The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

lenye mwanzo lina mwisho,walalahoi tumechoka

Walalahoi walishachoka siku nyingi sana....hatari ni pale walalahai nao wanapochoka na kuingia mitaani....hakuna dola linaloweza kuzima moto wenye baraka na ushiriki wa walalahai.....

Kaka JK wakati umefika wa kuchagua CCM ama Tanzania. Tafadhali chagua Tanzania. Chondechonde kaka tunaipenda Tanzania yetu....hatuna ulazima wa kujikuta ligi moja na Zimbabwe na wengineo waliokataa kusoma alama za nyakati

Tanzanianjema
 
[QUOTE=Tanzanianjema; ...hakuna dola linaloweza kuzima moto wenye baraka na ushiriki wa walalahai.....

nchi imegubikwa na wingu wa majambazi wanaotuibia machoni/mchana kweupee, hao walalahai wanafuata hao majambazi kiasi mlalahoi hawezi kusikika.hapo wanasubiri watoe bomu lingine.
wananchi wameamka kweli lakini ikifika kipindi mwananchi huyo huyo atimize wajibu wake kwa kura anapewa kula anajisahau
 
Hawa watu wa CCM ngoja waendelee kuwa na jeuri yao na kiburi."THE DAY IS COMING" watalala na kuamka na kujikuta wako nje.Tabia yao inawalazimisha na kuwapeleka Watanzania kwenye point of no return.Tusisahau kila kilicho na mwanzo kina mwisho.

Unasema kweli!
 
Nimeona kundi la waandamanaji na nafikiri ni mwanzo mzuri. Muhimu ni kuhakikisha huko kunara kwa Zitto kunaambatana na vyama vya upinzani kuungana na kushirikiana zaidi.

Makosa makubwa yatakuwa ni CHADEMA kuiteka hii hoja na kupuza vyama vingine, hayo ndio makosa aliyoyafanya Mrema.

Ni jambo lisilopingika kwamba hata ndani ya CCM kuna watu ambao hawapendi mabavu ya CCM na wangetaka upinzani wawe na wabunge wa kutosha ili kuzuia bunge kuburuzwa. Niliona prof. Mwandosya alivyokuwa uncomfortable wakati wa mjadala wa Zitto.

Kitila, umeongelea middle class, hao ndio inatakiwa mtumie kila mbinu kuwabadili maana hao wakibadilika juu mwisho wa watawala umefika. Middle class hawabadiliki kirahisi kwasababu wao wana mambo mengi ya kupoteza, wanafaidika na system iliyopo na pia ni wasomi kwahiyo wanaangalia pande zote za shilingi kabla ya kuruka. Zitto ni kijana kwahiyo anaweza kutumika sana kuwashawishi vijana wasomi na pia kwenye vyuo vikuu.

Ila ningelikuwa mimi nisingelimpandisha Zitto kwenye gari la pesa nyingi kama hilo, badala yake angetumia gari la kawaida tu kama pick up. Tamaa ya high life ndio inawafanya hao viongozi wetu wachukue rushwa.
 
Mtanzania umeleta mawazo mazuri lakini umemaliza kwa kuzua hoja ambayo itaondoa maana ya mchango wako . Najua hapo UK unaona mengi lakini sasa kuna uhalisia wa maneno. Hammer ya Zitto hajanunua kwa pesa ya walipa kodi , bali kapewa zawadi na marafiki zake ambao wanapenda juhudi zake za kuwatetea Watanzania . Wanaona maisha ya Zitto yalivyo ya kawaida sana .Zitto ana prado ya Ubunge lakini ni mbovu sana na haina nguvu .Zitto hakununua prado mpya bali alinunua hapa hapa Dar ikiwa ni second hand ,sasa kwa hali ya jana ambayo sisi tulikuwa pale jangwani na safari yake ndefu ya kutoka Dodoma na watu wengine walio kuwa naye na kwa kuwa gari lile kapewa zawadi na Rais wa Ujerumani ambaye anautambua mchango na uchapaji kazi wa Zitto kabla hajaanza kazi ya Ubunge . Now point ni msimamo wa Zitto kuungwa mkono na si swala la gari alilo kuja nalo .Jamani tusiwe wepesi wa kuwa ma spinning doctors maana ndiyo kazi ya wakubwa wetu hapa Tanganyika na sisi wadanganyika tunanunua uongo wao na wana tutumia .

