TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni zilizowekwa basi adhabu itakayotolewa kwa kosa hilo ni faini ya shillingi milioni tano, au kifungo cha mwaka au vyote kwa pamoja.

View attachment 2781209
TCRA inahakikisha kuwa kila mtumia mtandao wa simu lazima ashiriki kuibiwa bundles zake na makampuni ya simu.

Hii nchi inaongozwa na wapuuzi wengi sana.

Watu wanatapeliwa na kufanyiwa uhalifu wa kila namna mitandaoni lakini hawa jamaa wapo bize na watu wasiangalie maudhui privacy kana kwamba wameagizwa na Mungu kudhibiti tamaa za watu.

Ni uzwazwa wa karne
 
Du Masikini Mange Kimavi! Ulaji wake ndo Kwishney sijui atapata wapi madolari ya Kuhudumia Life aliyoizoea for these past two Years😭😭😭.Umbeya wake kwenye App yake kwa Wazaramo Wa Tanganyika ndo basi tena kwishney
Watanzania huwa hawaeleweki. VPN wanadhani umuhimu wake uko kwenye website za porn na Mange. Mimi nilidhani mngeona athari yake kwenye kuzuia wananchi kupashana habari muhimu na kuikosoa serikali na siyo mambo ya kijinga namna hii. Hii sheria ya VPN haitamuathiri Mange bali uhuru wa Tanzania wa kupashana habari na kusema mabaya ya viongozi. Anyways, kuzuia VPN kabisa ni ngumu kama kuzuia madawa ya kulevya.
 
TCRA inahakikisha kuwa kila mtumia mtandao wa simu lazima ashiriki kuibiwa bundles zake na makampuni ya simu.

Hii nchi inaongozwa na wapuuzi wengi sana.

Watu wanatapeliwa na kufanyiwa uhalifu wa kila namna mitandaoni lakini hawa jamaa wapo bize na watu wasiangalie maudhui privacy kana kwamba wameagizwa na Mungu kudhibiti tamaa za watu.

Ni uzwazwa wa karne
Uzwazwa ni wetu wananchi kwa sababu akili zetu zimedumaa na hatutafakari mambo. Kuna wengi wanashangalia hii sheria wakidhani Mange au wale wanaoangalia porn sites ndiyo wataathirika.... Hapa ndiyo upeo wetu ulipo...
 
TCRA wafunge Twitter.
Pia ni uwanja wa picha na video za ngono kuliko mitandao ya ngono moja kwa moja.

Sijajua lengo la kuzuia VPN ni nini?
Mbona liko wazi? Ku-block contents za kuikosoa serikali. Wanataka watawala wawe huru kufanya lolote bila kuhojiwa au wananchi kujulishwa. Wanaona ukosoaji wa kwenye mitandao ni tishio kwa CCM. Wewe unadhani serikali inajali wananchi kuangalia ngono wakati mitaani, kwenye vyombo vya habari na hata viongozi wa CCM wenyewe matendo yao kwa jamii ni mabaya kuliko sites za porn?
 
Hii nchi Ina upumbavu na ujinga mwingi sana,Yani wanaacha kutatua matatizo ya msingi kwenye jamii,wako busy kupambana na ujinga ambao hauna athari Kwa jamii au una athari ndogo Kwa watu binafsi.

Umeme tu ni shida,maji,mfumuko wa bei za mafuta hata chakula ni shida,wao wako busy kutunga kanuni za kipuuzi.
 
Hakika mwisho wa CCM umekaribia. That's why vikwazo vimekuwa vingi mno wanaogopa sana!
 
Wkt unaingia mjini daslam stand uliikuta ubungo au mnazi mmoja?
Mkuu japo hujaniuliza Mimi kwa upande wangu stand nimeikuta ubungo.
Na nahitaji msaada wa aina ya VPN ambayo ukiiwasha huhitaji bando.Asante.
 
