The Inner voice: Sauti ndogo iliyo ndani mwetu ikitueleza kusudi la maisha yetu

The Inner voice: Sauti ndogo iliyo ndani mwetu ikitueleza kusudi la maisha yetu

Mimi nina changamoto nyingi mpka sasa nina miaka 30 , Lakini sijui ni nini lengo la mimi kuwepo duniani, Kwa sababu nimejitaidi kufanya niliyoweza kufanya, Matokeo yake nimeambukia kutengwa, kuachishwa kazi,mahusiano pia nimekua nasubiri labda sku moja mambo yatabadilika, Amani ya nafsi sina, nina mda mchache sana ambao akili yangu hutulia .
Pole sana ndugu. Hujachelewa kabisa kuishi ndani ya kusudi lako. Hujui unatakiwa kuishi muda upi na Kwa Mungu muda haupo so hakuna kuwahi wala kuchelewa.

Yule bwana mdogo kutoka nazareth aliishi kusudi lake kwa muda wa miaka miatatu tu. Ila kafanya pakubwa mno mpaka leo tunamkumbuka.

Unajua nguvu ya wazo.?kwakua unataka kujua kusudi lako weka dhamira kisha omba Mungu utafunuliwa kadri ipasavyo
 
View attachment 1485284
Salute.
August 17 mwaka 2018 niliweka mada humu ambayo inakichwa cha habari kisemacho “ https://www.jamiiforums.com/threads...a-mwanadamu-kujitambua.1469399/post-27991776“. Lengo kuu la mada hiyo ilikua kumfanya mtu ajiulize maswali ambayo yatamletea majibu ya kujitambua kwamba yeye ni nani, Bahati mbaya mada hiyo haijibu moja kwa moja kwamba “wewe ni nani?” Ili ujitambue wewe ni nani lazima uanze kujua kusudi lako (purpose) ni lipi ndio utapata jibu kua wewe ni nani hasa. Hivyo basi mada hii ni Sequel ya mada hiyo ya mwaka 2018, Kwa mpangilio uliosahihi ili uelewe vizuri concept hii ya kujitambua mimi ni nani na kusudi langu ni lipi.

Kila mwanadamu ana kitu Fulani kilchopo ndani ya kichwa chake kitaalamu wanaita Internal Monologue au self-talk au inner voice. Hii ni sauti Fulani ipo ndani ya vichwa vyetu hua ni sauti ndogo tena ya upole sana, Sauti hii imeundwa na kitu kinachoitwa Self –Concept au sense of self. Self-Concept ni ile hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future selves (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo).

Self-schemas: katika saikolojia na sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Kama tulivyoona hapo juu kwamaba inavoice imeundwa na self-concept, self-concept ndio hupelekea mtu kuweza kujitambua kwamba yeye ni nani, hivyo basi vyote hivi humuweka mwanadamu aweze kujitambua na kujielewa.

Kusudi (Purpose)
Kila mwanadamu ameumbwa kwa “Kusudi/Purpose” Fulani, Hili ni lengo kuu lililofanya tuumbwe na kuwekwa hapa duniani, ukifungua kitabu cha Katekismu katoliki swali la kwanza kukutana nalo linauliza kwanini Mungu kaniumba? Mungu katumba ili tumwabudu na kumtumikia. Hilo ndio kusudi au lengo kuu lililofanya sisi tuumbwe na kuwekwa hapa duniani, si vinginevyo! Lakini mbali na hilo kusudi kuu pia kuna kusudi ndogo ambayo kila mtu kapewa tofauti na mwingine, Lakini pia unaweza kuta kusudi lako linafanana na mwingine.