Hoja ya Zitto na kusimamishwa kazi za Ubunge kwa muda itabakia kuwa ya Zitto kwa maana ya kitendo cha yeye kutolewa nje lakini hoza iliyopelekea kutolewa kwake ni ya Wabunge wote na wapenda maendeleo ya Tanzania yaani sisi Wadanganyika. Let us kindly stick on the main issue and no trvial issues .

Pia siamini kama Prof.Mwandosya was unconfortable as you have claimed . Pale ni ni Bungeni na alikuwa na nafasi ama haki ya kusimama na kukataa ama ku comment akiwa kama Mbunge wa wananchi na msomi anayetegemewa na Taifa hili lakini alikuwa kimya na alisema ndiyoooooooooooooooooooooooooooooo Zitto asimamishwe .
 
Mtanzania umeleta mawazo mazuri lakini umemaliza kwa kuzua hoja ambayo itaondoa maana ya mchango wako . Najua hapo UK unaona mengi lakini sasa kuna uhalisia wa maneno. Hammer ya Zitto hajanunua kwa pesa ya walipa kodi , bali kapewa zawadi na marafiki zake ambao wanapenda juhudi zake za kuwatetea Watanzania . Wanaona maisha ya Zitto yalivyo ya kawaida sana .Zitto ana prado ya Ubunge lakini ni mbovu sana na haina nguvu .Zitto hakununua prado mpya bali alinunua hapa hapa Dar ikiwa ni second hand ,sasa kwa hali ya jana ambayo sisi tulikuwa pale jangwani na safari yake ndefu ya kutoka Dodoma na watu wengine walio kuwa naye na kwa kuwa gari lile kapewa zawadi na Rais wa Ujerumani ambaye anautambua mchango na uchapaji kazi wa Zitto kabla hajaanza kazi ya Ubunge . Now point ni msimamo wa Zitto kuungwa mkono na si swala la gari alilo kuja nalo .Jamani tusiwe wepesi wa kuwa ma spinning doctors maana ndiyo kazi ya wakubwa wetu hapa Tanganyika na sisi wadanganyika tunanunua uongo wao na wana tutumia .

Hoja ya Zitto na kusimamishwa kazi za Ubunge kwa muda itabakia kuwa ya Zitto kwa maana ya kitendo cha yeye kutolewa nje lakini hoza iliyopelekea kutolewa kwake ni ya Wabunge wote na wapenda maendeleo ya Tanzania yaani sisi Wadanganyika. Let us kindly stick on the main issue and no trvial issues .

Pia siamini kama Prof.Mwandosya was unconfortable as you have claimed . Pale ni ni Bungeni na alikuwa na nafasi ama haki ya kusimama na kukataa ama ku comment akiwa kama Mbunge wa wananchi na msomi anayetegemewa na Taifa hili lakini alikuwa kimya na alisema ndiyoooooooooooooooooooooooooooooo Zitto asimamishwe .


Daaaaaaaaamn. hilo hummer lake haendagi nalo bungeni. alafu ni ya aina gani hiyo H1, H2 au H3?
 
Wazee pia tumtumie ujumbe rasmi mheshimiwa Zitto, kwamba ni muhimu akagombea ubunge tena 2010!

Halafu tu-stick na ishu, hummer sio tija na wala hatuko tena kwenye siasa ya uajamaa na kujitegemea, kwa hiyo ni rukhsa kuwa na gari lolote, kuwatetea wanyonge sio lazima na wewe uwe masikini masikini, na kiongozi safi sio lazima awe masikini masikini, hizo ndio zilikuwa zidumu fikra za mwenyekiti!

Hatuwezi kuangalia nyuma tena! Hongera Mbunge Zitto kwa hii hoja ya karimagi, sasa tukazanie kuundwa kamati ili kuona vipi na mikataba mingine nayo?
 
Ila ningelikuwa mimi nisingelimpandisha Zitto kwenye gari la pesa nyingi kama hilo, badala yake angetumia gari la kawaida tu kama pick up. Tamaa ya high life ndio inawafanya hao viongozi wetu wachukue rushwa.

..neno la busara!
 
