Televisheni ya Sh400,000 yawapeleka miaka 30 jela

Kabisa hawawezi kuuza laki 4 , ikizidi sana laki 2.
Wakigawana 50 ujinga mwingi sana.
Mnaenda kumuumiza mtu kwa hiyo hela.
Ficha ujinga wako huko so ulitka waachiliwe?? Haijawah kabwa roba au kuibiwa??? Bora wale mafisadi wanatuibia pasipo kuona madhra yake direct.... Jizii hpo hpo unapta maumivu makali na tyari kashakurudisha Nyuma.... Hpana aisee
 
Tena sio wezi tu na wamejeruhi. Yaani wanaiba mali ya mtu na bado wanamwachia majeraha.
Tena ingetakiwa na wao wanyongwe tu imagine jambo lako umelitolea jasho mtu akuibie na kukukata mapanga ka si ushetani Nini huo
 
Mwananchi

Muktasari:

Watu wanne wamehukumiwa na kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kuiba runinga yenye thamani ya Sh400,000.

Dar es Salaam. Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.

Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.

"Jamuhuri walikuwa na mashahidi wanne pamoja na vielezo huku upande wa utetezi washtakiwa hao walijitetea wenyewe,"amesema Mwankenja.

Amesema mahakama hiyo imewatia hatiani kwa kifungu cha 287A ya kanuni ya adhabu kwa kuwa kulikuwa na uthibitisho la wizi, wakati wa tukio walitumia silaha aina ya panga na ilielekezwa kwa mtendewa.

Mwankenja alisema mahakama hiyo imezingatia kifungu cha 287A kinaainisha adhabu pekee ni kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema kutokana na kifungu hicho cha sheria mahakama hiyo imewahukumu washtakiwa wote kifungo cha miaka 30 jela na kama hawajaridhika na maamuzi hayo wakate rufaa katika mahakama Kuu.
wafungwe tu maana wanaweza hata wakaua kwa sababu ya kutaka hiyo tv ya 400,000 na wakaenda kuiuza kwa hata laki mbili
 
Ficha ujinga wako huko so ulitka waachiliwe?? Haijawah kabwa roba au kuibiwa??? Bora wale mafisadi wanatuibia pasipo kuona madhra yake direct.... Jizii hpo hpo unapta maumivu makali na tyari kashakurudisha Nyuma.... Hpana aisee
Umeelewa nilichoandika we kima?
Hata umesoma ukaelewa nazungumzia nini.
Nyie wakuja humu mnatokeaga wapi.
Pumbavu sana
 
Fisasi hakati mtu na mapanga baada ya kuiba tena akibanwa anarudisha kwenye

Panya Road anaiba lakini .pamoja na kuchukua chako haridhiki lazima akukate Kate na mapanga akutoe kilema au kukutoa roho bila huruma

Chako kiondoke na mapanga upigwe miaka 30 wamewahurumia ilitakiwa wawanyonge
Kabisa kunyongwa mpaka mavi ilitakiwa hukumu isome hivyo
 
Hawa madogo wamesumbua sana watu wacha wewe mfano ili kutomeza mambo ya panya Road lazima washughulikiwe
ingekuwa ni hivyo kesi za mauaji zingekuwa hazipo kabisa kutokana na hukumu yake ya kifo!!Mbona adhabu kama hizo hazitolewi kwa mafisadi!!hiyo mifano ni kwa wagonga ulimbo tu!!!??
 
Serikali Tanzania:

1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.

2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.
Mtu anaiba billions of dollars anahukumiwa jela au kulipa million 5 Tshs tu.......hao wameiba tivi tu,miaka 30? Hao ilitakiwa wapewe adhabu ya kutumikia jamii tu kama kufanya usafi kwenye hospital,Ofisi za Umma, Barabara,kuzoa taka kwenye masoko Kwa mwaka mmoja hivi......Mahakimu na wao wako stressed sana
 
Hii ndio solution tu bila kujali status au cheo itaondoa hili tatizo sugu
Tulitegemea Jiwe angefanya vile ila yeye ndo akawa mwizi zaidi.
Aliyepo sasa anawaona ndo walimsaidia kuwa Namba 6
 
Mwananchi

Muktasari:

Watu wanne wamehukumiwa na kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kuiba runinga yenye thamani ya Sh400,000.

Dar es Salaam. Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.

Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.

"Jamuhuri walikuwa na mashahidi wanne pamoja na vielezo huku upande wa utetezi washtakiwa hao walijitetea wenyewe,"amesema Mwankenja.

Amesema mahakama hiyo imewatia hatiani kwa kifungu cha 287A ya kanuni ya adhabu kwa kuwa kulikuwa na uthibitisho la wizi, wakati wa tukio walitumia silaha aina ya panga na ilielekezwa kwa mtendewa.

Mwankenja alisema mahakama hiyo imezingatia kifungu cha 287A kinaainisha adhabu pekee ni kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema kutokana na kifungu hicho cha sheria mahakama hiyo imewahukumu washtakiwa wote kifungo cha miaka 30 jela na kama hawajaridhika na maamuzi hayo wakate rufaa katika mahakama Kuu.
Tanzania kichwa cha mwendawazimu kama alivuosemaga mh. mmoja yaani Screen ya 400k miaka 30 jela lkn majizi ya mabilioni wapo uraiani na wanaendelea kutuongoza😭
 
Mtu anaiba billions of dollars anahukumiwa jela au kulipa million 5 Tshs tu.......hao wameiba tivi tu,miaka 30? Hao ilitakiwa wapewe adhabu ya kutumikia jamii tu kama kufanya usafi kwenye hospital,Ofisi za Umma, Barabara,kuzoa taka kwenye masoko Kwa mwaka mmoja hivi......Mahakimu na wao wako stressed sana
Maisha hayako fair always
 
Vp wale waliotajw na C.A.G.

wanakwambia ukiiba iba kweli itakusaidia kuhonga hata mahakam***** kuliko kuib kuku
 
Fisasi hakati mtu na mapanga baada ya kuiba tena akibanwa anarudisha kwenye

Panya Road anaiba lakini .pamoja na kuchukua chako haridhiki lazima akukate Kate na mapanga akutoe kilema au kukutoa roho bila huruma

Chako kiondoke na mapanga upigwe miaka 30 wamewahurumia ilitakiwa wawanyonge
Hahahahahah wanyongelewe mbali ili wazee wa haki za binadamu waingilie kati.
Fisadi ni mbaya kuliko huyo panyaroad ni vile tu huwa tunapuuzia. Ila katika watu ambao tulitakiwa tumalizane nao ni hao wezi wa kwenye ma V8
 
Hukumu haiko sawa!
Kati ya hao wanne ni yupi hasa alitumia panga? Huyo ndio ale 30.
Ikiwa wote walitumia panga ni sawa watumikie
... ukishiriki kufanikisha uovu na wewe umetenda uovu! Wote walikuwepo eneo la tukio na walibeba tv na kutokomea nayo halafu unasemaje hukumu haiko sawa.
 
Back
Top Bottom