Wakati mungu anamuumba mwanadamu mwili wa mwanadamu ulikua ni kasha tu au kama mdoli au kipande cha mgomba tu ambao haujui chochote, Mungu alimuwekea mwanadamu pumzi yake ya uhai (Roho) akapata uhia na utambuzi, kama pumzi hiyo ilitoka kwa Mungu basi nayo ina uungu ndani yake. Roho imeundwa na Mind,intellect na Impression..subconcious mind iliyopo ndani ya Mind ndio sehemu kuu ya Roho, Subconcius Mind ndio data bank yako yaani inahifadhi taarifa zako zote,imani yako,Ujuzi na utambuzi wako,kumbu kumbu zako lakini kubwa zaidi ndio sehemu inayohusika na mfumo wa kukuongoza wewe. Huko juu tumeona kwamba kila mtu ana sauti Fulani iliyopo ndani yake, yaani ndani ya Mind yake…Sauti hiyo imeundwa na self-Concept ambayo inakuwezesha kutambua wewe ni nani lakini pia tumeona kwamba Subconcious Mind ndio inahifadhi kila kitu kwa mantiki hiyo Tunaweza kusema kwamba Sauti ile ndogo ambayo tunaisikia ndani yetu inatoka ndani ya Subconscious mind ambayo ipo ndani ya Roho. Roho imewekwa na Mungu hivyo ile sauti ndogo ndio wewe (Who you are) maana muda wote kama umeisikiliza kwa makini hua inakuambia mambo mema tu, muda mwingi hukushauri na kukumbusha ulipotoka, ulipo na unakoelekea. Muda mwingine hukuonya kwa kukukumbusha adhabu ambazo unaweza kuzipata kama utaacha kuishi ndani ya kusudi kuu kwa kuhitimisha sasa tunaweza kusema kwamba ile sauti ndogo inatoka ndani ya Roho mtakatifu-Mungu aliye ndani yako.

Sauti ndogo ile ndio hutuelezea kusudi la maisha yetu hapa duniani, bahati mbaya kwa ukiburi na kujifanya tuko wabize sana maishani hua hatuna muda wa Kusikiliza sauti ndogo iliyo nadani yetu ili tujue kusudi letu…. Kua makini Yule mwovu hua anatuma Virus kushambulia server zako rohoni ili kuinterupt request zote zinazotakiwa kua processed mwisho unajikuta unamsikiliza yeye. Mwovu kautawala mwili anatumia mwili wako kuivamila roho yako. Ndio maana unakuta sauti ndogo ile inataka ufanye kitu Fulani chema, kumbuka yeneyewe haiwezi tenda inategemea mwili, bahati mbaya roho inakuta Shetani kashafunga Firewall na Virus kibao kwenye mwili, mwili unakataa request za kutekeleza yale mema roho inayotaka unakua unaprocess request za kwenda kufanya yale mwili upendayo kama starehe. Cha kufanya ni kuinstall Antivirus za maombi na matumaini kwa muumba wako

Unaishi ndani ya kusudi/mpango wa Mungu?
Mfumo wa maisha yetu ya dunia ya sasa ukiangalia unaweza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu jinsi tunavyoishi. Ukichunguza kwa makini utaona tunaishi katika mfumo Fulani ambao watu walikaa wakaunda. Kwamba mtoto akizaliwa akue aende shule, akimaliza shule atafute kazi au kuoa kisha aanzishe familia yake na kuihudumia kwa kujitafutia kipato. Lakini je hivyo ndivyo muumba aliumba tuishi? Unaweza kuona mtu maisha yake yote anayatumia kwenye mahangaiko ya kutafuta maisha, je tulikuja duniani kutafuta maisha? Jibu ni NO. hatukuja kutafuta pesa wala utajiri duniani, hatukuja kutembea hapa duniani kuna kitu Fulani tumeletwa kuja kukifanya na si kutafuta maisha wala utajiri.

Inawezekana sisi waafrika ndio tunaongoza kutokuishi ndani ya kusudi letu tuliloumbiwa kutokana na mfumo mgumu wa maisha yetu, lakini kwa kiasi Fulani tunaishi ndani ya mpango wa Mungu alivyotaka. Tunaishi kijamii baina ya mtu na mtu, shida na raha tunachangia majirani. Lakini kusudi la kila mmoja mmoja mmoja hatuliishi. Mtu anaamka saa 10 usiku kila siku kwenda kujitafutia kipato, anayatumia maisha yake yote kutafuta pesa za kujikimu. Mwisho anafika uzeeni hajapata alichosumbukia maisha yake yote, anakufa hajui kama maisha yana maana kubwa zaidi ya kutafuta pesa.
Ukipata muda kaa jichunguze mfumo mzima wa maisha yako kuanzia asubuhi mpaka usiku, toka ulipozaliwa hadi leo ulipo. Je unavyoishi ndivyo ilitakiwa iwe? Je ni kweli ulikuja