Field Marshall ES said:
Halafu tu-stick na ishu, hummer sio tija na wala hatuko tena kwenye siasa ya uajamaa na kujitegemea, kwa hiyo ni rukhsa kuwa na gari lolote, kuwatetea wanyonge sio lazima na wewe uwe masikini masikini, na kiongozi safi sio lazima awe masikini masikini, hizo ndio zilikuwa zidumu fikra za mwenyekiti!

..image ni kitu cha muhimu!
 
leopc2.jpg

Zito Kabwe akisindikizwa kwenye viwanja vya Jangwani kwenye maandamano


48833537jr3.jpg

Umati wa watu uliojaa kumpokea Zito Kabwe kwenye viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam


35280156yt4.jpg

Umati wa watu Jangwani waliokuwa wanamsikiliza kwa makini
Mbunge wa Kigoma Zito kabwe kwa kulikosoa Bunge la serikali ya JK



13912743ig9.jpg

Umati wa wakazi wa Dar Es Salaam uliopigwa na mvua

katika maandamano ya jana ukidai katiba mpya na kuwafichua mafisadi wa mikataba ya madini.



79655928hn9.jpg

Viongozi wa vyama mbali mbali vya upinzani walikuwepo

kuweka msimamo wao thabiti



77658444ip5.jpg

Maandamano yakikaribia Jangwani.

98582531ae2.jpg

Waliokuwa kwenye msafara wa Zito
wakiwapungia maelfu ya wananchi waliokusanyika Jangwani



40868858fb1.jpg

Freeman Mbowe akiteta mara baada ya kuingia Jangwani.

Picha kutoka haki Ngowi blog
 
Very well said Es . Hapa the issue ni Karamagi na wana CCM kutuibia mchana .This guy Karamagi he went far kiasi cha kumwita Mh.Zitto more than 5 times na kumwambia alitamani kitu gani apewe na aachane na issue ngumu ya kutuibia .

Hongera Zitto
 
Viva, Kabwe viva!

96648.jpg

Member of Parliament for Kigoma North (CHADEMA), Zitto Zubery Kabwe shakes hands with Dar es Salaam residents who turned up to welcome the MP who has been suspended to attend the parliamentary seatings for four months. Picha kutoka IPPMEDIA.

Deus Bugaywa

MOJA ya misingi ya demokrasia ni pamoja na kuwa na mihimili mitatu ya dola inayofanya kazi moja ya kumhudumia mwananchi, lakini ambayo ni tofauti sana kutoka mhimili hadi mhimili.

Serikali kama moja ya mihimili hiyo ni mtendaji mkuu wa kazi za siku kwa siku za nchi, na Bunge kwa upande wake ni mtunzi wa sheria ambazo zinatafsiriwa na Mahakama ambao ni mhimili mwingine wa dola.

Bunge, lakini kwa kupitia uhalali wake wa kuwa sauti ya wenye nchi, wananchi, kwa serikali yao likapewa heshima ya kusimamia, kudhibiti na kuhoji pale inapobidi juu ya mienendo mbalimbali ya serikali katika mchakato wake wa kutoa huduma kwa jamii, yaani wananchi.

Hivyo basi katika mihimili inayotegemewa kuifuatilia na kuibana serikali katika kila jambo linalotia shaka au kuleta maswali yasiyo na majibu kwa wananchi ni Bunge, kwa kuwa lenyewe ndiyo sauti yao kwa serikali.

Wabunge kwa maana hiyo hawapaswi kwa namna yoyote ile kubembelezana na serikali pale masilahi ya nchi yanapokuwa yanawekwa katika mazingira tata, na kuibua hisia zisizo nzuri miongoni mwa wananchi, kwa kuwa wao wanawajibika moja kwa moja kwa mwananchi.

Kuchaguliwa kwa wabunge kupitia vyama bado hakuondoi jukumu lao la kuwa wasemaji wa wananchi kwa serikali yao, wanapaswa wahoji, wadadisi na wadurusu lolote, popote ili mradi tu jambo hilo lina masilahi ya nchi.

