Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

SA na TZ wana mikataba ya kiulinzi na usalama, ndio maana ilikuwa rahisi Mr Bester kukamatwa nchi TZ na kukabidhiwa kwa mamlaka ya SA.

Swala la dereva wa Lisu linatemea na nchi aliyopo. Kuna nchi ambazo hatuna mikataba nazo ya ulinzi na usalama. Kwahiyo hata serikali yetu ikijua kuwa dereva huyo yupo katika nchi hizo, kamwe haiwezi kuwa na uwezo wa kuingia katika nchi hizo na kumkamata dereva huyo. Hivyo swala la Lisu na huyu Mr. Bester ni mambo mawili tofauti.
Kama kweli SA na TZ Wana Mikataba ya kiulinzi,mbona kuna wahalifu wengi tu wameharibu TZ na Wamejificha huko SA na Serekali ya SA wala haina habari nao!? Mfano mdogo tu ni Alex Masawe!!
 
Hao ni majasusi wa dunia.

Mbaya kuua mtu ili wewe uokoke, mbaya zaidi mbele za Mungu pia.

All in all polisi wa tz wako vizuri, naogopa kusema CONGRATULATIONS.

Angesogea hapo kwa Uhuru asingekamatwa mpaka afe kweli kweli.
Ila najiuliza, aliechomwa mule kwenye cell aliingiaje? Na kama ni mfungwa mwingine hakuwa accounted for wakati wa kuwahesabu?
 
Ila najiuliza, aliechomwa mule kwenye cell aliingiaje? Na kama ni mfungwa mwingine hakuwa accounted for wakati wa kuwahesabu?
Hata hivyo ujue pia ilitumika nguvu ya pesa, ukute jamaa alifunguliwa migeiti kajipitia free, mnyonge mmoja ndo kachomwa.

Tukubali tu hivi vitu vipo duniani
 
Wanafanya siri ila ukweli Wa SA watakuja kuongea maana zile maiti zaidi ya kumi za wanawake zilizokua zinapatikana zote zilikua hazina viungo kama macho na Figo mwenye deal ni huyo Dr Mwanamke anajua hivyo viungo walikua wanapeleka wapi maana viungo vya binadamu SA ni deal sana hata mtu akipata ajali ndugu wasipokua makini watakuta baadhi ya viungo hakuna waache viswahili vingi wawe wazi hata kwenye hiyo kesi yao vitu vingi vikifichwa mtuhumiwa anakua huru kufanya chochote kama sasa huyo Mwanamke ndio mdhaminj wa kutoroka kwa Thabo ila hawajiulizi kapata fungu la 5 milioni rand wapi za kuhonga kama sio biashara yao haramu...niliwahi ona picha ya dada mmoja alitupwa Woodmed aisee nilisikitika sana muhuni anatongoza Facebook harafu anaishia kuwaua na kuwatupa maeneo tofauti iliwekwa mitego mpaka akaja kukamatwa...
 
Bado unarudi kule kule kwenye hoja yangu, ila tofauti ni kwamba unakataa kukubaliana na kile ninachokiandika kwa sababu zako binafsi.
Nimekwambia haya matukio ya hawa jamaa kutoroka gerezani na ku fake kifo cha mtuhumiwa yalikuwa wazi. Vyombo vingi vya habari viliripoti hizo taarifa. Na kwa vile dunia ya leo ni kijiji kupitia habari mbali mbali hususa news za redioni, magazetini, redioni nk ikawa rahisi watu wengi hata wale ambao sio askari kufuatilia ishu za jamaa.

Swala la polisi wetu kula rushwa sio la wote. Haiwezekani katika taasisi yoyote watu wote wawe na tabia za kufanana. Hata majambazi wanapokwenda kuiba kuna wale ambao hupenda kuuwa baada ya kuiba na kuna wale ambao huwa hawajishughulishi na mauji baada ya kuiba. Unakuta mmoja anataka kuuwa ila mungine anamkataza asiuwe.

Hivyo hivyo kwa jeshi la polisi duniani sio nchini tu, wapo wala rushwa na wapo wasiokula rushwa. Ndio maana hata kwao ingawa alikuwa gerezani chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya ulinzi lkn aliweza kupenyeza chochote na kufanikisha deal lake la kumtorosha, ila hili wewe haujaliona.

