazi yenye walakini mamlaka zitafungia.
Na ndicho kilichotokea.
Mimi hi mkristo mkuu... tena yule anayeumizwa na mienendo mibaya ya kanisa

Unasema ukileta kazi yenye uwalakini unafungiwa... je, nani kathibitisha kuwa kanisa lililotumika na aina ya kwaya no ya Mkristo.... ikiwa je ni dini tofauti na ukristo na hayo yanayoonekana humo yanaruhusiwa kwa aimani yao?
 
Back
Top Bottom