Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Or anaweza kutoza bei ya juu ili difference inayobaki baada ya kulipia kodi ikawa faida yake
 
Hayo ni maamuzi ya kwenye halmashauri madiwani wengi ni wapya kwenye siasa za maamuzi na wakurugenzi sio wanasiasa.

Isitoshe sio kila maamuzi ya siasa yanayogusa watu moja kwa moja ni sahihi ata kama yanafanywa na CCM.
Tusisingizie uzoefu hapo ni normal common sense tu kumfuraisha mfalme, kwanini wateuliwe watu wasio wazoefu huko
 
Walipe kodi hakuna shida, sajili watu wote hao as self employed na walipe kodi kupitia TRA kama biashara zingine that is understandable kwanza wengi mapato yao yanavuka threshold za taxable income kwa sheria na catering services nyingi za hizi sherehe na hayo ma-hall ni walipa kodi wa TRA tayari.

Issue hapa ni tozo za halmashauri ambazo wanataka wananchi ndio walipie zaidi kabla ya sherehe zenyewe.
 
Tusisingizie uzoefu hapo ni normal common sense tu kumfuraisha mfalme, kwanini wateuliwe watu wasio wazoefu huko
Vyanzo vya mapato ya halmashauri vinaanzishwa huko huko kwenye vikao vyao; ata Dr Mpango anaweza asijue kila halmashauri imekuja na tozo gani, let alone the president.

Na kama wanajua this is a bad one.
 

Mitano tena.
 
Safi sana but mbona viwango vipo chini hivyo?

Hivi hapa ndivyo vyenyewe sasa...

Ukumbi malaki 5
Chakula malaki 4
MC malaki 3
DJ malaki 2

Badala ya kuchangianaga kwenye mambo muhimu kama elimu, tiba, nk watu wanashobokeaga masherehe. Hiiiiiiiiiii!

Wacha wakomage kabisa kabisa wakufwage huko!
 
Tulia sindano ziingie ndg proMagufuli regime.
 
dah mbona hizo gharama za kodi ni ndogo sana kwa baadhi ya wahusikaa !

Ni jambo jema kwa namna moja ama nyingine kutafanya jamii kupunguza baadhi ya matukio ya sherehe na kuelekeza fedha kwenye mambo mengineyo ya kujenga familia / uwekezaji
Mkuu umeongea point.Walichofanya siyo kutanua uwanda wa kodi bali wamezifunga shughuli tajwa hapo juu kwa sababu ukitaka kutanua uwanda wa kodi inabidi kwanza uje na mbinu za kuongeza/kuimarisha pato la mwananchi halafu ndiyo uje na kodi.Ukileta kodi bila kuimarisha kipato cha mlengwa maana yake ni kuifunga shughuli husika ya mlengwa halafu kinachofuata ni economic colapse.Imagine hawa MC watakula wapi kama shughuli lengwa hizi zikifungwa/zikifa?Maana yake unemployment rate itaongezeka mara dufu halafu kutakuwa hakuna expenditures na hatimae uchumi unacolapse.Mimi huwa najiuliza serekali huwa haina wataalam wa kodi?!
 
Kuweka kiwango flat ni tatizo. Hao wanaolipwa wawe na efd kisha wanapopokea watoe risiti itozwe kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…