Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Yawezekana Leo nikawa na nyinyi natesa hila Kesho nikala madawa na kuwa chizi wa meditation.

Nikama hukumu inaenda kukamilika
 
Nawaombea waathirika wote kwa ujumla Mungu awarehemu.

Ila ninasiki dokta mkuu na mfawidhi wamesimamishwa kazi?! 🤣 🤣 Kisa hawakwenda kwenye maeneo ya tukio, hawajatoa vifusi, hawajasaidia lolote. Ila vikosi vya uokoaji havijafika wala nini. Tunawaona madokta tu, sijui ni utaratibu au nini?!
 
Tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 7.9 limepiga katikati mwa Uturuki na Kaskazini-Magharibi mwa Syria siku ya Jumatatu, na kuua maelfu ya watu na kujeruhi mamia wakati majengo yakiporomoka


Uokoaji wa walionusurika kwenye vifusi katika eneo hilo lenye theluji unaendelea.

Shirika la maafa la Uturuki limesema watu 76 wameuawa, na 440 wamejeruhiwa, wakati mamlaka ilipotawanya timu za uokoaji na kusambaza ndege katika eneo karibu na mji wa Kahramanmaras, huku ikitangaza "kiwango cha 4 ya uokoaji" inayotaka usaidizi wa kimataifa.

Vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimesema kuwa idadi kubwa ya majengo yameporomoka katika jimbo la Aleppo, huku chanzo cha habari katika utumishi wa umma cha Hama kikisema kuwa majengo pia yameporomoka huko.

UPDATES
Vifo zaidi ya 100 upande wa Uturuki, 39 Upande wa Syria huku watu wengi wakiwa bado chini ya vifusi.

Italia yaonya kuwa tsunami yaweza tokea kutokana na tetemeko hilo

UPDATE: WALIOFARIKI KWA TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI NA SYRIA WAFIKIA 1500

Wakati shughuli za Uokoaji zikiendelea baada ya kutokea Tetemeko lenye kipimo cha Richa 7.8, zoezi hilo linaanza kukabiliwa na ugumu kutokana na Mamia ya Watu kunaswa kwenye vifusi

Zaidi ya watu 5000 wamejeruhiwa na wengine bado hawajulikani walipo na wana hali gani. Nchi za Cyprus, Misri na maeneo ya Lebanon yamepata Mtikisiko kutokana na Tetemeko hilo.

---
UPDATE: IDADI YA WALIOFARIKI KWA TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI YAFIKIA WATU 1,800

Vifo zaidi vinazidi kuripotiwa kufuatia Tetemeko la ukubwa wa Richa 7.8 kuzipiga Uturuki na Syria usiku wa kuamkia Februari 6, 2023 na kuporomosha mamia ya Majengo wakati watu wakiwa wamelala

Idara ya Dharula Nchini Uturuki imeomba msaada kwa Jumuiya za Kimataifa baada ya kutokea Matetemeko mengine mawili yenye kipimo cha 7.5. Uingereza tayari imetuma Wataalamu 76 wa Utafutaji na Uokoaji.


UPDATE: Zaidi ya watu 2,300 wamepoteza maisha huku waokoaji wakiendelea kutafuta manusura
Zaidi ya watu 2,300 wamepoteza maisha huku waokoaji wakiendelea kutafuta manusura kutoka chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka kutokana na Tetemeko kubwa la ardhi lililozikumba Uturuki na Syria leo Februari 6, 2023 na kuacha majeruhi zaidi ya 10,000 na wengine wakiwa hawana makazi.

UPDATE: Staa wa zamani wa Chelsea Christian Atsu akwama kwenye kifusi

View attachment 2508725
Staa wa zamani wa Chelsea na Newcastle za England Christian Atsu (31) Raia wa Ghana ambaye kwa sasa anacheza Hatayspor ya Uturuki amekwama kwenye kifusi cha jengo lililoanguka baada ya tetemeko la ardhi.

Harakati za kumuokoa Atsu zinaendelea lakini kwenye tetemeko hilo lililotokea leo nchini Uturuki mitandao mbalimbali imeripoti kuwa watu zaidi ya 1400 wamefariki Dunia.

Atsu ambaye alijiunga na Chelsea 2013 na kuishia kutolewa kwa mkopo Newcastle na Everton, alikuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Uturuki jana kati ya timu yake ya Hatayspor dhidi ya Kasimpasa ambapo aliisaidia kupata ushindi wa 1-0 akifunga goli dakika ya 90+
Vipi huko? Madokta wamefika hawajafika?
 
Siasa ndani yake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
 
Itakuwa mwaka 1964 kama sikosei. ilipiga kwa sehemu kubwa eneo la bonde la Ufa hasa Manyara ya sasa ukanda wa milima ya Mbulu juu ya bonde la ufa.
Manyara kwa tetemeko ndo kwenyewe yani hasa usiku yanapenda kweli hata wiki iliyopita tu lilipita
 
Nashangaa Ktk mambo kama haya bado kuna watu mnaleta kejeli za kidini wakati kuna maisha ya watu kibao yamepotea bila kupenda ,haujui Kesho wake na wewe una ndugu na wazazi au watoto hivyo haipendezi mtu kukufanyia kejeli ikitokea hali kama hizo hata wewe hauko salama endapo kitu kama hiko kikitokea kwako ,tuombe sana Mwenyezi Mungu atuepeshe..
Sipati picha lingetokea bongo au afrika kwa ujumla janga kama la uturuki sijui kama wangeonekana watu kama Crimea na wenzie kuleta kejeli
 
Back
Top Bottom