Ni sawa kabisa! Unakuta sherehe kwa mfano ya harusi au sendoff watu mnachangishwa kila kichwa elfu hamsini mpaka laki moja,!
Unakuta sherehe moja tu ina gharimu mpaka milioni 10.
Unakuta kwenye bajeti ya sherehe eti
Mapambo milion 1.5
Ukumbi milion 1.2
Mc na music milioni 1.8
Picha na video milioni 1.6
Vinywaji milioni 1.7
Chakuala milion 4
Na hizi ni sherehe tu za uswahilini bado za ushuani ndio balaa
Unakuta mtu ana maisha magumu lakini akipewa kadi ya mchango anajipinda mpaka ipatikane, tena wanakuwekea masharti kabisa single 80,000 double 150,000.
Tena hili suala lilialamikiwa sana humu kwama ifike hatua hawa watu walipe kodi.
Walipe tu kodi aisee.