The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

System ya Tanzania ilivyo huwezi hata kuwasiliana na wabunge kwa e-mail sababu majority yao hawajui hata what is email. Sasa how you gonna complain?

Magazeti makubwa kama Nipashe, Majira and others will not take your complain and publish in the front page, sababu editor ana kadi ya kijani ndani. So, system is so complicated.

One thing i can demostrate is to consult Mr Zito that Tanzania siasa ni kichwa cha mwenda wazimu, go back to school and earn your PhD, then just utilize your knowledge to your fellow Tanzanian. I know if we can't stand then who will stand, but rememember we are fighting with CCM (chama cha Majambazi), and on top of that Zito hana waku msupport sababu wapinzani ni wachache na wote wanatunza viti vyao.

Smart move, iandikwe barua ya wazi ambayo itafanyiwa petition na majina atleast 500 humu JF kisha ichapishwe kwenye magazeti makubwa mawili amabyo itamuuliza kikwete yeye kama Mweneyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nini msimamo wake katika swala la Zito, na spika sitta nini msimamo wake.
 
Mtanganyika,

Mbona baadhi ya maandiko yako ya kiingereza ngumu sana kuyaelewa?

Najua kila mtu ana matatizo kwenye hizi lugha, ila kwa ushauri wangu jitahidi kuyapunguza hayo makosa kwa ku review posts zako kabla ya kutuma.

Pia naona tatizo ni kuandika, sijui uko wapi lakini jitahidi kuchukua course hata ya miezi michache ili kuongeza ufanisi katika maandishi yako.

Naomba usichukie na badala yake take it as a challenge. Wote tuna matatizo na wakati mwingine ngumu kujua mpaka mtu mwingine akuambie.
 
Chakaza
[QUOTE Malecela anapewa heshima sana ndani ya CCM katika kuendesha mambo kihuni.Angalia hata katika kuchangia hoja za kumfungia Zito,yeye kapangwa kuwa msemaji wa mwisho na kabla hajazungumza eti anaitwa Zito azungumze kama ana lolote la ziada(kuomba radhi) kabla HAKIMU mkuu Malecela hajapitisha hukumu.
Hii ni aibu sana. Hata hivyo kama ilivyotegemewa na wengi SHUJAA KIJANA WA KITANZANIA ZITO KABWE hakubembeleza wanafiki na wasaliti wa nchi hii bali aliwaambia wafanye vile watakavyo na kuwa fikra za kimapinduzi zitadumu.Wazee kama hao wasubiri aibu mwisho wa safari kisiasa[/QUOTE]

Kwa kweli sababu ya MAlecela, ambaye ni Makamu MWenyekiti wa CCM, na Spika wakati anampa nafasi alirudia mara mbili kusema, Meheshimiwa Mbunge Malecela, Mheshimiwa Mbunge Malecela..." hii ni kujaribu kufuta akilini mwaka mkakati wa kichama uliomopanga Malacela kusema mwisho... Na ndio maana badala ya kuacha wote waseme ndio amuulize Zitto kaama ana cha kusema, anamuuliza kabla ya "mtu anayetakiwa kuhitimisha mkakati wao wa Kijambazi"

Lakini watu kama "Mugongo Mugongo" na Jamaa yangu wa Pwani... kwanza majina yao yana maana mbaya sana na ashakum si matusi naomba tuwaombee dua kwa Mungu awape ufahamu wa kutambua wayafanyayo hata kama ni ile ya "Mtumikie Kafiri" lakini wazinduke na kuibua hoja za kutetea taifa maana nawaona ni watu waliozaliwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja lakini wanapindisha makusudi kama walivyofanya mabosi wao ndani ya Bunge jana usiku
 
Mtanganyika,

Mbona baadhi ya maandiko yako ya kiingereza ngumu sana kuyaelewa?

Najua kila mtu ana matatizo kwenye hizi lugha, ila kwa ushauri wangu jitahidi kuyapunguza hayo makosa kwa ku review posts zako kabla ya kutuma.

Pia naona tatizo ni kuandika, sijui uko wapi lakini jitahidi kuchukua course hata ya miezi michache ili kuongeza ufanisi katika maandishi yako.