Vile vile serikali inayojiamini kuwa ni mtumishi mwadilifu kwa watu wake wala haina haja wala sababu ya kuhofia Bunge au kuweka mashinikizo ya kuathiri shughuli za Bunge kwa kuwa wanajua walichokifanya ni chema na kwa nia njema na kwa manufaa ya taifa, hawaogopi hoja wa kuulizwa chochote juu ya utendaji wao, wala hawana kitu cha kuficha.

Ukiona serikali inafanya kila linalowezekana kujenga ‘uswahiba' na Bunge kwa gharama ya Bunge kuhama katika wajibu wake wa msingi wa kutetea masilahi ya nchi bila kujali mtoa hoja ni wa chama gani, basi ujue hapo kuna mushikeli na yamkini kuna jambo ambalo linafichwa.

Baadhi ya wabunge wa chama tawala wamenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari wakitamka hadharani kwamba wanazibwa midomo, kwamba linapokuja suala la kujadili hoja mahsusi bungeni kwa maana ya kujadili masuala ya masilahi kwa wananchi na taifa lao, haijalishi wao matatizo hayo yanawahusu na yapo mengi majimboni kwao kiasi gani, wanatakiwa tu waunge mkono hoja ilimradi tu wao ni wa chama tawala na chama ndicho chenye serikali.

Ndiyo maana haikushangaza sana na badala yake iliwaudhi watu wengi, kiasi cha kuwapa tabu kuamini kama mambo haya yanaweza kutendeka Tanzania, pale Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zito Kabwe, alipotoa hoja ya kutaka iundwe tume kuchunguza mazingira yaliyopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini mkataba wakati kukiwa na kauli ya serikali kusitisha utiaji saini wa mikataba mipya wakati hii ya zamani ikiwa inapitiwa na zaidi sana mkataba huo kusainiwa nje ya nchi.

Siku ya mjadala kwa sababu ya majukumu sikupata nafasi ya kuangalia mjadala huo moja kwa moja, lakini namshukuru rafiki yangu mmoja aliyeniambia kama sikuona mjadala huo wa hoja binafsi ya Zito, ilikuwa lazima niuone kwa gharama yoyote ile.

Kwa maelezo yale ya mwanaharakati mwenzangu, nilidhamiria kutimiza azima hiyo, hivyo nililazimika kuangalia marudio usiku saa nne, niliweza kufuatilia mjadala huo mpaka saa saba kama na robo hivi, lazima niseme ukweli usiku huo nilikuwa na usingizi wa mang'amu ng'amu, nilikuwa nashangaa kama kweli nchi hii tumefika hapo.

Nilidhani ni mimi tu, asubuhi tu nikakutana na mama mmoja ambaye katika mazungumzo aliniambia mumewe naye kama mimi alikuwa anafuatilia kikao kila usiku ule, mwenzangu alienda mbali, yeye shinikizo la damu lilipanda na asubuhi hiyo hakuweza hata kwenda kazini kwa ajili ya kutuliza hali iliyosababishwa na mijadala hiyo.

Mpaka kufika mchana wa siku hiyo, nilishapokea simu na ujumbe mfupi mwingi ukihoji ni nini kinafanyika na Tanzania inakwenda wapi, mimi kwa vile kazi ni hii kuujulisha umma hiki na kile, nahisi ujumbe umefika.

Tukirudi kwenye mada nashindwa kupata tafsiri sahihi ya kulidanganya Bunge ni ipi na inatumika wapi na kwa nani, Mheshimiwa Zitto amepewa adhabu na Bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge najiuliza sipati jibu, kulidanganya Bunge kunaanzia wapi na kunaishia wapi.

Nakumbuka wakati akichangia mjadala wa bajeti, Mbunge wa Nzenga, Lucas Serelii, alitishia kuzuia bajeti za Wizara ya Miundombinu na Waziri Mkuu kwa kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha uliotangulia huu, wizara hiyo ilisema bungeni katika mwaka wa fedha huo ingeweza kujenga barabara kadhaa jimboni kwake na haikufanya hivyo.

Mheshimiwa huyu alitishia hivyo kwa kuwa aliahidiwa na waziri, lakini hakutimiza ahadi hiyo, ndiyo maana alitishia kuzuia bajeti ya wizara hiyo kwa kuwa alidanganywa na kwa maana hiyo Bunge lote lilidangaywa, na hatukusikia hata harufu ya hoja ya kumwadhibu waziri kwa kuwa kutoa ahadi na kutoitimiza ni uongo.

