Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Hata sioni tatizo hapo wanataka muache kupoteza gharama kwenye mambo yanayoweza kufanywa simple na wanaopoteza muda na kufanya mambo makubwa walipe Kodi Ili watengenezewe miundo mbinu na huduma za jamii. Mpaka mbadilike mjue kuishi Kama ulaya mambo ya kupoteza muda Kama mnayo mlipie Kodi.
 
Usisahau ile mbinu ya awamu hii 'Tengeneza tatizo,kisha litatue".Usishangae Mkulu akatengua siku mbili na kama mazuzu tukashangilia tena kwa nguvu!
 
Duh! Wananchi tuliambiwa tutambue haki yetu na nguvu tuliyonayo katika kuiwajibisha serikali lakini wapi, tumejawa na uoga, unafiki na kutengenezeana majungu katika mambo yasiyokuwa na msingi.
Mitano teeeena au nasema uongo jamani?
 
Na viboko kwanza wamesahau kuongeza apo kodi ya uchafuzi wa sauti kila mtu afunguwe redio sauti ambayo jirani hawezi sikia kabisa wala mtu aliyepo nje kwako liwe kosa la jinai
 
Techinically kuna impact mbili hapo,
1) Kuna ma mc wadogo wataacha hiyo kazi maana costs zitakuwa kubwa kwao kumudu ukizingatia ujira wao.

2) Wale wakubwa watapeleka bei kwa mlaji ambayo kwa kiasi itaongeza gharama za u MC.

Kwa ufupi hii policy ita discourage zaidi, wenye vile visherehe vidogodogo
 
Mimi nafurahia sana haya mambo Sababu watz wengi bado hawajajitambua

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 

Hivi we unajua kwamba kumbi za sherehe zinalipa kodi. Hao ma MC wote unaowaona wamesajiliwa na wanalipa kodi.
 
Lipa kodi mzee
Serikali iko sawa kabisa kudai kodi hapo
Tena itakuwa vizuri walete kabisa kodi ya kichwa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Tunakoelekea hadi watembea kwa miguu watalipia kodi.Fursa hiyo kwa TANIRODI.
Dereva naomba niteremke nishafika kituo changu tafadhali.
 
Basi wazilenge hizo za mamilioni.
 
Harusi yangu itafanyika kwenye ukumbi uliopo Kambi ya Twalipo Mtoni Sabasaba. Hao mgambo waje "kunusa" hapo!
 
Yaani hata sisi wa huku "mbavu za Mbwa" tunaoishi chumba kimoja tumeamua kubariki ndoa....tukachangisha kupata ndoo mbili za mbege na kreti mbili za soda na banana kadhaa...Mwenye yumba kajitolea "venue" uwani kwake..Mc ni Mtoto wa Mjomba, Spika na kinasa sauti tumeazimwa na Mchungaji mwenye banda lake hapo jirani analoliita "Kanisa la vuguvugu".

Na sisi tunahusika na hizo kodi ama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