ELIMU KUHUSU MAPATO YA SIMBA NA YANGA
Anaandika Sangu Joseph
Nitoe elimu kidogo ni kweli Mechi imeingiza Milioni 410, na Simba imepata Mil. 188 ambayo hata ukizidisha mara 2 huwezi fikia kiasi cha pesa walichokiingiza.
Haya yote yanaanzia kwenye Kanuni za Uendeshaji wa Ligi Kuu, ambazo vilabu huwa wanapewa na kuzipitia kwenye Kanuni za Ligi Kuu Sura ya 8 inayozungumzia mapato na gharama inataja mapato yanavyokatwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu.
18% ni VAT, 3% kwa BMT, Gharama za Tiketi, Baki ya mapato timu mwenyeji atapata 60%, TPLB 8%, gharama za mchezo 7%, Uwanja 15%, , TFF 4%, FA Mkoa 6%,
Sasa nimeona watu wanasema eti ili Yanga na Simba ziondokane na hayo makato zijenge Uwanja wake bado sio suluhu la kupata mapato mengi kwa sababu hapo Klabu zitakua zimeokoa asilimia 15 tu ya gharama za Uwanja.
Hapo cha muhimu na chakufanyiwa kazi ni kuyaondoa makato yasiyokua na manufaa moja kwa moja kwa Vilabu.
ASILIMIA 8 ZA TPLB NA ASILIMIA 4 ZA TFF.
Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu, sura ya 14 Kanuni ya 12 anayeendesha Ligi ni Bodi ya Ligi na atawajibika na kushirikiana na TFF hivyo maana yake vilabu vinawajibika kwa Bodi ya Ligi na si TFF ila Bodi anawajibika kwa TFF.
Haya makato wanayokatwa Klabu na TFF ni batili kwa sababu kwenye mchezo husika / Mechi) hakuna mahali TFF anahusika na Klabu ila anayehusika ni Bodi, hivyo kilichopaswa kwenye asilimia 8 ambayo TPLB inachukua kwenye Get Collectiom ndiyo ilipaswa kukatwa asilimia 4 iende kwa anayemsimamia ambaye ni TFF.
ASILIMIA 3 ZA BMT
Kwanza hii ni Taasisi ambayo iko chini ya Wizara ya Michezo ambayo inatengewa Bajeti na Serikali Kuu.
Lakini pia ukisoma majukumu yake hakuna mahali ambapo anahusika na Vilabu bali yeye wanachama wake ni Vyama Vya Michezo, TFF, CHANETA, TBF hivyo yeye hiyo asilimia 3 alipaswa kuwakata Manachama wake ambaye ni TFF kumkata Klabu tena Get Collection ni kumuonea tu wakati hajahusika kokote.
FA MKOA ASILIMIA 6
Hizi asilimia 6 za Chama cha soka Mkoa ni nyingi sana kwa sababu ukiangalia ushiriki wa FA Mkoa kwenye mechi husika majukumu yao yanayotofauti gani na yanayofanywa na Bodi ya Ligi kwenye kuhakikisha mchezo husika unachezwa.
Kwa hiyo kujenga Uwanja pekee sio suluhisho, ila kuondoa na kupunguza makato
C&P