Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Hiki ndicho kitakacho tokea

Na chakushangaza zaidi mbona hao wapishi na wapiga picha wakati mwingine malipo yao huwa hayazidi hizo tozo walizoziweka au walikuwa wanzungumzia watu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu oneni jamani[emoji134][emoji1745][emoji1745]
 
Sherehe zatakiwa kulipiwa kodi au Mc na wapishi wa masherehe watakiwa kulipa kodi?
 
Hii sasa kali. Migambo itakuwa inachungulia madirishani kujua kama ndani kuna sherehe au la!!!!.
Ila katika ufafanuzi mwenye sherehe hajaguswa. Je nikifanya bila kumwalika MC, mpishi nitadakwaje?
... hujamweka MC, mpishi, DJ, mapambo, caterer, wala hujakodi ukumbi means hujafanya biashara so kimsingi kodi haipo.
 
Sherehe zatakiwa kulipiwa kodi au Mc na wapishi wa masherehe watakiwa kulipa kodi?
... nina kashughuli kangu ambako MC amekubali kunifanyia bei ya kishikaji elfu 25. Lakini anatakiwa alipie elfu 50 kodi. Kodi itakuwa imelipw na mimi mwenye shughuli au MC?
 
Sherehe nyumbani na kodi wapi na wapi
Wataanza hadi unyago na ngoma za mashetani
Kwa hiyo nyumbani chakula umejinunulia mwenyewe sokoni

Kuku umewatoa banda kwako la kuku ufanye kasherehe ka mtoto kutoka jando

MC mjomba wa mtoto unaenda dai kodi?

Huo ni uhuni kwa sherehe za krimasi na iddi zinszofanyika majumbani watu wanawake hadi mahema mtafuata kodi?

Watu wakiwa wana sherehe ya kupokea mahari au barua ya uchumba mtaenda? Huo ni udhañimu
 
... nina kashughuli kangu ambako MC amekubali kunifanyia bei ya kishikaji elfu 25. Lakini anatakiwa alipie elfu 50 kodi. Kodi itakuwa imelipw na mimi mwenye shughuli au MC?
Kwani unapoajiriwa ukalipwa chini ya kiwango cha mshahara kinachotakiwa kulipiwa kodi huwa tofauti analipa mwajiri?
Hiyo kodi analipa mc kwa sababu ni kipato kwake, kama hastahili kuilipa basi yatatolewa maelezo.
 
Hii sasa kali. Migambo itakuwa inachungulia madirishani kujua kama ndani kuna sherehe au la!!!!.
Ila katika ufafanuzi mwenye sherehe hajaguswa. Je nikifanya bila kumwalika MC, mpishi nitadakwaje?
Itabidi kukaa na mishale ndani ya nyumba. Nimealika ndugu zangu nyumbani kwa dinner ya kumpongeza mwanangu kupata kipaimara, nione dodoki linachungulia dirishani, mshale wa shingo. Hawa ndio vibaka wenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…