Naomba usichukie na badala yake take it as a challenge. Wote tuna matatizo na wakati mwingine ngumu kujua mpaka mtu mwingine akuambie.

sidhani mahala nilipo panasaidia nini kuhusu kuandika kwangu. I don't think at this point any course will make any life easy.

I don't take things personal, but we differ on tones, probably you find hard to understand my tone for some reasons. I wish i could help, but at this point i'm sorry.

third, i used kiswahili almost the entire post, however english is the second language so keep up with it.

Thanks for concern
 
Mtanganyika,

Sawa, post niliyoongelea ni ile ya kwanza ambayo umetumia kiingereza kwenye post yote.

Pili suala la uko wapi, lililenga kwenye kuonyesha urahisi wa kupata course ya kukusaidia. Najua TZ ni ngumu na aghali sana
kwa mtu kujiendeleza kuliko sehemu zingine. Samahani kama kuuliza hivyo ulinielewa vibaya.

Lilikuwa ni wazo tu na njia ya kusaidiana na kuelemishana.
 
GAzeti la Mtanzania la leo story yao imeandikwa na "Mwandishi Maalumu" wakati wana mwandishi wao kule Dodoma anaitwa Dilunga,lina kichwa kisemacho, "Zitto Kabwe hoi bungeni" likiwa na habari ya mapema yaani imeandikwa na wenyewe na kupelekwa.. walijaribu kufanya hivyo katika magazeti mengi ikashindikana ila hapo kwa sababu ni la kwao wakaweka. Hiyo imewadhalilisha sana. Inaonekana Mhariri amewaumbua kwa kuweka "mwandishi maalumu' kukwepa kuwajibika kitaaluma kwa wanaaaluma wenzake ambao wameona dhahiri kuwa si ya mwandishi wa gazeti hilo.

Huo ndio UTATU MTAKATIFU unajidhihirisha.. EL alikua akiishi nyumba moja na Rostam.. alipopanda akamwachia nyumba Rostam na KAramagi akakaribishwa na Rostam... Iko kazi hapo.. hayo ni makoti ya hali halisi, ukweli uko ndani ya hayo makoti
 
Wanasheria wawili wamenipigia simu wanasema, wa kwanza "jana usiku nilitamani kumaliza hasira katika TV yangu., lakini nikavumilia kabla ya kuamua kwenda kulala... Nina hasira na kuanzia leo niko tayari kwa gharama zote kuhakikisha hii vita inaendelea. Sina ushabiki na chama chochote" , mwingine akasema, "nilikasirika sana na ujinga wa kupita kiasi ulioonyeshwa na wabunge wetu wa CCM, lakini nadhani huu si wakati wa kukasirika ila ni wakati wa kutafakari HATMA YA TAIFA LETU... Tunakwenda wapi? Je, nani atazuia UFISADI ikiwa PCCB inasafisha wala rushwa, inafunga midomo waandishi wa habari na Bunge linegeuka mtetezi wa ufisadi... AMANI YA TANZANIA INAELEKEA KUTOWEKA SIKU SI NYINGI"
 
Binafsi nilijua ngoma itakuwa nzito kwa sababu kuu moja:
Wakati Ndugu Zitto anatoa hoja/swali kabla ya kuwasilisha hoja hii iliripotiwa kuwa huyo waziri wakati anasaini huo mkataba huko Uingereza, alikuwa safarini na mkuu wa kaya. Kwa hali hiyo, niliamini kuwa bosi mwenyewe alitoa baraka zake. Isingekuwa rahisi waziri asaini, akiwa ziarani na rais, pasi na rais kujua au kubariki, ilhali ni yeye aliyesema mikataba mipya sasa basi mpaka kieleweke!

Hata hivyo, kwa upande mwingine, ikiwa ni kweli mkataba huu una masharti mazuri KIDOGO kuliko ile mingine ya awali, basi ni afadhali.