Wakati wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Waziri Karamagi alibanwa kuhusu ahadi ya wizara yake kupeleka umeme huko Peramiho, kwamba alichoahidi sicho na kwamba yeye alidanganya Bunge na wananchi wa Peramiho, mpaka waziri mkuu walipoingilia kati kuokoa jahazi, hatukuona hata dalili tu ya kumchukulia hatua.

Haya yote tulidhani ni busara za Spika zinatumika kwa kuwa alishasema mwenyewe mapema kwamba Bunge lina kanuni nyingi sana zilizopitwa na wakati na hivyo inapokuwa lazima busara za Spika zingetumika ili kurekebisha hali ya mambo, je, busara za Spika zilikuwa wapi wakati wa hoja ya Mudhihir dhidi ya Zitto?

Hoja iliyotumika kumwadhibu ina uzito gani ukilinganisha na yale yaliyoibuliwa na maelezo ya mtoa hoja tangu wakati akichangia bajeti ya Waziri wa Nishati na Madini?

Je, si kweli kwamba wengi wa wabunge hata wa CCM hawakujua kwamba mgodi wa Buzwagi umeuzwa, tena kwa mkataba kusaniwa nje ya nchi, asingekuwa Zito na utundu wa udadisi wake si mpaka leo, tungekuwa gizani wakati mali yetu imeuzwa bila wenyewe kuwa na taarifa achilia mbali kujua mkataba wa uuzwaji wake?

Hili busara za Spika hazikuliona mpaka akasimamia kidete kusimamishwa kwa mbunge huyu? Katika hatua nyingi za mjadala huo Spika alisikika akisema kuwa yeye anafuata kanuni tu, je, si huyu huyu aliyetuahidi kutumia busara zake kwa kuwa kanuni nyingi zilikuwa zimepitwa na wakati?

Je, Spika aliona ni vyema sana kutumia busara zake katika kumuepusha na adhabu Mheshimiwa Malima wakati alishasema uongo bungeni, tena uliothibitishwa na tume iliyotumia shilingi milioni 100 za walipa kodi wa nchi hii, lakini busara hizo zikakosekana kwenye suala la Zitto ambalo mbali na uongo wake kutothibitishwa bila kuacha shaka yoyote, lakini pia hoja yake imewafungua macho Watanzania na kuilazimu Wizara ya Nishati na Madini kutoa maelezo ambayo katika hali ya kawaida haikuwa tayari kuyatoa mpaka hoja hiyo ilipoibuliwa?

Je, Waziri Chenge pamoja na ukongwe wake bungeni kwa kuwa mwanasheria wa serikali kwa miaka 10 na zaidi kama mwenyewe alivyosema, tumweke kundi gani anapojenga hoja ya kitoto kwamba Zito anataka kuganga njaa, eti anataka tume iundwe ili apate posho za tume, Spika hakuona kama hili ni tusi na kudhalilishwa kwa mtoa hoja?

Anataka kutwambia nini, kwamba wana CCM wanapounda tume lengo huwa ni kuganga njaa na kupata posho na si kuchunguza kile kilichoundiwa tume? Huenda ndiyo maana haishangazi kuwa tume nyingi zinazoundwa chini ya serikali majibu yake hayawekwi hadharani, pengine Mheshimiwa Chenge alikuwa anatufungua macho.

Hivi katika hili nani alikuwa na nia njema kwa taifa hili, Zitto aliyekuwa anahoji uharaka wa dharura kiasi hicho wa kusaini mkataba wa kuuza mgodi wa dhahabu kama vile ni nyanya mbivu zinazotarajiwa kuanza kuoza kesho au Chenge ambaye, kama mwanasheria mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu aliyehusika moja kwa moja na kutiwa saini kwa mikataba mibovu isiyokuwa na faida na ambayo tunairekebisha sasa?

Lazima ifike mahali tukubali kuweka masilahi ya taifa letu mbele bila kujali sana sisi ni wapenzi au mashabiki wa nani, na tuna kitu kimoja tu kinachoweza kutufikisha hapo, nayo ni kuwa na maadili yenye nidhamu za Kitanzania ambayo ndiyo yatasaidia sana kutuongoza kufikia malengo yetu kama taifa.

