The Inner voice: Sauti ndogo iliyo ndani mwetu ikitueleza kusudi la maisha yetu

This is me
 
Me ningependa kuuuliza Jambo hapa.

Ni kivipi nitaweza kung'amua hiyo inner voice inayonitaka kufanya mema yaliyo bora, ninapoamua kutuliza akili yangu na kuwaza juu ya Jambo linalonitatiza au juu ya maisha kwa ujumla naskia sauti zaidi ya mbili zinasema nami na kwangu Mimi nashindwa kujua ipi inafaa kufuata na sauti hizi zingekuwa mbili ningedhani moja ni ya muovu ibilisi na nyingine ni roho mtakatifu lakini kwavipi Mimi naziskia sauti zaidi ya mbili.
 
Mkuu sijapata jibu

Hakitaonekana kamwe kama utakuwa hujakifikiria kwenye mind yako..
Zaidi hapa, unamaanisha mind zetu hazina nafasi ya vitu vipya?
 
Da vincci Hii sauti ya Roho mtakatifu bana imeshaniletea majanga baada ya kuidharau sana...

Ushawishi ni mkubwa sana kuliko ile sauti isemayo kweli daima, kabla hujafanya tendo baya, itakuja hiyo sauti kwa upole itakwambia usifanye hilo jambo, ndipo babalao devil full kukushawishi na kuipotezea ile voice, utatenda hilo jambo, kifuatacho sasa ni kilio na kusaga meno..[emoji26]
 
Ndio ilivyo kiongozi. Tunapenda tunda kimasihara huku hapana.
Hii ni kwa wachache
Labda kwakuwa matunda yanalinda mwili.

Somo nimelielewa, Ila hiyo inner voice inakuja wakati gani? Au Ni Ile Hali Kama unawaza Jambo flani, unakuta mtazamo mkubwa then unakuja mtazamo mdogo, possibly uko tofauti kabisa na mkubwa?
 
Ukitaka kuiweza japo kwa asilimia kubwa badilisha mazingira uliypo nenda kwingine. Yaan kama upo ndani toka nje kama upo nje sogea sehemu nyingine. Kama ni mtu wa dini na imani kwa MUNGU omba akusaidie kuliepuka.

Mwili una ushawishi mkubwa sana kwa sababu upo nyumbani kwake (duniani). Wanasema hata mbwa muoga ni mkali akiwa kwao. Duniani sio nyumban kwa roho inazidiwa na mwili ambao humu ni kwake.

Inahitaji nguvu ya sala kuuweza. Ili uwe na nguvu kimwili lazima roho iwe dhaifu na kinyumeche. Kuepuka mabaya yanayoepukika ni lazima uufanye mwili kua dhaifu.
 
Hapo mwishoni ni mimi kabisa. Hua napata sifa kadhaa kutoka kwa watu, watu hunjona nipo kawaida sana naenjoy life, ila mimi najiona nipo kwenye tabu, nipo gereza ambalo sioni ukomo wa kifungo. Najiona nafsi ikiwa gerezani. Sinakumbu kumbu kama nimewahi kuipata furaha maishani.
 
Furaha maishani, unajua nini?
Nafsi uhangaika kwa sababu kila wakati haiko kwenye equilibrium na mwili, unahangaika Kwa sababu mwili hauishi kwa kulitumikia kusudi lako, kwa lugha nyingine unakumbushwa kuwa mambo yako hayako sawasawa, shtuka na jipange tena ili urudi kwenye mfumo utakaokupeleka kwenye kutumikia kusudi, ndiyo maana unakosa amani na unakosa utulivu, unajiona kama uko kwenye kifungo, indeed yes huitwa”vifungo vya nafsi”. “Soul ties”

Unajifunguaje sasa urudi kwenye kuishi kusudi ili uwe free???
Ni somo la peke yake pia.

 
Labda kwakuwa matunda yanalinda mwili.

Somo nimelielewa, Ila hiyo inner voice inakuja wakati gani? Au Ni Ile Hali Kama unawaza Jambo flani, unakuta mtazamo mkubwa then unakuja mtazamo mdogo, possibly uko tofauti kabisa na mkubwa?
Ukitaka kuisikia vizuri.. ukiwa unataka kufanya jambo baya. Utaisikia inakuambia kiupole sana (hio ndio original) baadae Utaisikia sauti nyingine inakupa amri ya kutenda jambo hilo (Hio ni fake inayotoka gizani)

Ukitenda hicho kibaya baadae utasikia ile sauti ndogo ya Mwanga inakulaumu kwa kutenda jambo hilo. Waswahili tunasems roho inanisuta.

Hata kwenye mawazo kama ulivyosema.. Sauti ile hukupa mitazamo ya mlengo chanya kwa njia ya upole kwakua Mungu ni pendo. Haamrishi kitu amekupa free will
 
Pole sana mkuu DS kwa yaliyokupata. Nikusahihishe kua sauti ile ya roho mtakatifu hua haimletei majanga mtu. Ni wewe binafsi ndio ulijiletea maana yenyewe ilifanya kazi yake ya kukushauri mema kwenye jambo lako. Ila hukuisikiliza. Mkataa pema pabaya panamuita..
Umepewa free will...ulitumia nafasi yako ya kuchagua sauti kubwa au ndogo.. usiilaumu saiti ya Roho mtakstifu

ukiwa unataka kufanya jambo baya. Utaisikia inakuambia kiupole sana (hio ndio original) baadae Utaisikia sauti nyingine inakupa amri ya kutenda jambo hilo (Hio ni fake inayotoka gizani)

Ukitenda hicho kibaya baadae utasikia ile sauti ndogo ya Mwanga inakulaumu kwa kutenda jambo hilo. Waswahili tunasems roho inanisuta.

