Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

Mwananchi

Muktasari:

Watu wanne wamehukumiwa na kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kuiba runinga yenye thamani ya Sh400,000.

Dar es Salaam. Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.

Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.

"Jamuhuri walikuwa na mashahidi wanne pamoja na vielezo huku upande wa utetezi washtakiwa hao walijitetea wenyewe,"amesema Mwankenja.

Amesema mahakama hiyo imewatia hatiani kwa kifungu cha 287A ya kanuni ya adhabu kwa kuwa kulikuwa na uthibitisho la wizi, wakati wa tukio walitumia silaha aina ya panga na ilielekezwa kwa mtendewa.

Mwankenja alisema mahakama hiyo imezingatia kifungu cha 287A kinaainisha adhabu pekee ni kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema kutokana na kifungu hicho cha sheria mahakama hiyo imewahukumu washtakiwa wote kifungo cha miaka 30 jela na kama hawajaridhika na maamuzi hayo wakate rufaa katika mahakama Kuu.
Huyu hakimu
 
IMG_20230424_150934.jpg



Le_Fisadi
 
It's craze mkuu na hawa watawala wanatuchukulia sisi ni mizuzu, hukumu gani hii huu ni ushenzi wa hakimu kwa kuonea vidagaa huku mipapa ikivuruga nchi, hukumu ya kipumbavu
Wewe utakuwa panya Road

Mtu anachuka TV hata ingekuwa ya elfu 10.halafu anamkata na mapanga aliyemwibia unamwita kidagaa muuaji kama huyo?

Huyo ni jambazi sugu linalotumia silahaiwe panga,shoka kisu,Wembley nk

Muuaji.huwezi ita kidagaa

Wewe utakuwa panya road au kiongozi wa panya road
 
Watu wanne mnaenda kumkata mtu mapanga mumuibie tv ya laki 4 kweli?
Mkigawana kila mmoja anachukua laki upumbavu gani huo.
Mnakamatwa mnafungwa miaka 30.
Miaka 30 hao watakula ugali maharage bure kodi zetu.
Bora wanyongwe tu
 
Watu wanne mnaenda kumkata mtu mapanga mumuibie tv ya laki 4 kweli?
Mkigawana kila mmoja anachukua laki upumbavu gani huo.
Mnakamatwa mnafungwa miaka 30.
Miaka 30 hao watakula ugali maharage bure kodi zetu.
Bora wanyongwe tu
Tv laki nne, Bei ya kimtaa inaweza uzwa hta 150000 c unajua tena wazee wa Kazi hawana muda wa kupoteza??
 
Back
Top Bottom