Utafutaji halali unapokumbana na mizengwe inayotishia mafanikio halali, Akili za watu Huwa zinapinduka.... Na ndivyo Maana kama ni fitina za kimwili, watu hutafutana Hadi kieleweke, na kama ni fitina za kiroho, watu pia hupambana mpaka kieleweke, ni katika kupambana huko baadhi ya watu hujikuta wamejisokota na kuwa watumwa wa MATATIZO mengine mazito zaidi kama mtoa Uzi anavyotufahamisha.
Any way, imagine wewe ndiyo Tanzania, umenunua midege mikubwa, miboeing na miairbus, unataka ufanye biashara halali, unapata WAZO ulaya nitapata soko, halafu KABLA HATA HUJAZINDUA SAFARI YAKO HATA MOJA TU, unasikia umepigwa Pini juu kwa juu hakuna KUPELEKEA ndege yako huko, kwa sababu ndege zako hazina viwango🤔🤔🤔 unajiuliza waliotengeneza miboeing na miairbus ya Ethiopia, Kenya na Emirate waliweka viwango TOFAUTI na KWAKO?? Je ukipata WAZO kwamba washindani wako ndiyo wanaokupiga Pini, utakuwa unakosea?
Ingekuwa ni gemu huria hujaenda kwa Mzee Ngurumo kweli?😂😂😂
Kwanza Boeing na Airbus ni kampuni mbili tofauti za utengenezaji ndege.
Boeing ni ya Marekani 🇺🇸,
Airbus ni ya Ufaransa🇲🇫.
Na kuna aina tofauti tofauti za ndege zinazo tengenezwa na makampuni haya. Na kila ndege ina mfumo wake wa ufanyaji kazi tofauti na nyingine.
Kuna aina nyingi sana za ndege za kampuni ya Boeing. Kuna Boeing 777-300ER, Boeing 787-9, Boeing 757-200, Boeing 767, Boeing 747-8, Boeing 737Max.
Pia ndege za kampuni ya Airbus hivyo hivyo, Kuna Airbus A300, Airbus A380, Airbus A 350-900, Airbus 400M Atlas.
Kwa hivyo si kila ndege ya Boeing au Airbus ni ya aina hiyohiyo kwa nchi zote. Unaweza kuwa na ndege za kampuni ya Boeing ila ni aina mbili tofauti.
Na ndege yako inaweza kupigwa marufuku ku operate kulingana na mfumo wa aina hiyo ya ndege.
Kwa mfano Boeing 737Max zilizuiwa ku operate kutokana na mifumo yake yenye hitilafu. Ambapo ndio ilipelekea ile ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737Max kuanguka na kuua watu wote march 2019.
Kwa hivyo ndege za nchi zako kupigwa
pin si kwamba eti ni wivu wa kibiashara au sababu za kichawi, kiroho au kishetani. Hapana.
Ni kwa sababu za kiusalama na kiufundi za aina hiyo ya ndege.
Kwa hivyo hakuna mizengwe wala uchawi kwenye ndege.
Usipofuata taratibu, kanuni na sheria za ICAO( International Civil Aviation Organization) lazima ndege zako zipigwe pin.
Do you get the point?