Tellers' kwenye benki zetu wanatuibia pesa zetu bila aibu

Shukrani boss
 
Na mimi nimemshauri hivi hivi. Kama hawezi kwenda basi aandike hata email aelezee. Japo hawatakubali kuwa zilikuwa pungufu lakini zitawaogopesha wasirudie tena. Huwa wanamsoma mteja na wakiona hana mwelekeo wa kuhakiki wanampiga.
Teller anayekupiga mara nyingi ni yule uliyemzoea!! Anajua huna shaka nae!
 
Wanawekana hawana ethics za kazi kwahiyo lazima mambo kama hayo yatokee, wakati wanahesabu fedha wanaiba sana hata huko kwenye maduka ya kubadili fedha za kigeni.
 
CCM imefundisha UHUNI kila pahala.
 
Mkuu ukiripoti wanareview very simple na itaonesha namna gani alikuibia..
 

Sijawahi ibiwa kizembe hivi, unashindwaje angalia pale kwenye mashine ikihesabu? Au kuhesabu mwenyewe?
 
Na ndio maana wawekezaji wanawaajiri wageni.
Mbongo akiajiriwa cha kwanza wizi tu, siyo kufanya kazi kwa bidii au kuleta ubunifu kwenye kazi!
Wepesi kulalamika, misiba, kuumwa, visingizio na uvivu!
Manyang'au na waganda walipigwa vita sana sana, sasa wahindi na wachina!
Husuda, Majungu, domo domo, utendaji ZERO!
 
Umenikumbusha nmewah kupigwa li 10 na teller pale dodoma pesa za kutumwa peleka bank na tulihakiki pamoja na anko
 
Wengine wakati wa kuweka anadondosha hela chini. Unakuta kwenye bundle ya 500k au 1m kuna upungufu wa hela.
 
Hizo ni nyingi sana. angalia vizuri mkuu,inawezekana umezichanganya. bora angeiba noti mbili au moja ,noti 20 ni rahisi kugundulika

kama ni hivo hali mbaya sana .. serious and fraud ya kijinga sana

teller anatakiwa ahesabu hela kwenye mashine ukiwa unaangalia.hata kama ni bundle limetoka benki nyingine au bot
 
Asante sana mkuu. Elimu,elimu elimu "hesabu fedha zako kabla ya kuondoka counter". Uvivu ni kichocheo cha malalamiko na hasara.
 
Kosa ni lako mnajifanya mmeridhika,,, mimi huwa nazihesabu kabla ya kuondoka
 
Mkuu nimechambua mojamoja na kurudia mara mbilimbil hizo pesa hazipo.Tena sasa naanza kurudisha akili yangu nyuma kidodogo,kuna Dada mmoja alikuwa yupo Counter aliongea naye kwa kirefu sana wakati anamhudumia inaonekana wanafahamiana kwani walikuwa wanaongea na kufurahi mpaka wateja tuliokuwa tunasubiri huduma tukaanza kukasirika .Huyo dada alivaa nguo nyeusi.Sasa inaonekana ile ilikuwa njama ya kutuchosha makusudi ili ikifika zamu yetu tuwe na mawazo ya kuchukua fedha haraka na kuondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…