Taarifa nilizonazo ni kwamba hawa jamaa walitaka kusainisha mkataba huu mwishoni mwishoni mwa utawala wa MJASIRIAMALI, somehow, ikashindikana. Alipokuja Muungwana wakataka kusaini chapchap, lakini jamaa somehow akachelewesha kubariki zoezi hilo. Binafsi nilipata habari hizi za mzee "kuwakwepa" hao wawekezaji kuhusu mradi huo tangu mwaka jana kwani walitaka akazindue mradi huo tangu mwaka jana. Najua vyombo vya habari (magazeti ya BONGO) vimekuwa vikiandika siku nyingi kwa kurudia rudia habari ya mradi huo (hata pale kulipokuwa hamna kitu kipya) kwa nia ya kuweka msukumo fulani kwa serikali (mtazamo wangu).

Kuchelewa kusainiwa kulikuwa kukinipa faraja kuwa serikali kwa ujumla na Muungwana in particular, wameamua kusimamia kidete mikataba safi katika sekta hiyo. Sasa hili la kusaini katika mazingira ambayo kidogo (kama si sana!) yameleta maswali kumenichanganya. NDIYO MAANA NAAMINI KUWA MZEE ALIBARIKI ZOEZI HILO!

Spot on bro!
 
HAya mwingine anakuja na kusema, "HUyu Zitto hajui kwamba anataka kumharibia KAramagi katika mbio zao za kuwa Waziri wa Fedha? kama THISDAY walivyomharibia Dr Dau kushika TRA?" aache kabisa kuwagusa wenzake ambao wako busy kupanga safu
 
Mi nadhani hoja ya msingi iwe ni mkataba huu aliosaini Mh. Karamagi kama una maslahi ya kweli kwa nchi na tushawishiwe na tujiridhishe kuwa huu mpya wa mwezi feb. 2007 ni tofauti na ile mingine ambayo wajanja wachache walijipatia 10% zao wakawaingiza Watanzania mkenge!
Sasa basi na mimi kwa kuchelea kutoka kwenye hoja ya msingi napendekeza, napigia debe na nataka mkataba huu mpya uwekwe wazi bungeni ujadiliwe ili na sisi wananchi tupate kujua yaliyomo na niliyogusia hapo awali tuyapambanue.
Bado nakubaliana na hoja ya Hayati Mwl. Nyerere kuhusu kuyaacha madini mpaka ambapo sisi wenyewe tutajenga uwezo wa kuyachimba. Pili nilifarijika jiasi na taarifa aliyoitoa Mh. Rais ya kwanza, kusitisha uingiaji mpya wa mikataba na pili, mapitio ya mikataba ya zamani.
Nisingependa tena kupata aibu ya viongozi wangu wa nchi wakienda kutudhalilisha Watanzania nje ya nchi kwa kuwaomba waanze kulipa kodi ya mapato..aibu! Wakati mikataba waliingia wenyewe wakiangalia matumbo yao tu na kuwatoa kafara Watanzania!

Ya zitto kusimamishwa vikao vya bunge naomba nitakapopata majibu ya Mh. Karamagi hapa JF, niyapitie kama ambavyo napitia hoja Mh. Kabwe, ndo nitoe maoni yangu
 
Mtanzania,
Nisaidie kunitafutia hiyo kozi 🙂
Gagnija,
Hapa nilipo zipo nyingi tu ila tatizo ni muda na mapesa ya kulipa.

Haina maana matatizo yote yataisha ila kuna makosa ambayo ni very obvious, hayo yanaweza kutatuliwa kwa course moja tena ya bei poa kabisa. Vipi huko uliko hakuna Open University? Ungelikuwa UK, ningekuambia jaribu OU au kwenye chuo chochote kwenye mji wako. Uzuri wa nchi za wenzetu kila palipo na mapungufu unaweza kwenda kusoma.

Siku moja nilikuwa bored nikaamua kusoma kupika kwa wiki mbili kwa pounds 50. Nikifurahi nawapikia wanangu.
 
Mtanzania,
Hapa nilipo tunayo OUT, lakini katika kona ya nchi ninayoishi sidhani kama itakuwa rahisi. Hata hivyo nashukuru sana kwa ushauri.
 
