TEC jitokezeni mapema kutoa ufafanuzi juu ya huu upotoshaji unaoendelea duniani, na pia nchini mwetu kuhusu kauli ya Papa.

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
33,092
Reaction score
96,127
Chonde chonde Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Tanzania (TEC)! Jitokezeni mapema kutoa ufafanuzi juu ya kauli ya Papa ya kuwaruhusu Mapadre wetu kubariki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Hiyo kauli yake pamoja na huo waraka wake alioutoa bila shaka mnafahamu ni kwa namna gani umeleta mtafaruku duniani kote. Na ndani ya nchi yetu mnaona ni kwa namna gani maadui wa Kanisa wanavyoitumia hiyo kauli yake kulichafua Kanisa la Mungu!

Rai yangu kwenu ni kuwaomba mjitokeze haraka na kutoa ufafanuzi wa kina. Maana mnatambua fika imani yetu, na pia mila na desturi zetu kwa ujumla wake; hazitambui vitendo vya aina hiyo.

Hivyo kama itabainika ni kweli Papa anahamasisha kuwatambua Mashoga na Wasagaji kwenye Kanisa Katoliki, ni bora tukajitenga tu na kuanzisha Kanisa letu; kama ilivyo kwa wenzetu wa KKKT.

Mwisho kabisa naamini hili ni jaribu dogo sana kwa Kanisa, ukikinganisha na majaribu mengine makubwa ambayo Kanisa lilipitia huko nyuma. Hivyo nikiwa kama muumini wa Kanisa, naamini tutalishinda.
Tumsifu Yesu Kristu.
Ni mimi Tate Mkuu, Padre niliyekimbia kiapo cha Useja. Naomba kuwasilisha.✍️🙏
 
Ili suala ukitumia akili utaona Papa yupo sahihi kwa 100% kwa sababu kuna kitu watu wanashindwa tu kujua na kuelewa kwa nn kabariki .
 
Sasa unashangaa nini wewe mkatoriki wakati kiongozi wenu kawaruhusu mpelekeane moto waume kwa waume mkizibuana mitaro!
 
Unataka Tec ifanyie kazi mihemko ya waislam na watesi wake?

Kuelezea upotoshaji tayari unaingia kwenye mtego wa maadui wa kanisa

Hakuna sehemu Papa amesema huo upotoshaji ni upotoshaji wa Bbc kubadilisha maneno


Kanisa limewahi kupitia vipindi vigumu kuliko huu utoto wa mitandao I


Kanisa ni moja na la mitume halitayumba kwa mihemko ya wasio jua hata imani yao


Ukiona mkristo anapokea mambo ya mitandaoni kuhusu imani yake naye aanze kulitukana kanisa huyo sio mkristo ni mpinzani
 
Kwahyo kujitenga umeona ni moja ya suluhisho Mkuu..?

HIZI IMANI ZA KULETEWA ZINA MAMBO MENGI SANA YA KUSTAAJABISHA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Kwa mtazamo wangu naona ni sahihi pia. Kwa sababu Kanisa Katoliki ni universal. Na kutokana na hilo, ndiyo changamoto kama hizi zinaanza kujitokeza.

Kwa nchi zilizoendelea, masuala ya LGBTQ ni jambo la kawaida. Ila kwa nchi za ulimwengu wetu, huu ni ushetani. Kwa hiyo katika mazingira ya aina hii, hatuwezi kuwa wamoja.
 
Sahihi kabisa. Na Mapadre/Maaskofu waruhusiwe kuoa. Huku Watawa nao wakiruhusiwa kuolewa. Haya mambo ya useja kwa mwanaume aliyekamilika, ni kudanganyana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…