Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

Wewe utakuwa panya Road

Mtu anachuka TV hata ingekuwa ya elfu 10.halafu anamkata na mapanga aliyemwibia unamwita kidagaa muuaji kama huyo?

Huyo ni jambazi sugu linalotumia silahaiwe panga,shoka kisu,Wembley nk

Muuaji.huwezi ita kidagaa

Wewe utakuwa panya road au kiongozi wa panya road
Panya Roads ndani ya JF!!!
 
Ibeni mabilion kwa mamilion

Hamtafungwa

Ova
 
Mwendo wameumaliza hao, ripoti ya CAG waliokwapua billions of money wanabadilishwa vitengo wanadunda mtaani
Serikali Tanzania:

1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.

2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.
Kwa hiyo wezi wanaoiba kwa kutumia silaha waachwe kisa ripoti ya CAG?

Mbona siasa zinawatoa akili kiasi hiki
 
It's craze mkuu na hawa watawala wanatuchukulia sisi ni mizuzu, hukumu gani hii huu ni ushenzi wa hakimu kwa kuonea vidagaa huku mipapa ikivuruga nchi, hukumu ya kipumbavu
Nenda kawakatie rufaa, uwaambie wana haki ya kuiba na kukata watu mapanga sababu serikali pia inaiba
 
Wangeiba tu ningewatetea. Lakini kitendo cha kumkata panga wanastahili hiyo adhabu. Wapumbavu kabisa. Lakini pia-kwa nini wajitetee wenyewe, si wanasema kama huna wakili serikali inakupatia!!? Au ni habari ya majuu tu huko?
 
Hilo panga ndio limewapa miaka 30, TV peke yake wangepewa miezi sita tuu na kuilipa
 
Mwananchi

Muktasari:

Watu wanne wamehukumiwa na kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kuiba runinga yenye thamani ya Sh400,000.

Dar es Salaam. Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.

Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.

"Jamuhuri walikuwa na mashahidi wanne pamoja na vielezo huku upande wa utetezi washtakiwa hao walijitetea wenyewe,"amesema Mwankenja.

Amesema mahakama hiyo imewatia hatiani kwa kifungu cha 287A ya kanuni ya adhabu kwa kuwa kulikuwa na uthibitisho la wizi, wakati wa tukio walitumia silaha aina ya panga na ilielekezwa kwa mtendewa.

Mwankenja alisema mahakama hiyo imezingatia kifungu cha 287A kinaainisha adhabu pekee ni kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema kutokana na kifungu hicho cha sheria mahakama hiyo imewahukumu washtakiwa wote kifungo cha miaka 30 jela na kama hawajaridhika na maamuzi hayo wakate rufaa katika mahakama Kuu.
...Yaani ni Kila Mwizi anfungwa Miaka 30 yake ? Au ni Miaka 30 gawanya Kwa Wahalifu Wanna ambapo Kila mmoja atatumikia Miaka Saba na Nusu ? Au....?
 
Hukumu haiko sawa!
Kati ya hao wanne ni yupi hasa alitumia panga? Huyo ndio ale 30.
Ikiwa wote walitumia panga ni sawa watumikie
Sio kazi ya mahakama kujua yupi alitumia panga wewe utakuwa panya road

Vitani kikosi cha jeshi chaweza au defender yaweza kuwa na bunduki moja humo.ndani kuna kamanda ,msaidizi wa kamanda ,koplo nk waelekeza mtu apige na apige wapi

Panya Road huwa kikosi kamili

Kikosi chai chote kilitakiwa kunyongwq sema wewe kama umenusurika shukuru

Lakini iko siku utadakwa tu kwa kuwemo hicho kikosi cha panya road waliokuwemo kwenye hilo tukio wakasepa

Ili uunganishwe kwenye hukumu
 
Serikali Tanzania:

1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.

2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.
Fisadi anaumiza nchi, kibaka anaumiza mtu.
Fisadi atazungusha hela itarudi mtaani SAsa kibaka ana faida gani
 
Back
Top Bottom