Bado unarudi kule kule kwenye hoja yangu, ila tofauti ni kwamba unakataa kukubaliana na kile ninachokiandika kwa sababu zako binafsi.
Nimekwambia haya matukio ya hawa jamaa kutoroka gerezani na ku fake kifo cha mtuhumiwa yalikuwa wazi. Vyombo vingi vya habari viliripoti hizo taarifa. Na kwa vile dunia ya leo ni kijiji kupitia habari mbali mbali hususa news za redioni, magazetini, redioni nk ikawa rahisi watu wengi hata wale ambao sio askari kufuatilia ishu za jamaa.
Swala la polisi wetu kula rushwa sio la wote. Haiwezekani katika taasisi yoyote watu wote wawe na tabia za kufanana. Hata majambazi wanapokwenda kuiba kuna wale ambao hupenda kuuwa baada ya kuiba na kuna wale ambao huwa hawajishughulishi na mauji baada ya kuiba. Unakuta mmoja anataka kuuwa ila mungine anamkataza asiuwe.
Hivyo hivyo kwa jeshi la polisi duniani sio nchini tu, wapo wala rushwa na wapo wasiokula rushwa. Ndio maana hata kwao ingawa alikuwa gerezani chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya ulinzi lkn aliweza kupenyeza chochote na kufanikisha deal lake la kumtorosha, ila hili wewe haujaliona.
Kwahiyo swala la rushwa sio la Tanzania tu peke yake kama unavyojaribu kukazia, bali ni la dunia nzima ndiomaana hata huko alipokuwa anatumikia kifungo chake rushwa ilitembea na jamaa akafanikiwa kutoroshwa katika mazingira tulioyaona ya ku fake kifo chake nk.
Kama unataka na kulazimisha tu sifa ziende kwa hao jamaa zako, mbona hao jamaa zako walishindwa kutumia hiyo njia unayoona waliitumia bongo kumkamata kabla hajavuka mpaka wao?
Imekuaje nchi yenye askari au wapelelezi makini (kwa mujibu wa mawazo yako) ilishindwa kutambua mapema kwamba kile kifo kilikuwa ni changa la macho muda wote aliokaa nchini kwao na mpaka akafanikiwa kutoroka kupitia mipaka yao?
Lkn pia kama ni wao ndio waliofanikisha kukamatwa kwake, kwanini kufanikisha huko kufanyike Tanzania tu na sio Zimbabwe, Msumbiji au nchi nyingine yoyote aliyopita?