Panya Roads ndani ya JF!!!Wewe utakuwa panya Road
Mtu anachuka TV hata ingekuwa ya elfu 10.halafu anamkata na mapanga aliyemwibia unamwita kidagaa muuaji kama huyo?
Huyo ni jambazi sugu linalotumia silahaiwe panga,shoka kisu,Wembley nk
Muuaji.huwezi ita kidagaa
Wewe utakuwa panya road au kiongozi wa panya road
Walimkata nani panga la kichwa?Mwendo wameumaliza hao, ripoti ya CAG waliokwapua billions of money wanabadilishwa vitengo wanadunda mtaani
Mwendo wameumaliza hao, ripoti ya CAG waliokwapua billions of money wanabadilishwa vitengo wanadunda mtaani
Kwa hiyo wezi wanaoiba kwa kutumia silaha waachwe kisa ripoti ya CAG?Serikali Tanzania:
1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.
2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.
Tatizo ni kwamba wanaiba kwa mujibu wa sheria, yaani kuna mianya kwenye sheriaNchi ngumu sana hii. Mtu anapiga bilioni za kutosha! Bosi wake anaishia kulalamika tu na kutukana hovyo.
Nenda kawasaidie kukata rufaa, sababu ni ripoti ya CAGNchi ngumu sana hii. Mtu anapiga bilioni za kutosha! Bosi wake anaishia kulalamika tu na kutukana hovyo.
Nenda kawakatie rufaa, uwaambie wana haki ya kuiba na kukata watu mapanga sababu serikali pia inaibaIt's craze mkuu na hawa watawala wanatuchukulia sisi ni mizuzu, hukumu gani hii huu ni ushenzi wa hakimu kwa kuonea vidagaa huku mipapa ikivuruga nchi, hukumu ya kipumbavu
...Yaani ni Kila Mwizi anfungwa Miaka 30 yake ? Au ni Miaka 30 gawanya Kwa Wahalifu Wanna ambapo Kila mmoja atatumikia Miaka Saba na Nusu ? Au....?Mwananchi
Muktasari:
Watu wanne wamehukumiwa na kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kuiba runinga yenye thamani ya Sh400,000.
Dar es Salaam. Wakazi wanne wa eneo la Charambe wamehukumiwa kwenda miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
Waliohukumiwa ni Samwel Chacha (20), Haji Ally (24), Athuman Halfan (25) na Sadid Seif (19) wote ni wakazi wa Charambe.
Inadaiwa kubwa Februari 8, 2022 eneo la Charambe kwa Mbiku waliiba luninga yenye thamani ya Sh400,000 mali ya Yahama Ngingile kabla na baada ya kufanya wizi huo walimkata na panga kichwani.
Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani kwa kosa hilo ambapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka lolote.
"Jamuhuri walikuwa na mashahidi wanne pamoja na vielezo huku upande wa utetezi washtakiwa hao walijitetea wenyewe,"amesema Mwankenja.
Amesema mahakama hiyo imewatia hatiani kwa kifungu cha 287A ya kanuni ya adhabu kwa kuwa kulikuwa na uthibitisho la wizi, wakati wa tukio walitumia silaha aina ya panga na ilielekezwa kwa mtendewa.
Mwankenja alisema mahakama hiyo imezingatia kifungu cha 287A kinaainisha adhabu pekee ni kifungo cha miaka 30 jela.
Amesema kutokana na kifungu hicho cha sheria mahakama hiyo imewahukumu washtakiwa wote kifungo cha miaka 30 jela na kama hawajaridhika na maamuzi hayo wakate rufaa katika mahakama Kuu.
Sio kazi ya mahakama kujua yupi alitumia panga wewe utakuwa panya roadHukumu haiko sawa!
Kati ya hao wanne ni yupi hasa alitumia panga? Huyo ndio ale 30.
Ikiwa wote walitumia panga ni sawa watumikie
Compared to mafisadi wa bilioni 50 za TCAA?Safi sana. Hao wapuuzi wanafanya maisha mitaani yanakua magumu sana. Hela shida na bado unaishi na hofu ya kukabwa na kupigwa mapanga.
Compared to mafisadi wa bilioni 50 za TCAA?
Huyo anaeiba billions hapigi mtu pangaNchi ngumu sana hii. Mtu anapiga bilioni za kutosha! Bosi wake anaishia kulalamika tu na kutukana hovyo.
Tena la kichwaNi haki yao.badala ya kuiba tu panga wewe hadi unakata mtu panga.
Fisadi anaumiza nchi, kibaka anaumiza mtu.Serikali Tanzania:
1.Raia mwizi wa TV, miaka 30 jela.
2.Raia Fisadi wa mabillioni ya serikali, mnaohusika naombeni mtupishe.