TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

Hata sasaivi kuna line ukinunua zinakuwa na PIN activated na huwezi iweka off labda kubadili, mimi yangu ya airtel ipo hivyo na nimeona hata nyingine za halotel PIN iko activated. Hata hivyo hiyo ni nzuri kama ukipoteza simu mtu hawezi itumia kwa uhalifu or utapeli.
 
Dah....nimesoma mara 9 Ila sijaelewa...labda nisubiri kvant ipungue kichwani
emoji2960.png
 
Yaani wanataka ikiwezekana wajue kila Mtanzania anaongea nini daah!!
Tunaiga wavimba macho kule ukipost chochote ambacho serikali haikipendi hakiendi hewani
Na kingine ni kuwapunguzia polisi majukumu ukifanya tukio hasa haya ya madereva barabarani husimamishwi na trafic , habari zako utasoma gazetini kesho yake au kwenye tv
 
PIN na PUK zipo tangu mwaka 1996 kwenye SIM card yako.

Huu ni ushamba tu.
Ukichunguza kuna ile pin2 huwa hatuitumii.

Kwa nilivyowaelewa.. kuna ile line hautuitumii muda mrefu anakuja kupewa mtu mwingine hivyo itakua ngumu mpaka aww na pin ya namba husika.. kwa maana hiyo namba ya line yako itakua ni ya maisha yako hata usipoitumia miaka haitawezekana kupewa mtu mwingine.

Nimeelewa hivyo bado sina uhakika lakini
 
Wakulungwa hii ina tofauti gani na Sim Pin Code?! Au hii hutokuwa na uwezo wa kuidisable?!
Hiyo hutoweza ku disable ila waweza kubadilisha. Na tayari line mpya tokea mwishoni mwa 2020 zina huo utaratibu.

Hiyo mambo ya julai nadhani ni kuacha nafasi stock ya line za zamani iishe mitaani.
 
Sasa itakuwaje kwa SIM cards ambazo tayari zipo sokoni? Kama lengo ni kumaliza utapeli hazitakiwi ziachwe bila PIN.

Bado sijaona faida ya ule usajiri wa alama za vidole kama mpaka leo bado kuna zile msg za matapeli.

KUNA MTU ANASAKWA HAPO
 
Amna kitu apo Kam wanatak kutokomeza utapel waanze na wale wa tuma kwny namb hii,,, ila kw saiz ukipata ajali au dharula yyte hatutakua tena na uwez wa kutumia lain yako kuwapigia watu wak wa karbu
 
Hata sasaivi kuna line ukinunua zinakuwa na PIN activated na huwezi iweka off labda kubadili, mimi yangu ya airtel ipo hivyo na nimeona hata nyingine za halotel PIN iko activated. Hata hivyo hiyo ni nzuri kama ukipoteza simu mtu hawezi itumia kwa uhalifu or utapeli.
Tunajidanganya, kina jambo limejificha hapo. Kwa nchi ambayo unataka kujua hata ya chumbani ya raia, ni muda, tuwe na subira.
 
Ndugu Mteja, laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri ambalo Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama.

I smell a fish juu ya laini hizi. Nitahakikisha sipotezi laini ilikuepuka kurenew laini nakuingia huku.

--
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo Julai mosi, laini zote zitakazotolewa zitakuwa na neno la siri ambalo mteja atatakiwa kulibadilisha ili kutumia laini mpya yenye usalama.

Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa jana kwenye simu za wateja mbalimbali ambao ulithibitishwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa TCRA, Semu Mwakyanjala, utaratibu huo utalinda wateja.

Alisema utaratibu huo una lengo la kuwalinda wananchi kwenye matumizi ya mawasiliano.

“Laini inapopotea ikachukuliwa na mwingine anaitumia vibaya lakini kwa kuwa na neno la siri, itamlinda mtumiaji na kuondokana na utumiaji usio salama,”alisema.

Mwakyanjala alisema utaratibu huo ni kwa mujibu wa sheria ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 na kanuni zake za 2018.

“Tunataka matumizi bora ya mifumo ya simu si kwa ajili ya kuongea bali kama benki, hivyo usalama ni muhimu kwa ajili ya kuwalinda watumiaji, watu watumie simu kwa biashara na maendeleo kuliko kufanya uhalifu,”alisema.

Chanzo: IPP
Unapopewa ATM card mpya unaambiwa ubadilishe password uweke ya kwako. Pia huwa unasmell fish?
 
Awa TCRA ata siwaelewi majukumu yao,, Mitandao inatunyonya, network mbovu, wao kazi kufungia TV station tu...

Nilitaka kuuliza wameshindwa ku monitor makampuni ya simu yanatuibia wamekalia ku track tu simu za watu !
 
Back
Top Bottom