Katiba, Ibara ya 16

Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake,
maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

===================================

HAKI YA FARAGHA kwenye katiba ipo imeandikwa lakini haitumiki, ni kama haipo. Ndio maana ni sawa hapa Tanzania polisi kukudukua na kukushitaki umemsimanga Rais kwenye simu, na ukafungwa kwa ushahidi uliopatikana kwa kuvunja katiba.

Rais Samia Suluhu alisema tuchukue miaka mitatu kwanza kusomeshana Katiba. Alikuwa sahihi kabisa, kwa saab hata yeye haijui, anaivunja kila uchwao, majaji hawaijui, viongozi hawaijui, na wananchi hatuijui.

Majaji wetu, wanasheria nguli, mawaziri wa sheria, magwidi na wakufunzi wa vyuo, wa kina Mwalimu Palamagamba Kabudi na wenzake huwa wanasemwa wamesoma nje, vyuo vizito, University of Berlin, Ujerumani na kwingineko Ulaya na Marekani. Mbona kule hivi vitu ndivyo wanavyofundishana, misingi hii ya haki kali za raia, hawa wa kwetu kule walipasije mitihani ya hao wajerumani ?????????
Palamagamba Kabudi ni mtaalamu wa SHERIA Aliebobea n, namkubali sana.
Tatizo ni kwamba msomi yeyote akishaingia kwenye siasa maneno na matendo yake hayawezi tena kiendana na maadili ya taaluma aliyosomea Bali atasema na kutenda Yale yanayoendana na maslahi ya siasa za chama anachokitumikia. Kwahiyo madoctor na maproffesor waliojaa ndani ya serikali kwao huangalia maslahi ya chama kwanza halafu taaluma itaangaliwa baadae.
 
😂😂😂 itakuwa wamekugusa na wewe ni miongoni mwa wanufaika wa VPN...

Sio kwa uchungu huo...🤣🤣🤣
Wala sijawahi na.sina shida hoyo na sijawahi.Ninapoona waziri.yuko busy.na.vitu havina msingi Kuna changamoto kibao kwenye sector ya mawaailiano internet inasua sua na still very expensive
 
Nahisi kuna kitu Cha ziada nyuma. Wanasema kama Kuna wananchi na kampuni ili kufanya kazi zake lazima watumie VPN lakini kazi hizo ni zipi? Hakuna mtu anafanya kazi za X ambazo ni halali. Maana yake Kuna mitandao imefungwa na haihusiani na X. Tatizo letu tumepeleka macho kwenye X tu tukaacha kule ambapo serikali ndo inataget. Kweli inatakiwa kulinda kizazi kinachokua na athari za utandawazi ila lazima wawe specific.
Wanataka kudhibiti taarifa wakati wanapofanya vibaya.
Wanawasaka whistle blowers.
Hasa nyakati za uchaguzi....
 
Jambo wasilolijua whistle blowers watasajiri laini za Kenya watafanya roaming wanatumia internet ya huko.

Huku kwetu mitandao (service providers) watatoa ushirikiano kukagua suspicious IP addresses wanazo hisi client anatumia VPN kisha wanakufanyia ambush/police raids na kukagua device ya mtuhumiwa.

Kama wameshindwa Iran na Kenya wataweza wao?
 
kuna kipindi walisema KIAMA YA MATAPELI wa mtandao i,efika wale wa TUMA KWA NAMBA HII watakomeshwa....hamna kitu bado zinatumwa kama kawaida, wakaja na mkwara mwingine kuwa watakomesha wanaojihusisha na mapenz ya jinsia moja pamoja na kukamata wanaosambaza maudhui hayo.. ila ndo kwanza mashoga na wasagaji wanajipost kila siku, wakatangaza kukomesha biashara ya ngono na kukamata wauzaji na wanunuaji mtandaoni... aah wapi, telegram kumekucha watu wana request nyapu kama UBER vile....
haya masihara ya ku deal na mambo madogo tena binafsi waachane nayo, wajielekeze kwenye maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano, wanatia aibu mamlaka kuanza kukimbizana na wapenda umbea wa mange au wapenda pilau, wakati nchi ina changamoto nyingi zakutatuliwa. serikali ya ccm kwa kweli ni hopeless
 
Back
Top Bottom