Kwahiyo swala la rushwa sio la Tanzania tu peke yake kama unavyojaribu kukazia, bali ni la dunia nzima ndiomaana hata huko alipokuwa anatumikia kifungo chake rushwa ilitembea na jamaa akafanikiwa kutoroshwa katika mazingira tulioyaona ya ku fake kifo chake nk.

Kama unataka na kulazimisha tu sifa ziende kwa hao jamaa zako, mbona hao jamaa zako walishindwa kutumia hiyo njia unayoona waliitumia bongo kumkamata kabla hajavuka mpaka wao?
Imekuaje nchi yenye askari au wapelelezi makini (kwa mujibu wa mawazo yako) ilishindwa kutambua mapema kwamba kile kifo kilikuwa ni changa la macho muda wote aliokaa nchini kwao na mpaka akafanikiwa kutoroka kupitia mipaka yao?

Lkn pia kama ni wao ndio waliofanikisha kukamatwa kwake, kwanini kufanikisha huko kufanyike Tanzania tu na sio Zimbabwe, Msumbiji au nchi nyingine yoyote aliyopita?
Sawa. Polisi wa Tz anafuatilia habari za mhalifu wa SA ili akija Tz amkamate huku akishindwa kupambana na wahalifu wa nchini kwake. Safi sana.
 
Sheria ya MTU akiuawa ni lazima auawe. Mawazo tofauti na hayo ni yawapuuzi. Na hayalengi kutenda HAKI
Samahani! Mtu akikupiga na kitu kwenye jicho na ukapoteza uono wako, na yeye atobolewe jicho!? Au mtu akimbaka mkeo, na wewe umbake mke wake!? Wewe hiyo Sheria ya mtu akiua na yeye auawe umeitoa wapi!?
 
Sheria ya MTU akiuawa ni lazima auawe. Mawazo tofauti na hayo ni yawapuuzi. Na hayalengi kutenda HAKI
Upuuzi sio neno la kistaarabu, na maneno haya ya vijiweni yaache huko huko, PM Pinda alivyotoa tamko lake la kutokukubiliana na death sentence, hukunyosha kidole chako juu, kutofautiana kwenye mada ni haki ya kila mchangiaji, this how we debate, USA kuna states zina death sentence zingine hazina na kila state ina respect hayo, SA haina death sentence na Tanzania tuna death sentence, ni kawaida kutofautiana, next time Linda status yako kwa kuheshimu mawazo tofauti na yako
 
Samahani! Mtu akikupiga na kitu kwenye jicho na ukapoteza uono wako, na yeye atobolewe jicho!? Au mtu akimbaka mkeo, na wewe umbake mke wake!? Wewe hiyo Sheria ya mtu akiua na yeye auawe umeitoa wapi!?

Sheria zipo wazi.

Sheria Dunia kote asilimia 99% MTU akiua anauawa.
Sheria za dini na Mila na tamaduni zote Duniani MTU akiuawa anauawa.

Ua Kwa kukusudia alafu utaiona ni sheria ipi itakufanya Uuawe.
 
Upuuzi sio neno la kistaarabu, na maneno haya ya vijiweni yaache huko huko, PM Pinda alivyotoa tamko lake la kutokukubiliana na death sentence, hukunyosha kidole chako juu, kutofautiana kwenye mada ni haki ya kila mchangiaji, this how we debate, USA kuna states zina death sentence zingine hazina na kila state ina respect hayo, SA haina death sentence na Tanzania tuna death sentence, ni kawaida kutofautiana, next time Linda status yako kwa kuheshimu mawazo tofauti na yako

Kwenye mijadala MTU akitoa mawazo ya kipuuzi lazima Watu tuseme hayo ni mawazo ya kipuuzi bila kujali nafasi yake.
Hata Mimi nikisema mawazo ya kipuuzi sitowakataza Watu kusema mawazo niliyoyatoa ni yakipuuzi bila kujali Status yangu.

Usinifundishe Unafiki.
Naheshimu mawazo ya wengine ikiwemo ya wapuuzi na wapumbavu lakini hainizuii kusema wazo Fulani(alilotoa fulani) ni la kipuuzi na mara nyingi wanaowaza hivyo ni wapuuzi.

Kwa hiyo Kwa uelewa wako Kwa vile MTU akiwa Waziri au Rais, au nabii au cheo chochote hawezi ongea Upuuzi?

Msifundishe Watu Unafiki
 
Sheria zipo wazi.

Sheria Dunia kote asilimia 99% MTU akiua anauawa.
Sheria za dini na Mila na tamaduni zote Duniani MTU akiuawa anauawa.

Ua Kwa kukusudia alafu utaiona ni sheria ipi itakufanya Uuawe.
Acha kuongea uongo, uongo ni tabia chafu na hope's kizazi chako hautawarithisha tabia hii chafu, utafiti gani huo wa 99%kuhusu death sentence hapa duniani?,Tanzania tuna death sentence, nenda magereza HQ ulizia ni ngapi zimetekelezwa, binafsi naelewa kwa miaka zaidi ya 25 ya utawala wa president Nyerere ame Saint death sentence moja tu, death sentence ni ukatili mwingine kwa kiwango cha juu
 
Usemaji wa watu kakupa nani cheo hicho?,wewe changing ya kwako usiwe mchangiaji wa watu, huu ni uongo mwingine, nachukia mtu mwongo
 
Acha kuongea uongo, uongo ni tabia chafu na hope's kizazi chako hautawarithisha tabia hii chafu, utafiti gani huo wa 99%kuhusu death sentence hapa duniani?,Tanzania tuna death sentence, nenda magereza HQ ulizia ni ngapi zimetekelezwa, binafsi naelewa kwa miaka zaidi ya 25 ya utawala wa president Nyerere ame Saint death sentence moja tu, death sentence ni ukatili mwingine kwa kiwango cha juu

Hivi ulitaka Death sentence itangazwe?
Tafuta wanaofanya kazi ya kunyongwa wao ndio watakuambia wananyonga kwa kiwango gani.
Sio kila kitu Serikali itakuambia, wewe ni MTU mzima jaribu kufikiri Mkuu.

Ingia Youtube tafuta video ya Yule Baba MTU mzima ambaye kazi yake ni kunyonga Watu tena anahama magereza,
Nenda kaangalie interview yake kuanzia alivyoapply kazi, namna anavyofanya kazi na changamoto zake. Kwa Siku ananyonga Watu wangapi, n.k.

Sio unabisha mambo usiyoyajua.
 
Sheria zipo wazi.

Sheria Dunia kote asilimia 99% MTU akiua anauawa.
Sheria za dini na Mila na tamaduni zote Duniani MTU akiuawa anauawa.

Ua Kwa kukusudia alafu utaiona ni sheria ipi itakufanya Uuawe.
Sheria za dini gani!? Serikali (ya Tz) inaamini dini!? Sheria za mila na tamaduni!? Mila za nani!? Tamaduni za nani!? Maana jamii ziko tofauti na kila moja ina taratibu zake. Usiisishi kwa kukariri. Huyo anayemuua huyo aliyeua naye anachofanya ni nini kama sio kuua!? Hiyo 99% umeitoa wapi!? Acha kutunga tunga porojo.
 
Uislam
Uyahudi
Dini za kimila za kiafrika zote zinasheria za kuua.
Ukristo pekee ndio hauna hiyo sheria.

Kuhusu serikali yetu, haina dini na haitukii sheria za dini katika Makosa ya jinai.
Ila inasheria ambazo MTU akifanya kosa Fulani ananyongwa mpaka Kufa.

Ndio maana nikakuambia Fanya mauaji ili ujue ninachosema ni porojo au sio porojo.
 
Nalazimika kusema "wewe ni mwendawazimu"
 
Nalazimika kusema "wewe ni mwendawazimu"

Ukimaliza kajiangalie kwenye Kioo alafu utajiona wewe ni MTU wa Aina gani?

Huwezi ondoa sheria ya kifo Kwa viumbe wanaouana. Hiyo haiwezekaniki.
Ni MTU mjinga pekee anayeshindwa kutofautisha kauli na matamanio ya kisiasa na Maisha Halisi.

Yaani MTU aue MTU Kwa Makusudi alafu yeye asiuawe? Hivi hizo Akili mlitoaga wapi?

Mnashindwa hata na wanyama
 
Hata hivyo ujue pia ilitumika nguvu ya pesa, ukute jamaa alifunguliwa migeiti kajipitia free, mnyonge mmoja ndo kachomwa.

Tukubali tu hivi vitu vipo duniani
Kuna mdau hapo kasema kwamba walienda kununua maiti kisha wakaiingiza kimagendo na kuichoma
 
Back
Top Bottom