The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Taarifa zilizoingia muda mfupi ulipita ni kuwa Rais Kikwete amezuiwa na wananchi kuingia Buzwagi, na msafara wake umegeuza njia kurudi Bulyanhulu (ambako tayari alishatembelea). Mbunge anayewakilisha eneo la Buzwagi anaitwa James Lembeli. Huyu bwana alizungumza kabla ya Zitto, na Zitto hakujua kuwa hili suala lilishaletwa Bungeni na Mbunge huyo.

Hili hapa swali lake:

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

(a) Kwa kuwa hivi sasa mchakato wa mgodi mpya wa dhahabu wa Buzwagi ulioko nje kidogo ya mji wa Kahama unaendelea ikiwa pamoja na zoezi la kulipa fidia wananchi na wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa wakifanya kazi katika eneo hilo, zoezi la kulipa wananchi linaonekana kuendelea vizuri lakini zoezi la kuwalipa wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa wakifanya kazi katika eneo hilo hasa eneo la Mwime, Mwendakulima na Chapulwa linaelekea kuwa na matatizo makubwa kiasi kwamba Serikali inatumia nguvu.

Je, Waziri anaweza kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba wananchi hao wachimbaji wadogo wadogo hawanyanyaswi na walipwe pesa zao kabla ya mashimo yao kufukiwa?

(c) Kwa kuwa utafiti wa madini katika eneo la Mwabomba katika Kata Idahina umeendelea kwa muda mrefu hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa wakitumia maeneo hayo kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Je, Serikali inaweza kuwahakikishia wananchi wa kata hii kwamba watafiti hao kama hawajagundua hayo madini wanaondoka?


ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #
Answer From Hon. Ngeleja , William Mganga ENERGY AND MINERALS
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI :

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa James Lembeli, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa James Lembeli, kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia hatma ya wananchi wake katika jimbo lake kutokana na matarajio ya kuanzishwa mgodi wa Buzwagi katika eneo la jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza naomba kumhakikishia Mheshimiwa James Lembeli kwamba wachimbaji wadogo watapata haki zao kama inatarajiwa lakini pia kama alivyokiri mwenyewe kwamba zoezi la kuwafidia wananchi linaendelea vizuri na kwa kweli katika hili ni pamoja na wachimbaji wadogo, fedha kadhaa imeshalipwa na tunaendelea vizuri na tunaomba tu Mheshimiwa James Lembeli tuzidi kushirikiana naye ashirikiane na ofisi yetu na Wizara yetu kwa ujumla ili kuhakikisha kwamba wale wananchi wachache ambao bado hawajachukua na hawajaanza kupokea fidia zao tuwashawishi waanze kupokea.

Mheshimiwa Spika, la pili, utafutaji kama tulivyoeleza kwenye jibu la msingi unafuata sheria, naomba nizidi kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini kwamba Serikali haitaruhusu utafutaji au uchimbaji ufanyike kinyume cha sheria kwa hiyo tunazidi kuwahakikishia wananchi wa Jimbo la Kahama na hasa maeneo ya Mwabomba pamoja na Idahina kwamba watafutaji wa madini walioko pale wanafuata sheria na Serikali inafuatilia kuhakikisha hawakiuki sheria zilizopo ambazo zinawezesha kufanya hizo shughuli.
 
Hii ni hoja ambayo mbunge wa kahama aliitoa bungeni,,,,,, Mheshimiwa Spika, Sekta ya Madini. Wilaya ya Kahama ni miongoni mwa Wilaya hapa nchini ambazo zina madini mengi na hususan dhahabu. Kahama dhahabu inapatikana karibu kila mahali . Hivi karibuni nimesikia redioni kwamba mgodi mpya wa madini ya dhahabu unaitwa Buzwagi utaanza kujengwa nje kidogo ya mji wa Kahama kilomita kama tano. Kwa kutumia Ilani ya Uchaguzi mimi nimeshiriki kikamilifu kuhamasisha wananchi kujiandaa na ujio wa mgodi huu.

Kinachosikitisha ni kwamba nimesikia tayari mkataba baina ya Serikali na Kampuni itakayochimba dhahabu hiyo tayari umeshawekwa. Lakini wananchi wa Kahama wamekuwa wakipiga kelele husasan wale wa maeneo ambako mgodi huu unajengwa hivi sasa wananchi wa Mwendakulima, Mweme na Chapulwa. Kila siku wanalalamikia juu ya fidia zao, hakuna mtu anaweza kuwaeleza kikamilifu kwamba Serikali inasema nini watalipwa kiasi gani na kadhalika. Matokeo yake sasa hivi ni vurugu tupu mpaka inalazimika Mkuu wa Wilaya anakwenda na Polisi kuwajaribu kuwazuia wananchi wenye hamaki wasiwashambulie wale ndugu zangu wa Barricks.

