TCRA kudhibiti utoaji huduma za vifurushi kwa kampuni za simu

TCRA kudhibiti utoaji huduma za vifurushi kwa kampuni za simu

Hili agizo athari zake ni kupunguza mapato ya mitandao , mapato ambayo yangesaidia mitandao kuwekeza zaidi kwenye miundombinu
Inapunguzaje mapato? Kwani nikimpa mtu mb zangu si anatumia ambacho kimeshalipiwa?

Lakini pia unaongezaje mapato kwa kula njama na kuibia watu kwa kuwaambia eti kifurushi chako kimeexpiry!
Kauli ya ajabu kbs!
Halafu hela zangu kachukua!
Hakuna alichouza/kutoa lakini kalipwa pesa
Ni wizi kama wizi mwingine tu"

TCRA wanakwama wapi?
 
Inapunguzaje mapato? Kwani nikimpa mtu mb zangu si anatumia ambacho kimeshalipiwa?

Lakini pia unaongezaje mapato kwa kula njama na kuibia watu kwa kuwaambia eti kifurushi chako kimeexpiry!
Kauli ya ajabu kbs!
Halafu hela zangu kachukua!
Hakuna alichouza/kutoa lakini kalipwa pesa....
Ni wizi kama wizi mwingine tu"

TCRA wanakwama wapi?
Tena Mkubwa sana
 
Kwa nini uhamishe bando wakati bado kuna option ya kumnunulia bando rafiki
 
Haya mambo rahisi sana..., kwenye hili soko letu huria (sababu wenyewe ni wataalamu na wanasikiliza kila kelele)..., Wawekeze kwenye kampuni ya Serikali TTCL ili hata igawe kabisa vifurushi bure..., thus watapata wateja wengi na haya makapuni either yatakufa au yataiga mfano...

After all si ni demand and supply ? Au?
 
Tigo kila laini ya simu ina menu yake ya bando, hazifanani
 
Kuna watu huwa wananunua vifurushi vikubwa ila hawavitumii vyote sasa hapo ambao watakuwa wanarushiwa hivyo vifurushi hawatakuwa wananunua vifurushi si watakuwa wanawaomba wale ambao hawatumii bundle lote


Kingine hii move mbaya maana jamaa watapandisha pia bei za vifurushi

Litapunguzaje mapato labda..?
 
Pia tuweze kuhamishiana "charge". U know what I mean
 
Pia, mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 kabla ya kuisha na kitakapomalizika kabisa kwa asilimia 100.
inatakiwa ukomo wa kifurushi iwe ni pale kinapoisha kutegemeana na matumizi ya mteja sio kupangiana muda.
 
Kipaumbele chetu sisi kama raia wala sio hicho TCRA wanashindwa tena kututete baada ya kusubiri takribani mwezi mzima
 
Sasa hapo hao TCRA ndo wameleta suluhisho gani sasa?yaani wametatua tatizo lisilo la msingi.Kiuhalisia watu wanalalamika kuhusu bei kubwa za vifurushi ambazo haziendani na matumizi halisi lakini pia zinazobadilika kila kukicha,kwa mfano,unakuta umejiunga kifurushi cha GB 5 kwa wiki,lakini unajikuta kimeisha baada ya masaa matatu kwa matumizi ambayo ni ya kawaida sana,ukiwapigia simu mitandao husika wanakupa ngojera za kutosha oooh mara hukuzima data na bla bla kibao.

TCRA waje na price control mechanism ili hata huyo wanayetaka nimuhamishie kifurushi changu nilichonunua,awe na uwezo wa kununua cha kwake.Utadhani wameenda kuongea bila kusikiliza hoja na wananchi na kufanya uchambuzi wa hoja zao.
 
TCRA imewataka watoa huduma za simu nchini kuweka utaratibu utakaomuwezesha mteja kuhamisha unit za kifurushi chake kwenda kwa mtumiaji mwingine aliye ndani ya mtandao wake.

Pia wametoa sharti la kiasi cha chini kuhamisha kutoka kwa mtumiaji kwenda kwa anayehamishiwa itakuwa kuanzia 250MB.

Hatua hiyo imetokana na uwepo wa malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji kuhusu vifurushi vya simu.
Kwa hiyo kwaangu kikikaribia kuexpire namtumia mwingine anaendelea kutumia c ndio
 
Back
Top Bottom