Teuzi mbalimbali kujaa majina ya watoto wa viongozi na vigogo Serikalini kama taifa tunaelekea wapi?

Kwamba uongozi ndo lengo la kusomesha watoto wako?wasipopata uongozi inakuwa umepata hasara?

Kwamba uongozi ni ulaji na unataka zamu ya ulaji Kwa watoto wako?

Hizo mentality Bora wakose kabisa uongozi hata wa mtaa...
Mentality za kijinga sana
Kwani kuna mtu ana haki ya kuwa kiongozi na wengine hawaruhusiwi kuwa na ndoto hizo?

Au hata kuwaza kuwaandaa watoto wako siku moja nao kuwania uongozi ni kosa?

Andiko halizungumzii tu uongozi (ambao umetumika kufikisha ujumbe) bali AJIRA kiujumla zimekuwa za kibaguzi, kujuana, rushwa na majina.

Hili kwako ni simple ila mataifa mengi yameanguka kwa mfumo huu ambao uanza kidogo kidogo baadae ukomaa na kuwa kansa.
 

Uongozi ni wito wa kuongoza wengine . uongozi sio ajira...
Kama huna uwezo wa kuongoza wengine basi huna haki ya kulazimisha upewe hiyo nafasi...
Tanzania kuna masikini Wengi wanachaguliwa Kwa uwezo wako...
Wala hakuna sababu ya kulialia upewe nafasi
 
Acha wivu! Kitu cha kufuatilia - je wana uwezo wa kazi wanazopewa? Je wanatatua matatizo ya wananchi na Taifa kwa jumla? Wewe jiongeze kutafuta maarifa na vipaji ili wananchi waone uwezo wako. Kuna msemo mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Kwahiyo Mtoto wa mwanasiasa ni rahisi kuwa mwanasiasa - anajifunza mbinu mapema kuliko Watoto wengine.
 
Mnaanzishaga mada nzuri huku mna jazba !
Hauelezei vya maana unaishia kulalamika tu!
Uoga wetu waTz ndiyo kaburi letu.
Hapo utaelezea nini ikiwa kichwa cha habari kinajieleza chenyewe na kila mtanzania anaona na kujua kinachoendelea ila tumeamua tu ile ya nani atakuwa wakwanza kumfunga paka kengele.
 
Wa kulaumiwa ni babu na wazazi wako. Wakati kina Julius wanapigania uhuru wao walikuwa wanakunywa Chimpumu na kuzichakata papuchi za wake wa watu...

Kaza buti wanao wasije kulalamika kama wewe...
Julius na wengineo kama ulivyowataja si wapigania uhuru bali majambazi wa kalamu, danganyika ilikuwa huru tokea mwaka 1951 wazungu walikuwa wameshaamua njia nyingine ya kuyanyonya makoloni yao pasipo kuwekeza nguvu na rasilimali zao kama awali(ukoloni mamboleo)

Lakini chakusikitisha Afrika kwa wakati ule haikuwa na wasomi kabisa, hivyo wachache hao waliokuwa matoashi wa malkia,walimu na wanaharakati au ma-ex soldiers wa mkoloni ndiyo waliosapotiwa na wananchi wao kupambania uhuru katika nchi zao

(kutokana na baadhi ya makoloni kuwa potential mno tamaa ilikuwa bado inawaijilia wakoloni wengine kuachia makoloni yao licha ya msukumo mkubwa toka kwa uingereza na mabeberu wengine waliokuwa wanapinga vikali mfumo huo kuendelea ki-analogia, hivyo kwa kuwa ni kwa faida yao na mataifa yao lazima mfumo ubadilike walitoa support kwa mataifa yote yalioanzisha chokochoko za kutaka uhuru wao na wakayakabidhi uhuru wa bandia/bendera)

but back to our country sisi ilikuwa ni kitendo cha kwenda tu na kuchukua ile certificate ya political freedom huko mambele ndiyo tulikosa mwakilishi maana muingereza hakuwa na interest sana na koloni hili tokea mwanzo bali alimpokonya mwenzake kuonesha ubabe tu.

Wazee wa DSM, uchagani na mafogo kadhaa wakamchangia ada mwalimu mmoja machachari wa sekondari pale pugu aende kupiga zake digrii kule uingereza na nauli akachangiwa tena ya kuendea uhuru 1961,

Wazungu wakamkabidhi kiroho safi ofisi wakiendelea kumfundisha namna ya kujiongoza akiwa waziri mkuu na hata walipotaka kumpindua wanajeshi wake hao hao kina malkia akaenda kuwapigia magoti kuhitaji msaada wao na wakamsaidia.

(Eti HARAKATI ZA KULIKOMBOA BARA LA AFRIKA tangu mwaka 1880s-1990s..My foot hamnaga kitu kama hicho hizo ni historia za darasani kwa ajili ya kuandaa watoto wa taifa la kesho kuamini kama babu zao hawakuwa wazee wa ovyo)
 
Hilo haliwezi kuwa taifa tena.
Taifa gani hapa duniani ambalo nafasi za uongozi ziko shared equally?
Nature ya mwanadamu ni tamaa ya kuwa juu ya mwenzake! kiuongozi na kiuchumi .

More over ni baba yupi alimpa nyoka mwanaye alipoomba samaki?

Kiukweli kuna classes kwenye jamii zetu kama msimamo wa ligi kuu NBC ... kuna top dogs, middle table, na wale wanapambana wasishuke daraja.

NB. ili ubadirishe daraja/class uliyopo there is price to pay.... either you learn how system work and be among them(hapa lazima uwe chawa)... or you choose the hard way .... fight them ..
 
Uongozi ni wito wa kuongoza wengine . uongozi sio ajira...
Kama huna uwezo wa kuongoza wengine basi huna haki ya kulazimisha upewe hiyo nafasi...
Tanzania kuna masikini Wengi wanachaguliwa Kwa uwezo wako...
Wala hakuna sababu ya kulialia upewe nafasi
Ilo neno "UONGOZI SIYO AJIRA" ukiacha unafiki "SIYO KWELI" katika kuakisi uhalisia wa mambo "KWA SERIKALI HII" tuliyonayo ila kwenye makaratasi na filosofia ya uongozi huko sawa kabisa.

Yaani ni sawa na kale ka msemo ka UALIMU SI AJIRA bali "UALIMU NI WITO" baada ya hapo mnawalipa ujira kiduchu, mnawarundikia makato na vyama vya upigaji na kama haitoshi mnawafungulia na taasisi za kuwakopesha mikopo komoa.
 
Mlaumu babu yako na uvivu au uoga wake. Angekuwa mpambanaji kama Kina Warioba hivi sasa ungekuwa Naibu waziri wa Afya, Jamii na Maendeleo ya watoto.
Babuu emu nikuachee, naona unataka nipewee ban, nirudi MMU tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wa kulaumiwa ni babu na wazazi wako. Wakati kina Julius wanapigania uhuru wao walikuwa wanakunywa Chimpumu na kuzichakata papuchi za wake wa watu...

Kaza buti wanao wasije kulalamika kama wewe...
walipigania uhuru wate walipa uongozi?
 
Kama binadamu tungetamani wote tuwe equally kitu ambacho hakiwezekani, ila kwa maana ya madaraja ya uwezo tunatamani kama taifa tuwe na wananchi daraja la tatu linaloweza walahu kupata mahitaji muhimu yaani chakula,malazi na mavazi na hili wapate hiki lazima kuwepo na mwanya kidogo kwao wa kutengeneza kipato na kujimudu ila kwa hali hii wachini atabaki wachini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…