Yesu alipofufuka alihubiri siasa!?..TEC wameichoka CCM au mtawala muislam!?..
Machafuko yote duniani husababishwa na wana siasa, tena wa vyama tawala, wana siasa pia ni waumini wa dini, sio wapagani na ndio maana nao wana apa kwa kutumia vitabu vya DINI. Moja kati ya kazi za wachungaji (sijui kuhusu ma sheikh ) ni kutoa tahadhari waonapo hatari inakuja, wasipo fanya hivo watahukumiwa na mwajiri wao. Nitakupa mifano michache ya manabii walio kemea watawala/wana siasa, wengine waliuawa na wana siasa kwasababu ya kukemewa maovu yao.
1. Yohana mbatizaji (Yahaya kwa Kiislam) aliuawa kwa kukatwa shingo yake kwasababu alimkemea mtawala wa wakati huo kwa kupora mke wa kaka yake.
2. Nabii Yeremia/Jeremiah aliiona tahadhari ya taifa lake kuvamiwa na taifa jirani, aliwakemea sana wana siasa kwamba warekebishe mambo or else watapigwa vibaya na miji yao kubomolewa na vijana wao watachukuliwa mateka, mfalme atatobolewa macho; hawakusikia. Jerusalem ilivamiwa, ikapigwa na kupigika hasa, nyumba yao ya IBADA ilIvunjiliwa mbali, wakatekwa kwa kuto kuwasikilikiza manabii.
3. Nabii Yona nae pia alikwenda kuwaonya taifa jirani na taifa lake kuhusu maovu wanayo tenda, na hatari iliokua mbele yao, wana siasa wa nchi ile wakasikia, wakaelewa na wakaamuru ifanyike TOBA, wananchi wakawasikiliza viongozi wao na nchi ikaponywa na hatari.
Sijui niendelee au niachie hapa kwanza?
Issues ya No reforms No election kwasasa imeisha escalate, wana siasa wasishupaze shingo. Bahati mbaya, yeyote mwenye ana shauri jambo jema huaga anapewa CHAMA, sijui huaga ni kwanini? Kama wewe hapa, eti kwakua rais ni Mwislamu. Sio hawa maaskofu waliokua wanampa za USO mkatoliki mwenzao Magufuli? Miaka hata 5 haijaisha na una pretend kama hujui? Sio unafiki huo kweli? Sijui kwenye Uislam lakini kwenye Ukristo unafiki ni dhambi ya mauti