TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi. https://t.co/qq7KDtZnZv

Sasa kiki ya penalt tayari, mpira wetu Polepole ana hanjahanja, goli nani analifunga!
Akome kabisa Bwn. Polepole, na hii iwe fundisho kwa wanasiasa wengine, mnapokuwa na dhamana ya cheo bas msiwaone wengine hawafai!!

Shda kubwa ya ndung Polepole ni kutumika na kutumia vibaya cheo alichodhaminiwa enzi za jiwe!!
 
Akilalamika kwa hili tunamuweka makofi ya maana,alikuwepo wakati sheria mbovumbovu kama hizo zinatungwa na akazibariki kwahiyo joka alilolifuga mwenyewe acha limtafune
 
Bora mwenezi amekuwa ni KOMREDI SHAKA HAMDU SHAKA....

Komredi Shaka ameiva na kuivishwa vyema itikadi ADHIMU YA CCM......

Komredi Shaka ni sawa na Komredi Dr.Suleiman Serera........hawa ni vijana wenzetu WATULIVU NA WAZALENDO HASWA....si ndg.Polepole......

Ndg.Polepole anaongozwa sana na HISIA za KISIASA.....ni rahisi kuusoma moyo wake uliyojaza kupitia MATAMSHI NA MANENO YAKE YA KISIASA.....

HASHTAG CCM IMFUKUZE ndg.Polepole

#Siempre CCM💪
 
Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi. https://t.co/qq7KDtZnZv
IMG_20211217_142142.jpg
 
Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi. https://t.co/qq7KDtZnZvView attachment 2047426
Nanyi pia ni wapotoshaji.
Hivi angekuwa upande wa pili si kina Siro na kundi la Kingai walishamsweka ndani.
Kwanini msiwajibike naye kama kipindi ni cha hovyo??
 
I might not agree with what you say.., but I will defend it to the death for your right to say it....

Haya mambo ya kuzibana midomo na kufungiana inabidi tuyakatae wote kwa pamoja..., leo anafungiwa adui yako, kesho utafungiwa wewe kwa mtaji uleule aliofungiwa adui
 
TCRA wanaweza kusibitisha hayo mbele ya sheria?

Naona kama wanampa kiki Polepole tu hapo. Tunamsubiri aje huku tweeter afungua space
Polepole anavuna matunda ya kazi yake. Ikiwezekana wasishie kumfungia tu bali wamfunge na yeye mwenyewe.

Sheria zote ovyo za awamu ya 5, Polepole alihusika. Uzuri wa sheria hizi, kwanza aufaidi Polepole, aliyezitolea jasho.
 
Alichokuwa anafanya ni kama uhaini....inatakiwa akamatwe wakati jeshi la polisi likiendelea na taratibu za uchunguzi 😆
 
Back
Top Bottom