Sasa hili naliona ni tatizo kubwa. Mimi niliamini wazi kuwa Mkataba huu utakuwa tofauti na mikataba ile ya nyuma; na kama umefanyika kwa nini umefanyika kwa siri siri hata mwakilishi wa wananchi wa eneo hilo Mbunge, hana habari. Kinachosikitisha zaidi nimewahi zaidi ya mara mbili kuomba Waziri wa Nishati au Naibu wake aje Kahama azungumze na wananchi wa eneo hilo Kata ya Mwendakulima kuhusu haki zao baada ya mgodi huu kuanza kufanya kazi. Mpaka hii leo hakuna na wanategemea mimi Mbunge niende pale nizomewe halafu ndiyo waje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili ni hatari sana kwa nchi yetu, ninamwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu ahakikishe kwamba Waziri wa Nishati anafika Kahama na si kwenda Blyanhulu, anakuja Buzwagi kuzungumza na wananchi wa Kata ya Mwendakulima.

Lipo tatizo, bado makampuni haya pamoja na kuahidi kwamba yatalipa dola laki mbili kwa Halmashauri ambako wanafanya kazi, nasikitika mpaka jana Barricks walikuwa hawajailipa Halmashauri ya Kahama dola laki mbili. Na sasa wameanza ujanja, barua na maulizo mbalimbali wakati jambo hili ni lipo wazi. Hela hizi zilitakiwa zitumike kwa maendeleo ya wananchi wa Kahama katika mwaka huu wa Fedha unaokwisha, mpaka leo pesa hizo hawajalipa.
 
Wananchi waanze sasa kuishitaki serikali na haya makampuni kwa kutowalipa fidia na rasilimali zao ambazo ni haki yao. Huwezi ati kulipa $200 000 kwa mwaka ati iwasaidie wananchi wakati hicho kiwango ni asilimia ndongo tu ya mshahara wa manager wa mgodi. Hii serikali ya JK ina kiburi sana.


Wao wachukuaji wanaingiza mabilioni ya dollars kwa mwaka halafu hao wanavijiji wanapata $200,000 kwa mwaka halafu Karamagi anaona wametendewa haki. Huu ni upumbavu wa hali ya juu!!
 
Kumbe sio Rais tu!Hata Mbunge wa Jimbo Husika alikuwa hajui kama Mkataba wa kuchimba Madini umekwishasainiwa? Ni nani huyo anayesema kuwa hakuna mazingira ya Rushwa hapa?.Ni Vyema huyu Nizar Karamagi atazamwe vizuri,kwa sababu si Waziri tu!,Nimesikia kuwa ni Waziri Mfanyabiashara!.
 
mwenye uwezo nendeni msikilize Voice of America idhaa ya Kiswahili, nadhani walikuwa na mwandishi kwenye msafara huo.
 
nadhani ili mhe kikwete aweze kuendeleza imani ya wananchi buzagwi ni kwa kwenda na huyo huyo karamagi mpaka hiyo sehemu ya mkutano nae karamagi afafanue kwa kirefu na mapana juuu ya process nzima ya kuweka saini.lakini nilikuwa najiuliza hivi kweli mbunge wa jimbo husika(lenye migodi)alikuwa anafahamu ama ameshafahamishwa juu ya sakata zima?au mhe zitto ndo amemfahamisha siku ile kwa kutoa hoja yake bungeni?kama alikuwa hajafahamishwa nadhani karamagi atakuwa amekosea,mana as karamagi ni jambo la kushangaza kwa kusafiri toka bongo mpaka uk na kisha kumwaga kuwekasaini yake bila hata ya kumtaarifu mbunge wa jinbo husika
 
mwenye uwezo nendeni msikilize Voice of America idhaa ya Kiswahili, nadhani walikuwa na mwandishi kwenye msafara huo.
Afadhali baadhi ya Watanzania wanaanza kutetea haki zao na kupingana na hawa Majambazi wa Serikali ya CCM. Hawa watu hawana utu hata kidogo na hawastahili heshima yeyote kutoka kwa wananchi, Ingewezekana wangemkata hata makofi huyo Kikwete.
 
ndio maana nikasema mpaka source ipatikane otherwise i just regard kama maneno toka mdomoni mwake !
 
Mwanakijiji inawezekana kama ukaweka hiyo link ya habari kutoka VOA??
 
Kumbe sio Rais tu!Hata Mbunge wa Jimbo Husika alikuwa hajui kama Mkataba wa kuchimba Madini umekwishasainiwa? Ni nani huyo anayesema kuwa hakuna mazingira ya Rushwa hapa?.Ni Vyema huyu Nizar Karamagi atazamwe vizuri,kwa sababu si Waziri tu!,Nimesikia kuwa ni Waziri Mfanyabiashara!.

Tena Mfanyabiashara wa MADINI...!!
 
