TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

Badala ya kushughulikia upatikanaji wa umeme busy na vitu visivyokuwa na kuchwa wala miguu kisa Mange
Mchongo wa nape huo ndo anajitahidi kila mara bos wake asipigwe m
Sheria za kishenzi zilizotungwa enzi za mwendakuzimu zitatutesa sana.
Amka ww unayemtaja ameshaafariki mika 3 iliyopita ,anayeungoza nchi ni mwanamke ,ww bado unamuota mwenda zake
 
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni zilizowekwa basi adhabu itakayotolewa kwa kosa hilo ni faini ya shillingi milioni tano, au kifungo cha mwaka au vyote kwa pamoja.

View attachment 2781209
Ukiona hivyo ujue Kuna kitu kinaandaliwa Maana Walifungia Clubhouse Wajanja wakatumia VPN na Kama kawaida vitu vikaendelea,
ukiona hivyo ujue wanapanga kufungia Twitter,Whatsapp na social network hizi ili wapate matokeo mazuri ya uchaguzi kusiww na majumuisho ya Watu..
 
Haya kataa ndoa, wazee wa kujidunga hatimaye mmefikiwaaa🤣🤣🤣 Kifungo au faini🤣🤣🤣🤣🥟
Torrent siyo kosa wataenda kupakua kwenye torrent sites.
Tena hizo watatazama hata wakiwa offline.
Nchi hii imeanza kuwa kama China, Iran au North Korea.
Bora Jiwe alituachia VPN.
 
Nahisi kuna kitu Cha ziada nyuma. Wanasema kama Kuna wananchi na kampuni ili kufanya kazi zake lazima watumie VPN lakini kazi hizo ni zipi? Hakuna mtu anafanya kazi za X ambazo ni halali. Maana yake Kuna mitandao imefungwa na haihusiani na X. Tatizo letu tumepeleka macho kwenye X tu tukaacha kule ambapo serikali ndo inataget. Kweli inatakiwa kulinda kizazi kinachokua na athari za utandawazi ila lazima wawe specific.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra) imewapa tahadhari wale watu wanaotumia program mbalimbali za kuvunja sheria moja wapo kutumia mtandao wa VPN.

View attachment 2781574

Watu wengi utumia mtandao wa VPN kuficha uwalisia wao mtandaoni au kuingia Kwenye tovuti au website, app ambazo zilizozuiliwa mahali Fulani basi unaweza kutumia vpn kuingia mahali humo.

Tcra imechukua jukumu la kuzidhibiti matumizi ya VPn nchini Tanzania yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa Vpn ambazo hazijasajiliwa au hazijatolewa taarifa zozote kupitia Tcra.

Tcravpn%20%E2%80%93%201.jpg


Tcra inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa utoaji, umiliki au usambazaji wa apps(program) au website (tovuti) yoyote ambayo inamsaidia mtu kupata taarifa au maudhui yaliyokatazwa ni kosa la jinai ambalo unaweza kuadhibiwa ukipatikana na hatia.

Kifungo kisichopungua miezi Kumi na mbili au faini ya milioni 5 au vyote kwa pamoja. "jihadhari kutumia Vpn Nchini Tanzania ni kosa kisheria utafungwa[emoji108]".

#tcra #sheria #bongotech255
 
Ukiwa una hela unahama tu hii nchi. Hii ni Nchi ya vilaza na masikini
 
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni zilizowekwa basi adhabu itakayotolewa kwa kosa hilo ni faini ya shillingi milioni tano, au kifungo cha mwaka au vyote kwa pamoja.

View attachment 2781209
Watumieni watalaamu wa it kuzizua hizo vpn ama kuwafungia juu kwa juu na sio vitisho kuwafunga, watu washindane ki mbinu hii dunia ya ujuzi saivi. Kama wamewekwa wawapishe vijana wakae hapo. Africans we've a long journey to travel
 
Back
Top Bottom