TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

Dunia nzima ndo maana kukawa na vyama vya siasa hata kwenye nchi zenye ufalme vyama vya siasa vipo . Mnapokuwa chama kimoja mnakuwa na ideology moja huwezi kuta mtu wa Dem kumchagua mtu wa Rep kwenye nafasi za kisiasa hata siku moja kwa maana mtakuwa mnatofautiana maono pia kumchagua mtu wa chama chako kunaleta amani na upambanaji kwa kuamini tunapigana vita tukishinda bhasi tutaongoza pamoja ndo maana Trump aliweka mpk watoto,wakwe nk kwa vile walipigana pamoja

Sasa unashangaa Tanzania wanaotukanwa matusi ,waliokesha,mvua ,jua,baridi,joto zote ziliwaishia na ktembea nyumba kwa vyumba kuomba kura wanaachwa wanakwenda kuteuliwa watu ambao hawana hata uchungu na chama wengine hata huwezi sema ni CCM mfano huyu Nick hv kweli??


Sidhani kama Chadema wakichukua nchi wanaweza waacha watu wao waliopambana usk na mchana kwenda kuchagua mamiss ,waimba muziki ambao hata si wanasiasa na kuwapa nafasi na kuwaacha watu waliokesha kutukanwa kufungwa kwa sababu ya chama

Japo unaweza kusema Nchi ni moja na wote ni Watanzania but hata Mungu mitume wote na manabii wote walitokea eneo moja la middle east kwani hakuona sehemu nyingine au maeneo mengine kulikuwa hakuna wanadamu akateua kutoka sehemu moja?

Kama Tumeona kazi ya DC ,RC mtu yeyote anaweza fanya ukipiga mahesabu ni nafasi zaidi ya 200 za kazi bhasi ziwe zinatangazwa tunatafuta international recurtment company wanasimamia zoezi la interview kuondoa vigisu watu wanafanya kila mtanzania mwenye vigezo na uwezo anaomba wanaoshinda bhasi wanakuwa wakuu wa wilaya kwa contract ya miaka 5
 
Maingizo mapya ya Samia nimeyaelewa, tasnia ya habari inaonekana ina kismati sana kwenye hizi nafasi. A. Mwaipaya (ITV/Radio One), G. Zakaria (TBC fm), Fatma Nyangasa from Azam Media.

- Mwaipaya akitoka kwenye msiba wa baba yake akatulie kwenye v8.

Huko Kigoma ngoma ni maafisa wa jeshi tu, ukiondoa Kigoma mjini kwingine kote ni maafisa jeshi.
Mama mtu wa media, hata humu anaweza kuwemo.

Kigoma ni mkoa wa kimkakati unahitaji kuongozwa na watu wakakamavu. Burundi na DRC ni pua na mdomo.
 
Siasa ndio ajira pekee zilizobakia .

Yaani serikali imeshindwa kutengeneza ajira imebakia kuteua watu nafasi za kisiasa.

Shame.
Wakiwa ni vijana wanao wajibu wa kupeleka ubunifu na maarifa yao katika kukuza chumi za maeneo husika.

Wengi wao ni mafundi wa kukosoa wakiwa Facebook, Twitter na humu ndani. Sasa hayo mawazo na yakachangie kuleta mabadiliko yenye kuonekana.

Rais amekikabidhi rasmi kizazi cha vijana ule mustakabali wa Tanzania.
 
Kila jambo na muda wake hii ni awamu sita tuvumiliane.
 
BAVICHA mnateseka sana. Waliomuunga mkono Magufuli wameteuliwa ili sasa kazi iendelee.
 
Huu uteuzi ni sawa na uteuzi wa class rep au admin wa magroup ya whatsapp tu. Sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu. Poor
 
Hizi ni ajira kama zilivyo ajira zingine.
Tanzania raha sana, hata uchumi uyumbe vipi ajira za kisiasa hazikosi mtu
 
Back
Top Bottom