Tenzi za rohoni

Tenzi za rohoni

Ingawa mara ya mwisho kwenda Kanisani ilikuwa 2016 lakini hapo no 8 na 10 ni hatari sana.
 
Mwenyezi Mungu awabariki wote walioshiriki kutunga nyimbo hizi za TENZI ZA ROHONI.

Hizi ni baadhi tu ya nyimbo hizo zinazogusa moyo (Heart touching songs)
1.Mungu ni Pendo
2.Usinipite Mwokozi
3.Salama Rohoni
4.Yesu unipendaye
5.Mwamba wenye imara
6.Nataka nimjue Yesu
7.Bwana u sehemu yangu
8.Ni tabibu
9.Kumtegemea Mwokozi
10.Kaa nami
11.Bwana Mungu nashangaa kabisa.

Wakati mwingi unatembea au uko busy na shughuli zako unajikuta unaimba tu peke yako, unahisi amani ya ajabu ndani ya moyo wako.

Muwe na siku njema wana wa Mungu.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏
Kama wewe ni mlutheri kuna kitabu cha nyimbo za kwaya! Hizo nyimbo zinaimbwa kwa "note" ukizijua kuziimba ni nzuri kuliko maelezo! Hila ni uzembe wa watu kujifunza! Natamani siku moja kuanzisha kituo cha TV mahususi kwa ajili ya nyimbo za kiroho! Watu wengi wana msongo wa mawazo kutokana na kukosa nyimbo za kiroho! Nyimbo nyingi tunazosikia zinapigiria msumari stress
 
Duh kazi ipo,kweli kila mtu anaufahamu wake..Tuombe robo mtakatifu atuongoze kabla ya kunena
Mkuu hili sio swala la ufahamu wa mtu ni swala ambalo ni kanuni ya kawaida tu kwenye Ulimwengu wa roho watu wengi bado hawajajua bado ulimwengu wa Roho unavyo tenda kazi,
Ufahamu hawana wengi hata viongozi wetu wa kiimani pia,
Sisemi kwa ubaya au kujitukuza ila hua naumia sana kuona watu wengi sana bado wapo gizani
mambo madogo tu bado hawajayajua Bado inahitaji Neema ya MUNGU na kweli Ya Kristo iwafikie watoke huko maana Yesu alisema enendeni Ulimwenguni pote mkawafanye watu wawe Wanafunzi Ila ajabu sasa hao wanafunzi sasa wamekaa makanisani miaka Tele na bado hawaja hitimu still waMeshikiliwa na taratibu,Kanuni na Mapokeo ya kanisa still bado watumwa na hata Neno na Mambo ya msingi ni Zero kwao MUNGU ni kama Foreigner Na sio BABA tena
nakubaliana na wewe Ndugu ROHO MTAKATIFU atuongoze tujitambue na tUtambue Mamlaka tuliyopewa Katika jina La YESU!
 
Back
Top Bottom