Tellers' kwenye benki zetu wanatuibia pesa zetu bila aibu

ATM zikivyoanza Dar zilikuwa zinakosea sana kutoa hela, mara nyingine zinakuongezea πŸ˜‚πŸ˜‚
Hahahaha me kwangu naona watu wajifunze kubadilika hasa kwenye malipo siku hz cash sio lzm sana πŸ˜‚ πŸ˜‚

Ila nimefurahi sehemu nyingi siku hizi ni lipa namba, ni bank account unalipia juu kwa juu aani, hata ille kuumiza kichwa kwa wingi wa cash inarahisisha,
 
i wafanyakazi wa benki wengi ni wezi uzuri waki shika huwa wana lambwa kweli kweli yani nyonywa hadi wapauke .
 
Wiki iliyopita kuna mtu alikuwa analalamikia makato.

Kutumia mifumo hiyo cashless hakuna makato makubwa kwenye miamala?
 
Wiki iliyopita kuna mtu alikuwa analalamikia makato.

Kutumia mifumo hiyo cashless hakuna makato makubwa kwenye miamala?
Makato yapo lakini kwangu Mimi naona ni rahisi zaidi maake gharama ya kutuma na kutoa always ya kutoa inakuwa juu, kwahiyo Bora kutuma ama kulipia ni rahisi kuliko kuhangaika na cash mara utembee kwa wasiwasi hizo naona taabu tupu
 
Rudi bank, kuna surveilance camera wanaweza kuona kila kitu kilichofanyika. Unapaswa kurudi mapema kwani kuna muda ukipita recordings zinafutwa.
 
January 2025 nilienda CRDB Mlimani City nikatoa 2M.

Nimefika kwa wakala nikampa pesa aniwekee kwa simu kila bando lilikuwa na upungufu wa 20,000, jumla nikapigwa 40K.


Namuuliza wakala una hakika? Tukarudia kuhesabu kwa machine na kwa mkono na ikawa imekula kwangu.

Huwa wana zile bando za milioni moja moja ambazo ziko kando ambazo wameshachakachua. Muhimu usikubali akupe bila kuhesabu kwenye machine.
 
Mimi ilishawahi kutoiea, nilitoa mil 5. Teller aliniibia 50,000. Na pesa ilikuwa ya kulipia kiwanja. Tulipofika kwa wakili, wakili akashauri tuzihesabu bila kujali zimetoka benki. Niliaibika sana, kuona kila fungu la m.1, elfu kumi imechomolewa. It was crdb. Sheria inataka transparency and high integrity kwenye kazi za benki. Na kwa mujibu wa sheria, tellers hao wanatakiwa kula kiapo wanapoajiriwa, cha kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.
 

Kmmmke kakuangalia usoni.

Kwa mimi, Kesho asubuhi ningeenda kulitifua.

Kuna siku nikaenda bank kuchukua mil 1.2

Sababu ya haraka (supplier wa bidhaa alikuwa nje ananisubiri) nikapewa hela na teller mi nikazichukua na kwenda kumkabidhi supplier.

Usiku wake supplier anasema "Ilipungua 65k""

Aisee nilienda kuliamsha bank, mpaka leo wananijua.

USICHEZE NA HELA ZANGU MANGIIII
Cheza na Mav(i) yako ila SIO HELA YANGU.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kwa nini hukuangalia tarakimu zinazoandikwa kwenye machine? Au alikuwa anakuongelesha maneno matamu ukalegea wakati anafanya yake? Mwisho, hakukuwa na bango linalokutaka uhesabu kabla ya kutoka dirishani?
 
Sie wenye vibubu nyumbani hapa hapatuhusu.
Japo hoja ya msingi hii
 
Hizo tabia wanazo sana me niliwahi pigwa bank moja kati ya zile zilizomo mle mliman city nilianzisha vagi kesho yake mpaka wakanipatia , cha kufanya nenda kwa meneja muelezee kuna camera itaangalia muda na saa kisha wataona
 
Naomba kuuliza mwisho wa kutoa ATM ni shi ngp ? Na ukitoa Teller mean ukikuta zipo pungufu inakuaje?
Viwango vya kutoa ATM hutofautiana baina ya bank ila unaweza kuchukua hadi milioni moja na kuendelea kutegemeana na uratibu wa Bank husika.

Ukichukua kwa ndani ukapewa pesa sheria za Bank zote zinakutaka uhesabu pesa zako kabla ya kuondoka counter (pembeni ya dirisha la kuchukulia pesa). Ikiwa ukikuta ni pungufu una haki zote kisheria kurudi dirishani ulikochukua pesa ( tena kwa hasira za kimasai/kikuryaπŸ˜‚πŸ˜‚) na kumwambia kuwa pesa alizokupa ni pungufu. Km atakuwa siyo msumbufu na km atakuwa anajua alichokuwa amekufanyia atakupa kiasi kilichopungua tena kwa kukuomba msamaha wa kiwango cha VIP, (Ukikataa msamaha wake huyo teller atakalia kuti kavu). Tofauti na hapo utatakiwa kusubiri waangalie kwenye camera waone km wakati unahesabu hukuwafanyia ujanja. Wasipoelewa wewe ni kuwapeleka mahakamani tu ili sheria ifuate mkondo wake.

Iwapo utaondoka counter bila kuhesabu pesa zako, ukifika tu mlango wa kutokea ukashtuka ukasema urudi ndani kuhesabu upya, hapo hata ukikuta zimepungua inakuwa imekula kwako, hata ukienda na mzuka wa kimasai/ kikurya hupati hata mia mbovu ya nuongeza. Sanasana ukileta mikwara utakamatwa na walinzi na polisi wanaolinda hapo. Hiyo kesi lazima upigwe mvua ya miaka ya kutosha na si rahisi kuchomoka.

Ndo maana kila bank pale dirishani wameandika "count your money, before leaving".

NB: Usisimame dirishani kabisa wakati wa kuhesabu maana utazuia huduma kuendelea kwa wengine, simama pembeni ya hilo dirisha ili wengine waendelee kuhudumiwa.
 
Utaratibu hua mashine ya kuhesabia pesa ni lazima iwe imeelekezwa kwa mteja ili ahakikishe hesabu ya pesa zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…