TCRA yapiga stop wimbo wa Nay wa Mitego kuchezwa kwenye vyombo vya habari

TCRA yapiga stop wimbo wa Nay wa Mitego kuchezwa kwenye vyombo vya habari

Nay - Emmanuel Elibariki.
Mb - Elibariki Emmanuel.
Hili nalifahamu sana tu.

Lakini umeona jina lililotajwa kwenye barua ya TCRA? Barua yenye inaanza na number 2 wakati number moja hakuna? Barua inayosema "KUZUIYA" na sio "KUZUIA"?? Tena ikisainiwa na DG mteule wa Rais anaelipwa hela ndefu tu za kodi zetu?

Umeiona?
 
View attachment 2701756

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) impokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuzuiya wimbo uitwao "Amkeni" uliopigwa na mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) kutopigwa katika mitandao ya kijamii na vombo vya habari..
Wamemvunjia haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni, hii ni censorship.

Tutasikiliza mitandaoni.
 
Hili nalifahamu sana tu.

Lakini umeona jina lililotajwa kwenye barua ya TCRA? Barua yenye inaanza na number 2 wakati number moja hakuna? Barua inayosema "KUZUIYA" na sio "KUZUIA"?? Tena ikisainiwa na DG mteule wa Rais anaelipwa hela ndefu tu za kodi zetu?

Umeiona?

Noma Sana ,makosa mengi sana ya kiuandishi ,hapo kama mimi ningeendelea kupiga mziki wa Amkeni kwasababu haukuimbwa na Kingu huo uliofungiwa.
 
TCRA wasingehangaika kuufungia kwasababu ney mwenyewe na waliomfadhili kuutengeneza, ni yao ilikuwa kuurusha mtandaoni basi na walitarajia muda si mrefu utafungiwa. Matarajio yao hayakuwa uishi hata wiki kwenye vyombo bali urushwe, watu waudake, ufungiwe, ila ujumbe umeshafika.

Ningekuwa mimi ndio TCRA wala nisingehangaika kwenye ulimwengu ambao majority wanamiliki smartphones,wanao kwenye simu.

Na lazima kwa kuufungia kwao watu watatamani wausikilize wajue una nini hadi umefungiwa? Si huwa unaona mtu amepiga picha chafu, tcra imefungia porn ila watu wanatoa hadi pesa waone hiyo porn ipoje. Ndio ushetani,sembuse wimbo tu.
 
Ule wimbo wa siasa. Sio wimbo wa mapenzi. Kwa hiyo ule wimbo ni superior kuliko nyimbo za mapenzi. Kwa sababu wimbo wa mapenzi unaimba kuhusu mapenzi . Such a song will tamper with your hormones.

Na kama watu wanaongelea DP World kila kona,unategemea Ney wa Mitego ataimba juu ya nini?
 
Kuna watu wanaripoti wimbo huu una maovu mabaya ndio maana system ya youtube haiingizi trending na mbaya zaidi inakuwa rahisi kuiaminisha sababu haisikii maneno ya kiswahili kwenye video.

Cha kufanya ingia yputube chukua maneno haya kama yalivyo nenda ukayaposti.

Hey @teamyoutube, there's growing concern that "amkeni" by Nay wa Mitego from Tanzania isn't trending due to possible manipulation by a group of people trying to supress freedom of speech. Please investigate and ensure a fair playing field for all creators.

Kama kiingereza kinapada watag hao @teamyoutube ambatanisha na ujumbe
 
Ney kazoea kukosoa tuu kipindi cha magufuli alikosoa leo hii tena anasema anamkumbuka magufuli hata sielewi anasimamia wap

Ney ni Msanii ambae ameona uhitaji wa Wimbo Kama huu nyakati Kama hizi na akauleta kwa njia ya kisanii kwenye jamii ambayo ipo katikati ya mgogoro wa kutokuelewana na kuaminiana na serikali yao.

Kwanini TCRA na sio BASATA? Mazingira yanataka hivyo, katikati ya makelele nchi nzima BASATA hasingesikika vizuri Ilivyokusudiwa.
 
Mwenye huo wimbo tafadhali.
Tunataka na sisi tuusikie Kama unakisoa au unasifu na kuabudu.
 
View attachment 2701756

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) impokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuzuiya wimbo uitwao "Amkeni" uliopigwa na mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) kutopigwa katika mitandao ya kijamii na vombo vya habari.

Aidha, kwa mujibu wa BASATA, maudhui ya wimbo huo yana melekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali, kuchochea wananchi kuwa na mapokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali yao kwa ujumla, na kuwa ni wimbo wa uchochezi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.

Hivyo, kwa barua hi, TCRA inaelekeza chombo chako cha habari kutopiga wimbo huo.

Tafadhali zingatia maelekezo.

Pia soma: Nay wa Mitego aitwa BASATA. Atuma Wanasheria wake
Badala ya kuzuia nyimbo zuieni Rushwa, Uzembe na lifanyeni Taifa kuheshimika. Ondoeni neno hatuwezi kwenye maongezi yenu. Watanzania tunaweza, tunaweza kuchimba dhahabu yetu, tunaweza kuendesha bandari yetu. Tengeneza mfumo wa wazi wa ajira wenye uwezo waingie pale
 
View attachment 2701756

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) impokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuzuiya wimbo uitwao "Amkeni" uliopigwa na mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) kutopigwa katika mitandao ya kijamii na vombo vya habari.

Aidha, kwa mujibu wa BASATA, maudhui ya wimbo huo yana melekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali, kuchochea wananchi kuwa na mapokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali yao kwa ujumla, na kuwa ni wimbo wa uchochezi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.

Hivyo, kwa barua hi, TCRA inaelekeza chombo chako cha habari kutopiga wimbo huo.

Tafadhali zingatia maelekezo.

Pia soma: Nay wa Mitego aitwa BASATA. Atuma Wanasheria wake
Fear of the unknown...! Maneno ya Mungu yanasema: Mwenye dhambi hana raha..! (Yaani ni mtu wa kujistukia kila wakati)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nape hajawahi kua mweledi, uiunge mkono serikali kwa uuzaji wa bandari au kipi kipya samia kafanya cha maana ? Uliunge mkono bunge ambalo sekretarieti yake yenyewe imesema ilichopitisha hakina maana
 
Ney kazoea kukosoa tuu kipindi cha magufuli alikosoa leo hii tena anasema anamkumbuka magufuli hata sielewi anasimamia wap
Ata wakiingia chadema lazima atakosoa tu, ukikosea anakuchana hanaga unafiki kama unaotaka wewe awe! anaamini katika uwajibikaji na usipowajibika anakukumbusha haijalishi wewe ni nan!? amkeni acheni uchawa
 
Back
Top Bottom