TCRA yatolea ufafanuzi sheria ya umiliki wa laini moja iliyoanza kutumika leo

naona wamefungia line za makampuni wakihisi ni mtu mmoja anamiliki line mingi (CUG closer use group)

zipo taasisi ambazo wafanyakazi wake wanatumia huduma ya CUG, nadhani hapa watarekebisha baadae
 
Huo ufafanuzi watu wanautolea wapi?
Hiyo sheria ilitungwa lini? Inawahusu na wale waliosajiri namba zaidi ya moja kabla sheria haijatungwa?
 
laiti Chakwera ndo angeshinda hapa kwetu, kwahiyo kazi ya ile fingerprint ya nida ilikuwa nini serikali woga kama hili sijawahi ona
 
... halafu hayo ni maelezo ya huyo afisa wa TCRA aliyekuwa anahojiwa; sheria haitamki hivyo; haiko wazi kwenye hilo; haitoi hiyo provision! Wanaotunga hizi sheria sijui wanakuwa wamesinzia?
walikuwa ccm siunazijua akili zao zinawaza tu kula,kusifu na kuabudu
 
Vyama mbadala chukueni hii changamoto muiweke kwenye ilani zenu ili sie tusiopenda kuburuzwa tupate pa kuhemea🙂
 
sasa maana ya fingerprint za NIDA ni nini.

Hii nchi kwenye mambo tunayopiga hatua mbela hapakosekani mtu wa kiturudisha hatua mbili nyuma.

Yani huyo kiongozi wa tcra sijui mwakanani kaona tcra pamepoa kaamua tu kuamka asubuhi na kuleta sheria za ajabu ajabu ilimradi asikike tu, Huu ni ushamba!!.

Kile kipindi tulipokuwa tunasajili laini hata tano kwa vitambulisho tofauti tofauti ndio hii sheria ilibidi itumike kwasababu ya uhalifu mwingi mitandaoni.

Ila sasa hivi kweli inaingia akilini ninasajili line zangu kwa alama za vidole alafu kiongozi moja huko tcra kaamka anavyojijua yeye katunga sheria kwa kakichwa kake kamoja kutuletea kero watanzania.

Naposajili line kwa fingerprint inamaana utambulisho wangu kwa laini hata zikiwa kumi ni ule ule, sasa ya nini tena tunaanza kuminyana tena kwa sheria hizi za kijinga, mbaya zaidi zimetungwa na tcra tunaodhani wapo mbali kiteknolojia na wanajua umuhimu w afingerprint.

Kitu kingine kinachonipa wasiwasi na huyu kiongozi wa tcra ni kama ana cheti cha kughushi, hivi sheria inaanzaje kutumika leo na adhabu zinaanza leo leo bila kutoa mda kwa wenye lain zaidi ya moja waende ofisi za mitandao kuzifungia line zao za ziada au kwenda tcra kuomba fomu za kuruhusu lain zaidi ya moja

huyu kiongozi ni Jipu.
 
Hata wakisema tubaki na laini 1 kushughulika nayo inaweza kuwa ngumu tu, mwishowe watasema kumiliki laini ni mwisho yaani hautakiwi kuwa na lain yeyote isipokuwa umetoa maelezo kwanini umiliki laini moja, dunia inapiga hatua mbele kudeal matatizo kitechnolojia wao wanarudi nyuma kukimbia tatizo.
 
Kwa upande wangu leo ndo nimeona taarifa kwamba Kuna sheria ilitungwa na kupitishwa na Bunge kuwa kuanzia leo haruhusiwi mtu kumiliki laini zaidi ya moja za mtandao mmoja mfano Vodacom.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa kama ukitaka kuwa na laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja utapaswa kuitolea maelezo laini ya ziada.

Tunaitaka Serikali itoe maelekezo kwamba ni wapi mtu akitaka kutolea maelezo laini ya ziada atapaswa kwenda ofisi zipi.

Maelekezo haya yanapaswa kulenga Tanzania kwa ujumla na siyo Dar es Salaam pekee.
 
Waliotunga hii Sheria walivuta bangi ya Wapi sijui, Wana Mambo mengi ya ku deal kuliko hyo minor issue, mtu hata akiwa na line Mia hajazifanyia uhalifu shida ni Nini?
 
Huyo mkurugrnzi naona hajui kazi, yake na kakurupuka maana ya kusumbua watu na NIDA ilikuwa Nini Sasa, TCRA Kama chombo Ina Mambo mengi muhimu kuliko kuanza kuchosha watu kujaza ma form na tayari wamejisajili kwa finger print. Hizi nafasi nyingine wawe wanatafutwa watu wenye exposure wanaofikiria mbele kuliko wanaofikiria kinyume nyume.
 
Huyu kiongozi wa TCRA lazima ana shida mahali hivi hzo form mtu anazipata wapi, why kusumbua Raia eti ujieleze kwanini una line nyingi?

Fa fa fa kupata vyeo vikubwa ni janga, Mimi wanifungie tu hyo line na Sina fine
 
Sheria ipo ndio na inakataza Kama ulivyosema kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja.

Sehemu ya kuitolea maelezo ni lazima iwe ni TCRA kwani wap ndio wanaofanya kazi ya ku-regulate mawasiliano ya simu.

Kumbuka kuna mikataba kati ya makampuni ya Simu Mfano Airtel na kampuni Kama COCA-COLA ambao wafanyakazi wake wote wanapewa laini za simu za mtandao huo na kuwa recharged kila mwezi.

Hivyo moja kati ya maelezo unayotakiwa kutoa ni;

Mimi nilikua na laini ya Airtel kabla sijaajiriwa Coca-Cola. Au nahitaji laini ya Airtel kwa matumizi yangu binafsi sio ya kampuni.

Wasalaam
 
Wewe ni mwanasiasa wa Ufipa?
😀 Hapana mkuu. Line mbili za tigo zinatumika kwenye vifaa vingine ambavyo sio simu. Moja ya halotel anatumia dogo, hizo nyingine ni mazingira tu yalinifanya nikawa nazo.
Niliwauliza Kama naruhusiwa kusaji line zaidi ya Moja mtandao mmoja wakasema inawezekana.
 
Inakuaje watu tuliowapa madaraka wanatutesa hivi? Wapo madarakani warahisishe maisha yetu au kuyafanya yawe magumu? Wanafaidika nini hasa wakishatuumiza. Kama kazi imewashinda wakae pembeni wawaachie wengine.
 
hawa wote c akili zao zimewekwa kwenye mfuko moja na mweyekiti wa ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…