EL alikua akiishi nyumba moja na Rostam.. alipopanda akamwachia nyumba Rostam na KAramagi akakaribishwa na Rostam... Iko kazi hapo.. hayo ni makoti ya hali halisi, ukweli uko ndani ya hayo makoti

This is such a monumental discovery! Enhe, leta habari za mabibi zao sasa.
 
Wanasheria wawili wamenipigia simu wanasema, wa kwanza "jana usiku nilitamani kumaliza hasira katika TV yangu., lakini nikavumilia kabla ya kuamua kwenda kulala... Nina hasira na kuanzia leo niko tayari kwa gharama zote kuhakikisha hii vita inaendelea. Sina ushabiki na chama chochote" , mwingine akasema, "nilikasirika sana na ujinga wa kupita kiasi ulioonyeshwa na wabunge wetu wa CCM, lakini nadhani huu si wakati wa kukasirika ila ni wakati wa kutafakari HATMA YA TAIFA LETU... Tunakwenda wapi? Je, nani atazuia UFISADI ikiwa PCCB inasafisha wala rushwa, inafunga midomo waandishi wa habari na Bunge linegeuka mtetezi wa ufisadi... AMANI YA TANZANIA INAELEKEA KUTOWEKA SIKU SI NYINGI"

PCCB = Preventing and Cleaning Corrupt Burglers
PCCB = Previnting and Cleaning Corrupt Bandits
 
Malecela sawa na Kingunge wana mawazo finyu na ya kizamani , wamejewa fitina na usongo sawa na Mudhihiri nk lazima asimame aonyeshe u CCM kuwa mbele.

Zitto is a hero maana hakuna maisha bila ya historia . Tanzania we had Mwalimu, Kenya D Kimathi, SA -Mandela, Ghana -Nkrumah nk .Huwezi kuchimba dhahabu ama almasi bila kwanza kuingia machafuni uzoe taka then upate dhahabu ikiwa safi baada ya kutoka jasho . Zitto kaza uzi historia na sisi Watanzania tuna angalia, hongera sana na usijute kusimamishwa maana Sitta alionyesha nia ya kutaka usimamishwe tangia mwanzoni akiwa na wapambe wenzake akina Buriani.
 
Uwe unasoma kwanza kabla ya kupost. Hiyo habari imeshajadiliwa sana kwenye thread nyingine.

Siyo rahisi kama unavyodhani kupitia threads za JF ili kuhakikisha kwamba thread unayotaka kutuma imeshatumwa au la. Halijaharibika neno kwani hii inaweza kuunganishwa na ili nyingine au ikafutwa.
 
Bunge la chama kimoja halitatufikisha popote Watanzania! Yaani ishu zote Bungeni Watanzania zaidi ya milioni 35 tubategemea wabunge wanne au watano ambao ndio wanao ongea kila siku...Zitto Kabwe, Halima Mdee, Dr Slaa, Ndesamburo basi! Wengine wako wapi?

Sheria ya chama kuwa na mamlaka ya kumfuta uachama mbunge na akawa si mbunge tena kwa kufukuzwa uachama kunafanya wabunge wa CCM wawe mabubu!!

Kwa kifupi mfumo mzima wa utawala wa nchi hii una walakini mkubwa sana na umepitwa na wakati. Katiba inatakiwa kuandikwa upya au la basi ifanyiwe reshuffle kubwa sana!

Yote ni yote, adui yako muombee njaa. Viongozi wetu wanahahakikisha Watanzania ni wenye njaa muda wote, wasio na elimu ya kutosha ili iwe rahisi kuwarubuni na hata kuwaibia kura kipindi cha uchaguzi! Niliwahi kusema hapa kwamba kizazi hiki hakitashuhudia mabadiliko nchi hii, labda kizazi kijacho! LABDA!!
 
Hoja ya mheshimiwa Zitto, nitaiweka hapa.

