Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Mwananchi

Muktasari:

Watu wanne wamehukumiwa na kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kuiba runinga yenye thamani ya Sh400,000.

Dar es Salaam. Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.

Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.

"Jamuhuri walikuwa na mashahidi wanne pamoja na vielezo huku upande wa utetezi washtakiwa hao walijitetea wenyewe,"amesema Mwankenja.

Amesema mahakama hiyo imewatia hatiani kwa kifungu cha 287A ya kanuni ya adhabu kwa kuwa kulikuwa na uthibitisho la wizi, wakati wa tukio walitumia silaha aina ya panga na ilielekezwa kwa mtendewa.

Mwankenja alisema mahakama hiyo imezingatia kifungu cha 287A kinaainisha adhabu pekee ni kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema kutokana na kifungu hicho cha sheria mahakama hiyo imewahukumu washtakiwa wote kifungo cha miaka 30 jela na kama hawajaridhika na maamuzi hayo wakate rufaa katika mahakama Kuu.
 
Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.

Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.

MWANANCHI
 
Serikali Tanzania:

1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.

2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.
It's craze mkuu na hawa watawala wanatuchukulia sisi ni mizuzu, hukumu gani hii huu ni ushenzi wa hakimu kwa kuonea vidagaa huku mipapa ikivuruga nchi, hukumu ya kipumbavu
 
Serikali Tanzania:

1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.

2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.
Fisasi hakati mtu na mapanga baada ya kuiba tena akibanwa anarudisha kwenye

Panya Road anaiba lakini .pamoja na kuchukua chako haridhiki lazima akukate Kate na mapanga akutoe kilema au kukutoa roho bila huruma

Chako kiondoke na mapanga upigwe miaka 30 wamewahurumia ilitakiwa wawanyonge
 
bado sio hoja ya kuwaonea huruma. Kinachouma zaidi hawa majamaa sio wanakuibia tu bali wanakudhuru, hawachelewi kukipiga mapanga. Safi sana
Kaka hakuna anaewaonea huruma wezi, jamaa anamaanisha ili ufanikiwe kwenye uwizi bongo piga mabilioni, kwa taarifa yako hao mafisadi wanaoiba hela za madawa, hela za kununua ambulance, hela za kujenga vituo vya afya nk. Unazani wamesababisha madhara na mateso kwa watz wangapi?
 
Back
Top Bottom