Viwango vya kutoa ATM hutofautiana baina ya bank ila unaweza hadi milioni moja na kuendelea kutegemeana na uratibu wa Bank husika.
Ukichukua kwa ndani ukapewa pesa sheria za Bank zote zinakutaka uhesabu pesa zako kabla ya kuondoka counter (pembeni ya dirisha la kuchukulia pesa). Ikiwa ukikuta ni pungufu una haki zote kisheria kurudi dirishani ulikochukua pesa ( tena kwa hasira za kimasai/kikurya😂😂) na kumwambia kuwa pesa alizokupa ni pungufu. Km atakuwa siyo msumbufu na km atakuwa anajua alichokuwa amekufanyia atakupa kiasi kilichopungua tena kwa kukuomba msamaha wa kiwango cha VIP, (Ukikataa msamaha wake huyo teller atakalia kuti kavu). Tofauti na hapo utatakiwa kusubiri waangalie kwenye camera waone km wakati unahesabu hukuwafanyia ujanja. Wasipoelewa wewe ni kuwapeleka mahakamani tu ili sheria ifuate mkondo wake.
Iwapo utaondoka counter bila kuhesabu pesa zako, ukifika tu mlango wa kutokea ukashtuka ukasema uruhesabu upya, hapo hata ukikuta zimepungua inakuwa imekula kwako, hata ukienda na mzuka wa kimasai/ kikurya hupati hata mia mbovu ya nuongeza. Sanasana ukileta mikwara utakamatwa na walinzi na polisi wanaolinda hapo. Hiyo kesi lazima upigwe nvua ya miaka ya kutosha na si rahisi kuchomoka.
Ndo maana kila bank pale dirishani wameandika "count your money, before leaving".
NB: Usisimame dirishani kabisa wakati wa kuhesabu maana utazuia huduma kuendelea kwa wengine, simama pembeni ya hilo dirisha ili wengine waendelee kuhudumiwa.