TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

Kwenye huu uteuzi sijaona jina la kinyakyusa hata moja. Mama angemteua hata Mwakalebela mzee wa Yanga atuwakilishe Green City....kkkkkkkk
 
Pongezi kwa wateule wote.
Wote mnafaa na mnastahili kupewa dhamana hiyo, Mhe. Rais amewaamini na sisi wananchi tunawaamini kuwa mtachapa kazi kwa nguvu na maarifa.
usisherehekee kupata cheo bali sherehekea pindi utakapo tatua kero za wananchi na kuleta maendeleo kwenye kipande chako ulicho kabidhiwa.
Mungu awatangulie.
Aaaamin 🙏
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo ameachia mkeka wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali uliosheheni vijana. Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wapya ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji, pia yupo Joshua Nassari na Wakili Albert Msando. Wengine ni Mwenyekiti wa UVCCM Kherry James, mtangazaji Hassan Ngoma kutaja kwa uchache.
Masanja mkandamizaji mbn teuzi zimemkataa
 
Hivi mama anafeli wapi wadau ?yaani ndani ya ccm hakuna vijana wa kupewa uteuzi hadi anawapa ulaji hao wahamiaji wenye tamaa ya madaraka toka chadema, kuna vijana wengi ccm wamekipigania chama toka zamani lakini hawajapata uteuzi,daah yaani anarudia yale yale kama ya hayati magufuli
Mtajijua
 
Back
Top Bottom