Tetemeko la Ardhi latokea baadhi ya Mikoa ya Tanzania

Tetemeko la Ardhi latokea baadhi ya Mikoa ya Tanzania

Ni saa mbili na dakika 16, nikiwa nimejilaza ndani ghafla kitanda kikaanza kutikisika kwa nguvu, ardhi inavibrate, nikatoka speed, ile nmefika tu mlangoni naona wapangaji wenzangu wanatoka mbio huku tukiwa hatusemeshani.

Limedumu kwa dakika kama moja hivi.

Vipi huko kwenu ?
Acha bangi, dakika moja unaijua wewe?
 
juzi niliota nyumba yetu imeanguka kwa mtikisiko nikaanza kulia, kustuka ni ndoto kumbe chaajabu leo nasikia habari za tetemeko
 
Niliona sio hali ya kawaida mkuu,kufika nje ndio napata habari ni tetemeko
basi wewe kichwa chako kiko fasta sana, kitu cha sekunde chache umweza kutafsiri ninini na kuzima jiko na kukimbia ndani ya sekunde chache hizo hizo, hongera aisee!!
 
Mpaka sasa Serikali haijasema kitu ipo kimya.. Bunju huku balaa
 
Wakuu hili tetemeko limepita Huku Ubungo mkoa wa Dar es Salaam. Vipi huko kwenu?

Earthquake M6.1 - 3.495 miles of Field Patch - Tanzania by BMKG (2020-08-12 17:13:13 UTC)
--
Taarifa ya WanaJF walio mkoa wa Morogoro
Wapendwa watumishi ama ndio unyakuo na wengine tumeachwa "behind" nini!? Wachungaji na manabii kuna yeyote aliyetoweka? Jamani wenye imani tuzidi kuhabarishana. Mimi binafsi kwenye muda kama saa mbili na robo nilihisi kama mara mbili mtetemo fulani.
 
Back
Top Bottom