TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

Kabda ya Wasafi media mwaka 2017 jun 16 huyohuyo alitoa huyo hukumu ( sipendi kumtaja kwa jina) alitutamkia kuwa "Leseni (kibari) cha kulusha matangazo ( kufungua) Radio na tv kwa Der-es salaam hakitolowi tena nafasi zimejaa " tulipokuwa tunafatilia kibali hicho. Baadae tunaskia Wasafi wamepewa, dah! Nikachoka . Kufuatilia naambiwa Mtia nia wa Kigamboni amehusika .

Nachotaka kueleza hapa ni kwamba taasisi na kampuni nyingi za kitanzania huwa tumia watu walio kwenye mamlaka (aidha kwa kuwapa rushwa au kwa ukaribu wake na watu hao) kuwapitia mbele katika kufanikisha masuala flani hata kama ni kinyume na taratibu. Sasa baadae kampuni/taasisi hizo hujiaminisha kupitia mtu wao huyo au ukaribu na kiongozi flani kwamba hakuna wakuwagusa.

Sasa inapotokea mambo yamewageuka na haki inapotendeka huisi wanaonea wanasahau kuwa kipindi wanakiuka sheria kuna watu wamedhurika
 
Kwa mujibu wa chadema, hiyo haki yao wanapaswa kuachwa tu!

Ndio maana hata mgombea wao anaona ushoga ni ishu ya faragha hivyo atawacha tu wafuasi wake wafanya watakavyo.


Kwa akili za wana chadema mtu akikosea kama hivyo aachwe tu ili mabebeu wasikunyime misaada.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo ni kutokana na kituo hicho kukiuka kanuni namba 11 ya Kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya mwaka 2018.

Mhandisi Kilaba amesema kuwa ukiukwaji huo wa kanuni ulifanyika katika vipindi vya The Switch na Mashamsham.

Aidha, ametoa rai kwa vyombo vya habari kuzingatia kanuni za utangazaji wa maudhui yenye lugha ya staha kwa Watanzania huku akiitaka Wasafi FM kuomba radhi kwa umma wa Watanzania.

My Take:
Viongozi wenye dhamana TCRA tusiishi kwa kukariri, mnaweza kuwapiga faini kama onyo kuliko kila kosa dogo mnafungia tu hamjengi bali mnabomoa.
 
😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Are you team kiba?
 
Kumbuka sasa hivi huyo mlezi wao yuko out of system.
 
TCRA wapo sahihi kabisa, hiyo adhabu wanastahili.
 
Mchawi akimaliza kula watoto wa jirani hugeukia wanawe. Hiyo ndiyo dhambi ya ubaguzi asili yake🤣🤣
 
Hivi TCRA makucha yao yanaishia tu kwenye chombo kilichoboronga na siyo hadi kwa mtangazaji aliyeongea lugha ya kutia kichefuchefu kwenye chombo hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…