Hivi nchi hii itajifunza lini kuwa vilio vya wengi ndivyo Sababu ya mipango mingi kuanguka?
Kweli mnajua kuwa Watanzania wengi ni wapenzi wa michezo hususani Soka, na kuwa soka linaunga nisha wengi hata wenye tofauti za siasa.
Jee ni kweli nchi hii I mekosa kabisa watu wa kuunda Kamati ya Saidia Stars ishinde hadi kumuweka Makonda kuwa mwenyekiti na Jerry Muro mjumbe? Mnajua kuna watu wanachuki kubwa na hawa watu na kuwahisi ni watu waliomo kwenye kundi linalotuhumiwa mabaya mnadhani wataendelea na mapenzi na Stars? Mie nimeingia baridi.
Mumeivuruga Stars na sitashangaa tukaambulia kipigo maana sasa hata wenzetu wengine dua zao zitakuwa against Stars.
Hivi Karia anatumika kwenye siasa? Maana ukiangalia kuna dalili wameona STARS wanashinda na hapo anatafutwa mtu asiye na aibu asifie kuwa hizi ni juhudi za awamu ya tano maana mbona tokea Nyerere hatujaenda tena AFCON hadi sasa.
Ile milioni hamsini itatajwa kuwa kichocheo kikubwa utadhani ni big deal. Nani asiye na mshipa wa aibu kusema hayo kama sio Makonda?
Lakini hamjiulizi jee Makonda na MO Dewji wanaweza kukaa meza moja na kujadili jambo la maana au kutuzuga tuu?
Pia mnadhani Wachezaji ni robot tuu hawana chembe ya itikadi na chuki zao mioyoni? NALIONA ANGUKO LA STARS. MSIONE AIBU VUNJA HIYO KAMATI UNDA MPYA
Sent using
Jamii Forums mobile app