Tetemeke la ardhi limetokea Bukoba leo alfajiri

Tetemeke la ardhi limetokea Bukoba leo alfajiri

Kama limepiga basi si 5.0 na inawezekana lipo chini ya 2.5.

Lingepiga la zaidi ya 2.5 USGS wangeliweka hapa.

Usije kuonekana huna akili kijana check hio picha afu twambie linaukubwa gani nahisi hata historia ya matetemeko yanayotokea bukoba huijui fatilia tetemeko lililowahi kupita hapo na nini kilitokea
 
Kwa nini wakimbie nje uchi.? Hawalali na mapajama? Au ukute tetemeko lime tokea na mtu ndiyo alikuwa on the way kukojoa.. stimu zina kata ghafla
 
Usije kuonekana huna akili kijana check hio picha afu twambie linaukubwa gani nahisi hata historia ya matetemeko yanayotokea bukoba huijui fatilia tetemeko lililowahi kupita hapo na nini kilitokea
Kwanza kabisa sijawahi kuwa na haja ya kuonekana nina akili.

Tusawazishe hilo awali ya yote.

Pili, tetemeko la ardhi halipimwi kwa kutazama picha, katika dunia hii ya AI picha mtu yeyote anaweza kutengeneza, na kama unapima tetemeko la ardhi kwa kutazama picha wewe ndiye akili zako zinahojika hapo.

Tatu, kama matetemeko yashawahi kutokea Bukoba haina maana ni lazima tetemeko litokee tena leo. That is a logical non sequitur fallacy.

Nne, matetemeko mengi yakitokea magnitude huwa inakuwa revised down baada ya muda si kitu unapima na kujua mara moja kwa uhakika.
 
Ndio ushangae hata hapo kigoma wapo TMA ila wameshindwa kudetect hawana akili wamekalia uchawa
Kwamba TMA wana deal na tetemeko..daah aiseee.CHADEMA kila kitu mnajua eti
 
Magnitude 5 ni himilifu. Moderate tu.

Ngoma inaanzia 6 hapo mnatafutana.
 
Kabla ya 2016 paliwahi kuwa na tetemeko?
Yes tetemeko hutokea ukanda huo ila sina kumbukumbu kama liliwahi pita la ukubwa ule, na babu alisema hajawahi kushuhudia tetemeko la ukubwa ule na wakati huo alikuwa na 94yrs,
 
Sehemu nyingine yenye matetemeko sana ni ukanda wa Arusha, manyara na singida, madogo madogo mengi hasa miezi ya August mpaka October
 
Sehemu nyingine yenye matetemeko sana ni ukanda wa Arusha, manyara na singida, madogo madogo mengi hasa miezi ya August mpaka October
Kuna kanda mbili za bonde la ufa. Lipo la Mashariki na lipo la Magharibi. Maeneo yaliyo kwenye bonde la ufa ndiyo yaliyo hatarini zaidi kupata matetemeko. Mikoa uliyoitaja kama Arusha na Manyara ipo kwenye upande wa Mashariki wakati Kagera inaangukia upande wa Magharibi.
 
Back
Top Bottom