Kikwete apokewa kwa mabango Buzwagi
*Yeye awaambia matatizo yao yatashughulikiwa na mkoa
*Barrick wasema Karamagi aliwaita kusaini mkataba London


Na Mwandishi Wetu, Kahama


WANANCHI wa vijiji vya Kakola na Tegete wilayani hapa, jana walizuia kwa muda msafara wa Rais Jakaya Kikwete kwa mabango wakati akielekea katika mgodi mpya wa madini wa Buzwagi jana. Rais Kikwete yupo katika ziara ya siku nane kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani Shinyanga.


Wananchi wenye mambango na wasio na mabango, walijipanga katikati ya barabara na hivyo kuzuia msafara wa Rais ambao ulikuwa ukielekea katika mgodi mpya wa Buzwagi ambao ulizua mjadala mkubwa baada ya Mbunge wa Kigoma Kasikazini, Zitto Kabwe, kuwasilisha hoja binafsi akitaka kuundwe Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza mazingira ya utiwaji saini wa mkataba wa mgodi huo uliofanyika jijini London Februari mwaka huu na waziri wa nishati na madini, Nazir Karamagi.


Wananchi hao waliokuwa wamejipanga barabarani, walikuwa na mabango mbalimbali yakionyesha shida wanazokumbana nazo kila siku na kumtaka Rais Kikwete kutoa tamko kuhusiana na kero zao. Katika mabango hayo kulikuwa na ujumbe kama "Tunataka huduma za maji na umeme, tunataka barabara ya lami, asilimia 70 ya dhahabu inakwenda sisi tunaachiwa 30, tunakwenda wapi?


Baada ya kusimama, Rais Kikwete aliwaambia kwamba matatizo ambayo wanakumbana nayo kila siku yatashugulikiwa na serikali ya mkoa na kwamba huduma za maji zitakamilika baada ya mradi wa maji kutoka katika Ziwa Victoria kuhitimishwa.


Hata hivyo, Rais Kikwete, wakati akihutubia wananchi katika mgodi wa Buzwagi, hakuongelea mjadala unaondelea sasa dhidi ya mazingira ya utiwaji saini wa mkataba wa mgodi huo huko London, Uingereza. Badala yake, Rais alishukuru kampuni ya Barrick kwa kukubali kutoa fungu katika mapato yake na kuzipa halmashauri za wilaya zinazozunguka migodi hiyo. Pia alishukuru kampuni hiyo kwa kujenga nyumba za wanakijiji ambao walikuwa katika maeneo ya machimbo ya migodi ya dhahabu.


Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Barrick, Deo Mwanyika, alisema ni kweli mkataba wa mgodi wa Buzwagi ulisainiwa nchini Uingereza. "Ni kweli kabisa mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini nchini Uingereza baada ya kuambiwa kufanya hivyo na Wizara ya Nishati na Madini," alisema Mwanyika.


Alisema ulipowadia wakati wa kusaini mkataba wa mgodi huo, alimpigia simu Waziri Karamagi, lakini yeye alimwambia aende wizarani kwa ajili ya kupata maelekezo. Mwanyika alipokwenda wizarani, aliambiwa waziri alikuwa Uingereza na Rais Kikwete hivyo, wampekekee huko akausaini.

Pia Mwanyika alisema ni kweli walisaini mkataba huo hotelini kwa kuwa Barrick hawana ofisi London bali ofisi yao ipo Canada. Hata hivyo, hakueleza kwa nini hawakusaini mkataba huo katika Ubalozi wa Tanzania ulioko London Uingereza. Mwanyika alisema walilazimika kumfuata Waziri kwa kuwa muda wa kusaini mkataba ulikuwa unaelekea ukingoni.


Mapema Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi wa Kakola kuwa hawatahamishwa kutoka katika kijiji hicho ili kutoa nafasi ya kupanua mradi wa machimbo ya dhahabu ya Bulyanhulu. Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi hao akiwa njiani kuelekea Kahama ambako alifungua shule ya sekondari na nyumba za wananchi wa Buzwagi zilizojengwa na kampuni ya Barrick kama fidia ili kupisha mgodi mpya wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni hiyo.


"Hamtahama na matatizo yenu mengine mtaendelea kuyazungumza ili mpatiwe ufumbuzi," alisema Rais Kikwete. Vilevile, aliwahakikishia wananchi hao wa Kahama kuwa ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni zitatimizwa kama vile kuleta maji kutoka Ziwa Victoria ambapo vijiji kumi vitarajia kufaidika.


Alisema majaribio ya maji yanatarajiwa kufanyaika Septemba na baadaye mradi kukamika Desemba mwaka huu. Ahadi ambayo Rais alitoa ni ujenzi wa shule ambapo awamu yake ilikuta shule 78 na sasa ziko shule 265 yaani shule mpya 187.

Kuhusu ahadi ya barabara Rais Kikwete alisema tayari tathimini imeanza na ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni za mwaka 2005 ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom