Tetesi: Tetesi za usajili wa dirisha kubwa ligi kuu Tanzania bara 2025/2026

hili la musa bala konte limekaaje?
 
Diarra anaelekea Kaizer chiefs
Coach Nasredine Nabi amaemhitaji
Kaizer chiefs tayari wametuma ofa ya billion 1.5
Yanga wapo wanafikiria ofa hiyo
Kumbuka Diara aliongeza mkataba wa miaka 3 kusalia Yanga
Kuna uwezekano 90% Yanga wakamuuza Diarra
 
Simba chukua Dube huyo
Hatuna muda mkuu na huyo. Kwanza kashasain yanga tayari..hizo porojo nyingine ni za wachambuzi uchwara...sasahivi Bora kusubiria official statement mchezaji ntakayemuona Simba day ama utopolo Day ndio rasmi ...saizi ni kupotezeana muda tu..embu ona mtu kama konte sijui, huku wanasema timu inalipa pesa timu bila kuwasiliana na mchezaji, kule wanasema mchezaji anataka kwenda timu nyingine hataki hata kusikia hio timu ya kijani ..sasa huoni ni kujisumbua tu kichwa kuwaza mchezaji ataangukia wapi...
 
Hapa kwa Conte tetesi zinasema wakati Mangungu anabishana na MO wenzao wakamaliza dili na timu ya Conte halafu kinyume nyume wakarudi kwa mchezaji. Insemekana narudia tena inasemekana mchezaji akabisha bisha kidogo pesa mwanaharamu mwishowe akakubali akasaini utopolo jumamosi iliyopita. Ndio maana utopolo sasa hawana wasiwasi wa Aucho kuondoka.
 
Basi utopolo watakuwa na kikosi kikali kuliko misimu yote
 
Twafaaaa!
Hivi kweli najiuliza kua kweli Mo hata kama ingekua hapendi timu ama ni bahili kwamba atashindwa kusajili wachezaji Wazuri ? Ina mana usiposajili vizuri timu inakua tia maji na ikitia maji hata na biashara zake zitakua mashakani mana watu watakosa mwamko hata wa kufatilia timu ...huwez kukosa bilioni 1 na milion 700 kumsajili mchezaji kama unajipiga kifua kua umeshatoa bilioni 87...hizo pesa zinaliwa ..narudia kusema mo angepata mtu aina ya hersi na wawe wawili tu kwenye usajili wakisaidiwa na kocha tu na kumuweka mtu kama magori tu , kila kitu kingeeleweka...ila kuwakumbatia maswaiba zake wasiojua chochote na wapigaji , tutavuna tulichopanda..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…