MAELEZO YANGU KUHUSU HOJA YA KUUNDWA KAMATI TEULE YA BUNGE KUCHUNGUZA MAPITIO YA MIKATABA YA MADINI NA MAZINGIRA YA KUSAINIWA KWA MKATABA (MDA) MPYA WA MADINI WA BUZWAGI KULIKOFANYWA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWA NAZIR KARAMAGI (MB) HUKO UINGEREZA MWEZI FEBRUARI 2007.
{Kanuni 104(2)}

1. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako Tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.

2. Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako Tukufu nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za Mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…… naomba kutoa taarifa rasmi …… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa Madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba ya Madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Desemba, 2005. Mwisho wa kunukuu.

3. Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.

4. Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha Bungeni wakati wa mjadala wa Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007 nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:

i. Kusainiwa kwa Mkataba mpya wa wa Madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London Uingereza na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
ii. Kuondolewa kwa kipengele katika sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako Tukufu.

5. Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo,

a. Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.

6. Mheshimiwa Spika, Wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la Mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo, nanukuu,

“Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya Migodi, Mgodi wa Buzwagi ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya sasa ya bei ya Dhahabu uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, Mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani”. Mwisho wa kunukuu.

7. Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa Rais alikwishapiga marufuku kusainiwa kwa mikataba mipya ya Madini mpaka hapo sheria za madini zitakarekebishwa. Akisoma hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mnamo tarehe 17/7/2006, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Ibrahim Msabaha alilitaarifu Bunge kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezuia kusainiwa kwa Mikataba mipya ya Madini. Nimeambatanisha Hansard ya siku hiyo kama uthibitisho wa kauli hiyo. Sasa inakuwaje Waziri wa Nishati na Madini kwenda kinyume na maagizo ya Rais? Tena nje ya Nchi?

7. Mheshimiwa Spika, Licha ya Marufuku hiyo ya Rais, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa Bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.

8. Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini Mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je Waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?

9. Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako Tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile Waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio Mgodi.

10. Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya ‘Barrick Gold Corporation-Global operations-Africa- Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii ninaiambatanisha katika hoja hii.

11. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninanukuu. “A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive EIA approval”.

12. Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, Je serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na kampuni ya Barrick?. Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?

13. Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Tulawaka na North Mara?

14. Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/98), pamoja na mambo mengine kinataka leseni yeyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.

15. Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini Mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa? Kulikuwa na haraka gani? Maslahi ya Taifa yalizingatiwa?

16. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya Waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za Kiserikali, kama kamati ikimshauri Waziri na Waziri akakataa ushauri huo, inampasa Waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. Je Waziri alifuata ushauri wa kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka wa kusaini Mkataba huu?

17. Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, Mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. Ni mingapi kati ya Mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa Mkataba kusaniwa Uingereza? Je Mkataba umeandikwa “signed in London ……..” au “signed in Dar es Salaam …..? Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.

18. Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la Kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini wabunge wataamua kwa maslahi ya Taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.


b. Kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’

19. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, ninanukuu “..….kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa Bungeni mwaka 2001 kwenye Bajeti kikabadilishwa…..” Mwisho wa kunukuu.

20. Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.

21. Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14 ya 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninanukuu

‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act’

22. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/1998) kinazungumzia Mrahaba wa Madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge?

23. Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.

24. Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha Mhe. Basili Mramba

“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
(v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998”….. Mwisho wa kunukuu.

25. Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002 nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya Madini haitajwi.

26. Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?

27. Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya Waziri ni ya kweli. Je kwa nini makampuni ya Madini ambayo yameingia Mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?

28. Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya Serikali na ufisadi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.



…………………………….
KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI



Nampongeza sana huyu kijana kwa ujasiri wa hali ya juu.
Nitaweka ya kagamagi baadae ili tuweze kuchambua moja baada ya nyingine ,tumalize kwanza hii ya zitto the great to me.

Hii haitusaidi chochote bila kujua majibu ya waziri. Ungeambatanisha majibu ya waziri ndipo tungeweza kulinganisha hoja na jibu na hivyo kujua wapi hoja zilizidi majibu na wapi majibu yalipozidi hoja.
 
Mapak kieleweke shukrani kwa kutuwekea hoja za Zitto, ngoja nizipitie.

Mzee Lunyungu
Good to see you back!!
 
Back
Top Bottom