Haya yatakuwa kinga ya watu wetu na taifa letu dhidi ya kila aina ya mbinu chafu na unafiki uwao wote, kwa kuwa ni vigumu sana kuwa na katiba inayokidhi mahitaji yetu bila kutumiwa kwa manufaa binafsi na baadhi ya wajanja ambao si haba nchi hii, ni maadili na miiko ya Kitanzania tu ndiyo inaweza kuliokoa taifa hili.

Ukiangalia kwa mapana hoja ya Kabwe ilikuwa imejikita katika muktadha huo kwamba inawezekana kabisa sheria haikatazi au haisemi chochote, lakini tumueleweje waziri wetu anapokwenda kusaini mkataba wa kuuza mgodi wetu, nje ya nchi, na anakuja anakaa kimya kana kwamba Tanzania ni kampuni yake au familia yake anayoiendesha kwa matakwa binafsi?

Wakati huo huo kila mtu anajua uzoefu wetu na sekta ya madini, kila panapoingiwa mkataba serikali hujifanya haisikii, wote tunakumbuka yaliyojiri katika mgodi wa Bulyanhulu wakati wa hatua za awali za ubinafsishaji wake, Tundu Lissu na LEAT wanalielewa vizuri hili, hakuna asiyejua misukosuko ya wananchi wa Mtakuja huko Geita na fidia zao, halafu leo waziri anasaini mkataba wa madini katika mazingira tata tena nje ya ardhi ya Tanzania na hatuambii wenye mali juu ya kuuzwa kwake, anaonekana ‘shujaa na mzalendo halisi' tunaipeleka wapi nchi hii?

Safi sana! CCM kama hiyo ndiyo njia mliyochagua sawa, lakini mwisho wa siku hii ni mali ya Tanzania si ya CCM, mnaweza kuwa nambari wani lakini linapokuja suala la mali za Tanzania hakuna nmbari wani wala ziro, wote kama raia tuna hisa sawa za mali ya nchi hii Muumba aliyopenda iwe ya kila raia wa ndani ya mipaka ya taifa hili, wala msidhani kuna hali ya kudumu katika maisha haya, hakuna kinachodumu isipokuwa mabadiliko.

Zitto aliwaeleza, akinukuu toleo la mwisho la jarida la Cheche kwamba ‘You can ban organizations, you can liquidate people but revolutionary ideas never die' huo ndio ukweli wa maisha kama zilivyo nguvu za uvutano (gravitational force) ukubali au ukate zenye zipo ili kuishi.

Katika hili la kusaini mkataba nje naomba wabunge waliopinga hoja ya kuundwa kamati teule ya Bunge na kuunga mkono hoja ya kufungiwa shughuli za Bunge Mheshimiwa Zitto watueleze, kimaadili ni sawa kwa waziri kufanya alivyofanya?

Yaani, kusaini mkataba mpya wakati kuna tamko la serikali kusitisha utiaji saini wa mikataba ambalo halijatenguliwa na kusaini mkataba nje ya nchi, wanataka kutuambia huo ndio uadilifu wa nidhamu za uongozi wa Kitanzania?

Wakati muasisi wa taifa hili, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, anawasilisha hoja bungeni ya kuundwa kwa Jamhuri ya Tanganyika Juni 28, 1968, kwa mujibu wa hansard za kikao hicho kipindi cha kwanza (1st session) anasema hivi kuhusu uadilifu, naomba nimnukuu kwa urefu kwa sababu ya unyeti wa suala hili.

"Kama taifa lisipokuwa na maadili yanayoiwezesha serikali kusema ‘Hatuwezi kufanya hivi, huu si Utanganyika' au watu kusema ‘Hatuwezi kuvumilia hili, huu si Utanganyika'. Kama watu hawana maadili ya namna hiyo haijalishi mnaunda katiba ya namna gani. Watakuwa siku zote ni waathirika wa udikteta.

"Tunachotakiwa kuendelea kufanya ni kujenga maadili ya taifa letu, muda wote kuendelea kujenga maadili ya taifa yatakayomwezesha kiongozi yeyote wa nchi kusema ‘Nina mamlaka ya kufanya hivi kwa mujibu wa katiba, lakini siwezi kufanya kwa kuwa huu si Utanganyika' au watu wa Tanganyika, kama wamefanya kosa kumchangua mwendawazimu kuwa kiongozi wao ambaye ana madaraka kikatiba kufanya XYZ, akitaka kufanya hivyo, watu wa Tanganyika waseme ‘Hatukubali hili kutoka kwa mtu yeyote iwe ni kutoka kwa rais au rais kipeo cha pili.'"

Kwanini Mwalimu anasisitiza hili, ni kwa sababu wakati mwingine na hasa kwa mazingira kama yetu, ni vigumu sana kuwa na katiba isiyo na mianya ya kuruhusu watu kufanya lolote wanalotaka. Kinga pekee dhidi ya uhuni wa aina hii ni kuwa na maadili ya taifa ambayo si lazima yawe sheria lakini ambayo kwa akili ya kawaida tu yanatuwezesha kutambua kuwa hili ndiyo na lile siyo.

Ni utetezi dhaifu sana kuanza kutetea uozo ambao uko dhahiri kwa jina tu la kwamba eti katiba au sheria fulani haikatazi au hata haisemi kitu, ni kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa kuacha kutumia kwa makusudi akili alizotupa kwa ajili ya kuutiisha ulimwengu.

Na kwa hatua ya Bunge ya kumsimamisha ubunge, naomba nimpongeze Kabwe kwa kuwa kwanza ametudhihirishia tofauti kati ya wabunge wanaodhamiria kuwa wabunge kwa ajili ya ubunge na wale wanaokwenda huko kwa masilahi, kwamba walikutishia posho na nusu mshahara, hongera kwa kuwakumbusha kwamba ubunge si posho au mshahara, ni kutetea masilahi ya nchi na wananchi wake.

Kama mzee Malecela alivyokuita kwamba wewe ni ‘mwiba', hata mimi namuunga mkono, kama wewe ni mtu makini utakosaje kuwa mwiba kwa Bunge ambalo limesahau wajibu wake na kuwa kama kamati ya chama?

Utakosaje kuwa mwiba kama wewe ni mzalendo halisi na mwanaharakati wa ukombozi halisi wa taifa hili katikati ya nchi ambayo hata mwasisi wake alikiri inanuka rushwa?

Wewe ni jasiri na Mtanzania daima, wewe ni tumaini la Tanzania ya leo na ya kesho ndiyo maana sipatia hata kigugumizi kusema VIVA, KABWE VIVA!

Mungu ibariki Tanzania, uilinde dhidi ya unafiki unaoitafuna!

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu; 0754 449 421 au barua pepe: drbugaywa@yahoo.com
 
Wanaona maisha ya Zitto yalivyo ya kawaida sana .Zitto ana prado ya Ubunge lakini ni mbovu sana na haina nguvu .Zitto hakununua prado mpya bali alinunua hapa hapa Dar ikiwa ni second hand ,sasa kwa hali ya jana ambayo sisi tulikuwa pale jangwani na safari yake ndefu ya kutoka Dodoma na watu wengine walio kuwa naye na kwa kuwa gari lile kapewa zawadi na Rais wa Ujerumani ambaye anautambua mchango na uchapaji kazi wa Zitto kabla hajaanza kazi ya Ubunge.

Pia siamini kama Prof.Mwandosya was unconfortable as you have claimed . Pale ni ni Bungeni na alikuwa na nafasi ama haki ya kusimama na kukataa ama ku comment akiwa kama Mbunge wa wananchi na msomi anayetegemewa na Taifa hili lakini alikuwa kimya na alisema ndiyoooooooooooooooooooooooooooooo Zitto asimamishwe .


Jamani...gari ni issue kama alipewa zawadi na kiongozi wa taifa jingine; haya ndio mambo ya viongozi wetu kupokea zawadi halafu later wanakuja kutuuza jumla jumla. On Zitto nimefurahi kusikia alipewa zawadi kabla ya kuwa mbunge.

Kuhusu Prof Mwandosya...ukishakuwa CCM na uprofesa wako unaingiwa na backteria wa ccm...sishangai kwa yeye kukaa kimya..ila siamini kabisa kama alikuwa anasikitika.
 
Siasa za Tanzania bwana,,, Zito amejitahidi hili halina ubishi lakini jambo ambalo mpaka leo mimi sijaweza kulipa uzito huo ambao wengi wamempa!

Kwangu mimi najua kwamba alikosea na kama sio adhabu nzito kama alivyopewa haya yote yasingejitokeza... time will tell... sijauna msingi mkubwa wa kumpa sifa Zito alizopata na namshauri ndugu yangu achukue heshima hizo kwa tahadhari sana,,, maana wananchi watu wengine pia mzee.

Lakini du! Leo hii Zito anachukua umaarufu zaidi ya kina Mbowe, Hamad Rashid, Dr. Slaa, ambalo kwa mtu anangalia mbali... not yet... Ingawa anajitahidi!

Bado hoja moja naomba hotuba ya JK mei mosi iliyosema kusisainiwe mikataba mingine tena.
Katika Hotuba yake kwenye sherehe ya Mei Mosi/2006,Jk alisema kwamba Utiaji saini mikataba yote ya madini umesimamishwa na serikali ya awamu ya NNE ili kutoa nafasi kwa Mabingwa wa mikataba kuipitia Upya kwani Mikataba iliyopita ina Utata,Alirudia maelezo hayo ya kusimamisha Utiaji saini Mikataba ya Madini huko Afrika kusini kwenye Seminar ya Madini.Sasa Mkataba huu uliotiwa Saini na Karamagi una utofauti na Mingine?"[/QOUTE]
 
Siasa za Tanzania bwana,,, Zito amejitahidi hili halina ubishi lakini jambo ambalo mpaka leo mimi sijaweza kulipa uzito huo ambao wengi wamempa!

Kwangu mimi najua kwamba alikosea na kama sio adhabu nzito kama alivyopewa haya yote yasingejitokeza... time will tell... sijauna msingi mkubwa wa kumpa sifa Zito alizopata na namshauri ndugu yangu achukue heshima hizo kwa tahadhari sana,,, maana wananchi watu wengine pia mzee.

Lakini du! Leo hii Zito anachukua umaarufu zaidi ya kina Mbowe, Hamad Rashid, Dr. Slaa, ambalo kwa mtu anangalia mbali... not yet... Ingawa anajitahidi!

Bado hoja moja naomba hotuba ya JK mei mosi iliyosema kusisainiwe mikataba mingine tena.


Katika Hotuba yake kwenye sherehe ya Mei Mosi/2006,Jk alisema kwamba Utiaji saini mikataba yote ya madini umesimamishwa na serikali ya awamu ya NNE ili kutoa nafasi kwa Mabingwa wa mikataba kuipitia Upya kwani Mikataba iliyopita ina Utata,Alirudia maelezo hayo ya kusimamisha Utiaji saini Mikataba ya Madini huko Afrika kusini kwenye Seminar ya Madini.Sasa Mkataba huu uliotiwa Saini na Karamagi una utofauti na Mingine?"


Jiulize huo mkataba umewekwa sahihi Hotel ya Churchill London wakati huo huo huyo rais unayemsema yupo hapo hapo Churchill anakula kuku kwa mrija. Unafikiri wa kumwamini ni nani hapa? Na wakati huo huo anapiga porojo za kwenda kuwaona Tottenham Hotspurs n.k.

Usanii at its best.
 
Jiulize huo mkataba umewekwa sahihi Hotel ya Churchill London wakati huo huo huyo rais unayemsema yupo hapo hapo Churchill anakula kuku kwa mrija. Unafikiri wa kumwamini ni nani hapa? Na wakati huo huo anapiga porojo za kwenda kuwaona Tottenham Hotspurs n.k.
Dua,

I don't care mkataba usainiwa kaburini ooh kwenye ndege ft 45000ft that is not a point to me,,, the only thing I will care if the content is wrong. full stop.


Naomba url ya hotuba ya JK, ya mei mosi...
 
nnapendekeza shujaa zitooagombee urais mwaka 2010, maana tayari keshawafunika kaka zake kina mbowe na mrema.

ama kweli penye shari huzaliwa heri
 
Dua,

I don't care mkataba usainiwa kaburini ooh kwenye ndege ft 45000ft that is not a point to me,,, the only thing I will care if the content is wrong. full stop.


Naomba url ya hotuba ya JK, ya mei mosi...

How can you care? Your answer says it all.
 
Back
Top Bottom