Hata kwenye mawazo kama ulivyosema.. Sauti ile hukupa mitazamo ya mlengo chanya kwa njia ya upole kwakua Mungu ni pendo. Haamrishi kitu amekupa free will
 
Mate

Tunaposema sauti ndondo hatumaanishi "High Volume/sound" maana zote zipo kwa mfumo wa mawazo. Tunachogundua kwenye kutofautisha sauti hizo ni Jinsi sauti hizo zinavyosound ndani yetu.

Ile tunaita sauti kubwa maana hua inakua na Command kwenye mawazo/maamuzi yako. Na command hiyo hua inataka utekeleze vitu ambayo ni vibaya. Kumbuka Shetani hana free will kwamba atakuacha uchague lipi unalotaka yeye anataka utekeleze ubaya wake tu ndio maana anakupa Command

Sauti ndogo utaitambua maana yenyewe inatumia Polite Request, Itakushauri kiupole mno juu ya kitu unachotaka kufanya. Itakueleza madhara ya jambo unalotaka kufanya wakati sauti kubwa haitakueleza. Lakini Mungu si dikteta bado atakuacha either uichague sauti hiyo au ufuate sauti kubwa.
 
Shida mara nyingi hua tunasoma fani kwa sabubu
  • Fani fulani inaajira nyingi na msahara mzuri
  • Wazazi wanatuhimiza kusoma fani fulani kwa kua wanatamani watoto wao wawe watu fulani kwenye jamii ili kwao iwe kama pride.
  • Tunaenda kusoma kitu fulani kwakua marks nilizopata ndio zinaniwezesha kusoma kitu fulani (Hasa waalimu)
Hizi mkuu zinasababisha watu kuishi nje kusudi lao pia. Inatakiwa mtu usone kitu ambacho unakipenda toka ndani..sio ukisome kisa msukumo kutoka nje ya mazingira yakuzungukayo. Kama umesoma kitu unachokipenda toka ndani hata uwe unalipwa 50k utaifanya kazi yako kiuweredi na furaha kubwa
 
Interested.
So what next what to do and how to do.
Maana umeniacha njia panda nakosa uelekeo.
 
Mate..
Safi sana, mimi ndivyo ninavyoishi pia. Furahia hivyo ulivyo na wala usijione wa tofauti. Ukianza kujiona haupo sawa jinsi unavyoishi utampa chansi shetani apenyeze roho ya tamaa ya vitu/mali. Furahia hali yako mkuu hakuna kitu kibaya kama tamaa ya mafanikio. Jipongeze sana kama umeweza kudhibiti hali hiyo.
Swali langu je, ndio sauti ndani mwangu ikizungumza na mimi juu ya baadae yangu ijayo? Au ni mawazo tu najiwazia yananitia moyo?
Mawazo, Ushauri wako na wengine pia.
Swali gumu lisilojibika kwa wengi ni WHO AM I?
Kwanza uelewe wewe unaishi tu ila usukani/Destiny wa maisha yako upo kwa aliyekuumba.
Kama inakuyia moyo ni sawa pia. Duniani cha msingi sio pesa hatukuja kutafuta pesa. Utajiri mkubwa kwa binaadamu ni furaha ya maisha anayoishi,haijalishi maisha yakoje.
Mkuu wewe ni Roho iliyotoka kwa Mungu. Swali hilo linajibik vizuri sana..Wewe ni kusudi. Ndio maana inatakiwa ujue kusudi lako
 
Je kuna uwezekano wa kutokea mgogoro wa nafsi na mwili. Nafsi inataka hiki mwili unataka hiki, Hapo unakuta kuna shida kiroho? Ama ni jambo la kawaida.

Najihisi kukosa utulivu wa nafsi kwa kitambo sasa. Kiasi chakua *sometime yes somwtime no*
Nb. Nafsi/Spirit haihusiki juu ya hilo mkuu. Inayohusika ni roho yako, Roho/soul yako ndio kila kitu chako
Roho ipo radhi lakini mwili ni dhaifu. Mambo mengi inayotaka roho ifanye hua yanaukandamiza mwili kwa kiasi fulani hivyo mwili hua haukubali unajitahidi kushindana. Mfano roho itakuataka leo ushinde kwenye maombi na mfungo ila mwili unakataa unataka leo uende kula bata somewhere. Kufunga kunatesa mwili ila kunashibisha roho. Shetani anakamatia huko kwenye mwili sasa.
Mateso ya mwili ni ya kipindi kifupi kwa hapa duniani..ila raha ya mwili yataiteketeza roho yako milele na milele
 
Ahsanate sana Brother kwa kunipa sifa hizi
Naomba sana sana Mungu azidi kunifunulia mengi nisoyoyajua tujuzane humu ndani
 
Nimekuelewa mate. Hope Yatakaa sawa.
Hua ni muumini wa kuwaambia watu utajiri wa ya kweli ni wewe kua wa kweli yaani nikua na amani ya moyo inatosha.
Japo ni ngumu ila huu ndio ukweli.
 
Nimeelewa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…