Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Wataalamu hudai tetemeko la kwanza huwa si baya, matetemeko yafuatayo ndio mabaya maana hudondosha majengo yaliyolegezwa.

Mungu atuepushie mbali Tanzania maana tutarudi ujimani na itatuchukua miaka 50 kusimama...
Tobaaa

Mungu ni wa rehema.
Nchi zetu hizi za kimaskini tukipigwa lol sijui.
Mungu aepushie mbali.
 
Hiyo nimejisemea mimi mkuu kwasababu nikiona au kupata taarifa ya msiba ninalazimika kutamka maneno hayo lakini si maana mbaya, sisi ni wa allah na kwake tutarejea.
Nadhani kwakuwa umeandika kwenye platform inayosomwa na wengi na si wote wanaelewa kiarabu ndiyo maana amekushauri kutumia lugha inayoeleweka na wengi.
 
Yametokea matetemeko 2
Hivyo nyumba kadhaa zitaendelea dondoka baada ya kulegea kutokana na tetemeko la kwanza.

Kuna video zaonesha nyumba zikidondoka zenyewe
Kawaida huwa iko hivi: likitokea tetemeko moja kubwa lazima tena nyuma yake lifuatwe na matetemeko mengine madogo madogo (after-shocks), angalau moja au mawili. Ukubwa wa matetemeko haya madogo huwa unategemea ukubwa wa lile la mwanzo.

Kadri tetemeko la mwanzo linavyozidi kuwa kubwa, ndivyo kadri na matetemeko mengine madogo yatakayofuata yanavyozidi kuwa makubwa
 
Back
Top Bottom