Hapana. Mara nyingibe bei inaweza kuwa juu au chini kuliko thamani.
Kunaweza kununua kitu kilekile Mazense na Samora kwa bei mbili tofauti.
Na pia, mtu anaweza kununua Mercedes Benz mpya ambayo mtu mwingine aliinunua akaitumia kwa siku mbili tu kisha akairudisha, na utauziwa kwa bei nusu ya bei ikiwa mpya. Sio kuwa imeshuka thamani bali imeshuka bei kwa kuwa ilishatoka show room.
Ndio maana TRA ukiingiza gari wanakugonga kitu kinaitwa price uplift, kwa madai kwamba bei ya kwenye karatasi sio thamani ya gari.
Na pia Kahawa ya Kempinski na ya Sinza Hotel, ya Sinza hotel inaweza kuwa na ubora kuliko Kempenski lakini ukalipa mara tano zaidi kahawa ya Kempinski.
Mnaweza kusafiri kwenye ndege siku moja watu wawili wote mko economy lakini mmelipa nauli tofauti. Sio kuwa thamani ya kiti cha ndege kwa mmoja wenu iko juu ya ile ya mwingine.