TCRA kudhibiti utoaji huduma za vifurushi kwa kampuni za simu

TCRA kudhibiti utoaji huduma za vifurushi kwa kampuni za simu

Hayo maandishi yote mnaweka kama kujitetea tu kwa Rais Magufuli baada ya kuwapa ONYO, lakini msipotekeza yote hayo na kusikiliza kero za wananchi ni BURE TU.

Uongozi wa TCRA unapaswa kubadilishwa kabisa, viongozi wa juu wanapaswa kutumbuliwa tu.

Hamna tofauti na HESLB.
 
Hayo maandishi yote mnaweka kama kujitetea tu kwa Rais Magufuli baada ya kuwapa ONYO, lakini msipotekeza yote hayo na kusikiliza kero za wananchi ni BURE TU

Uongozi wa TCRA unapaswa kubadilishwa kabisa, viongozi wa juu wanapaswa kutumbuliwa tu

Hamna tofauti na HESLB

Lini Magu aliwaonya TCRA?
 
Nilicho kuja kugundua ni kwamba hii mitandao ina milikiwa na vigogo wa serikalini ambao wameficha identity zao wasijulikane na wananchi ila viongozi wakubwa kwenye system wanajua mchezo wote...
Serekali ilifanya vizuri sana kwa Dangote, lengo la dangote ilikuwa sio kuwasaidia wananchi bali kuuwa viwanda vingine vya cement kwakuwa ana nguvu ya kipesa, kama angeuza cement 7000 kwa mwaka mmoja tuu angekuwa ameshachukua wateja wote viwanda vingine vingekosa wateja na ili kuja kupambana na dangote ingebidi virun kwa hasara.

So in two years angekuwa ameshaviua, then angeanza yeye kucontrol bei yeye mwenyewe mpaka hawa wengine waje kuamka,yeye kasharudisha faida ya kutosha na ameshakuwa papa sokoni,so ingekuwa ngumu sana kwa viwandz vyetu vya ndani.

Wakati mwingine msiilaumu sana serekali,wanajitahidi sana kuakikisha nchi inafika mbali kwa kuwainua watanzania bila kuumiza watu wengine wanaowekeza.
 
Baba la mawasiliano TCRA wameshasema gharama za vifurushi viko chini kuliko wakati wowote ule, kwamba ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo gharama ya MB 1 ilikuwa TSH. 104.46, kwa sasa MB 1 ni TSH. 24.26.

JamiiForums-1845015046.jpg


Sasa kwa muktadha huo, hai-make sense mwaka 2018 tulikuwa tunanunua lets say GB 10 kwa 5000/= wakati gharama za data zikiwa juu, halafu kwa sasa ambapo gharama ziko chini kabisa eti utuuzie GB 10 kwa 20,000/=. Hatutawaelewa na kimahesabu haitakubali kubalance.

Screenshot_20210206-093748.jpg


Nanyi TCRA japo mmejitahidi kutoa ufafanuzi na maelekezo lakini mmekwepa kwepa sana ku-hit the point ambayo watu walikuwa wanailalamikia ya vifurushi kupandishwa mara dufu.

Yetu macho, kuanzia kesho tunategemea tuone vifurushi vikirudi bei za mwanzo au chini ya hapo maana gharama zimepungua.
 
Serekali ilifanya vizuri sana kwa dangote....lengo la dangote ilikuwa sio kuwasaidia wananchi bali kuuwa viwanda vingine vya cement kwakuwa ana nguvu ya kipesa, kama angeuza cement 7000 kwa mwaka mmoja tuu angekuwa ameshachukua wateja wote viwanda vingine vingekosa wateja na ili kuja kupambana na dangote ingebidi virun kwa hasara.

So in two years angekuwa ameshaviua...then angeanza yeye kucontrol bei yeye mwenyewe mpaka hawa wengine waje kuamka,yeye kasharudisha faida ya kutosha na ameshakuwa papa sokoni,so ingekuwa ngumu sana kwa viwandz vyetu vya ndani.

wakati mwingine msiilaumu sana serekali,wanajitahidi sana kuakikisha nchi inafika mbali kwa kuwainua watanzania bila kuumiza watu wengine wanaowekeza.
Sio kweli kwamba lengo la dangote lilikua ni kuua viwanda bali hakuwa na tamaa ya kutaka faida kubwa

Dangote alikuwa anajua jinsi ya kucheza na akili ya mteja ambapo pande zote mbili zitanufaika

Aliweka bei ndogo ili kuhakikisha kwa hata mwananchi mwenye hali ya chini aweze kuimudu gharama na lengo lilikuwa mzigo uuzike haraka na pesa iingie

Viwanda vya ndani sio kwamba vikiuza kwa bei hiyo hawapati faida hapana ni kwasababu wanafanya hivyo kwa tamaa ya kupata faida mara tatu zaidi

Biashara ni competition tamaa ya ku demand high profit ndio inayowafanya watu waone competitor anauwezo wa kuua biashara yako
 
Akizungumza leo Jumanne Machi 2, 2021 mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema utekelezaji wa kanuni hizo utaanza Aprili 2, 2021.

Miongoni mwa yaliyoelekezwa kwenye kanuni hizo ni huduma zote za vifurushi lazima zipate vibali vya TCRA huku mamlaka hiyo pia ikitoa mwongozo wa bei zilizowekwa na mamlaka hiyo.

Nyingine ni vifurushi vyote havitaondolewa au kurekebishwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuidhinishwa.

Pia, mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 kabla ya kuisha na kitakapomalizika kabisa kwa asilimia 100.
Hawakutakiwa kuja kutuambia sisi, walitakiwa waende kazini nasi tuone matokeo
 
Back
Top Bottom