Je nitalifahamu vipi kusudi langu..?
Kwanza kabisa ili ujue kusudi lako inabidi uelewe kwamba wewe ni nani? Ulitoka wapi? Upo wapi na kwa sababu ipi? Na nitaelekea wapi? Majibu ya maswali haya yote yanajibiwa kwamba “kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vionekanovyo na visivyonekana na vyote viliumbwa kwa kusudi yake na kwa ajili yake” Wakolosai 1:16
Kama unataka kujua kwanini upo duniani hapa inabidi uanze kumkiri Mungu muumba wako kua ndie aliyekuumba,ulizaliwa kwa kusidi lake wazazi wako hawakupanga wewe uzaliwe ni yeye ndio aliyepanga uzaliwe. Hukutokea duniani hapa bahati mbaya, huwezi kulifahamu au kutambua kusudi la maisha yako kama hutoanza Kumtanguliza muunmba wako kukuonyesha kusudi alilokuumbia. Kila mtu kaumbwa na kusudi lake hapa duniani bahati mbaya wengi hatuishi ndani ya kusudi letu maana hatumuweki mbele Muumba wetu atujulishe kusudi letu, Lakini pia kwa hali ya ajabu kabisa usishangae kusudi lako likawa lipo tofauti na wengine kwa kiasi Fulani..Kuna watu wameletwa hapa duniani wao kusudi lao kuu ni kusaidia watu wengine wanatimiza makusudi yao. Kwa mfano Yohana mbatizaji alikuja duniani kwa ajili ya kukahakikisha kusudi la Yesu Kristo linatimia kwa kumuandalia njia. Pia mitume wa Kristo kusudi lao ilikua kusambaza kusudi la Kristo kwa walimwengu wote. Mungu ndie aliyekuumb naye ndio anayejua kusudi lako ni lipi, mwambie akuonyeshe kusudi lako.

Maana ya maisha yako hapa duniani utaijua kama utalijua kusudi la maisha yako, kusudi la maisha yako linatoka kwa Mungu. Muombe Mungu akujulishe kusudi lako atakueleza kwa kupitia ile sauti ndogo iliyopo ndani ya roho yako. Chukua muda wako sikiliza sauti ndogo iliyo ndani yako inakueleza nini, siku zote kusudi lako hua ni jema machoni pa watu wanaokuzunguka na mbele za Mungu muumba wako. Sikiliza ile sauti inakuambia ufanye nini, kitu chema..anza kukiishi.Binafsi nilikua nikiona watu wanaoomba barabarani naogopa kukutana nao pengine nawakwepa, nikiona watu wanashida roho inaniuma sana ndio nikajua roho yangu inataka nifanye nini kuhusu watu wenye shida.I pledged and dedicated my life to those who need help, hatakama itakost uhai. Bahati mbaya bado sijafika hatua nayotaka hasa.moja ya kitu nifanyacho ni kushare na wenzangu chochote kile kilichopo ndani ya akili yangu-for free.

Nyie hamuwaonei wivu baadhi ya watu waliosihi ndani ya kusudi lao, wameacha alama duniani mpaka leo tunawakumbuka. Namuonea wivu sana Nyerere,yesu,newton,Da’Vinci,Mother Teresa,Paulo,St.stephano nk nk. Natamani siku moja niishi ndani ya kusudi langu kwa asilima japo 60% hata nikifa niwe nimekufa kihalali. Maana dunia na wakazi wake watakua wamefaidika uwepo wangu hapa duniani.

“Mungu anasema Nilikuumba katika fikra zangu kwanza kabla ya kukuweka tumboni mwa mama yako, nilikujali toka siku unazaliwa. Nitakujali ukiwa kijana mpaka ukiwa mzee na siku zote za maisha yako. Maana mimi ndio nilikuumba na nitakujali”
Ahadi za Mungu ni timilifu, akisema anatenda. Japo tunamkosea pakubwaaa ila anatujalia mengi sana tuliyomuomba na mabayo hatujamuomba. Usiokope kumuuomba muumba wako akujuze kusudi lako, yeye ni muumba wako na baba yako, Onyesha utii japo kidogo juu yake uytaaona neema nyingi maishani mwako. Hukuumbwa uje kubeti,kuibia watu, kua karaha na kikwazo kwa wenzako, kuja kuua watu, kuja kuonyesha umahiri wako wa kua na wanawake/wanaume wengi kwa wakati mmoja.
Miasha ni mafupi mno, ukiyaangalia unaweza kuona hayana maana tumekuja kupoteza muda tu hapa duniani bora tusingezaliwa. Huwezi kuona maana ya maisha yako kama hujajitambua. Ukijitambua utajua kusudi la maisha yako na maisha yako utayaona yana maana kubwa. Hivyo basi tusikilize sauti ndongo iliyo rohoni mwetu inayotoka kwa Mungu inatuambia kusudi jema la maisha yetu, tukishajua kusudi letu tutajitambua na maisha yetu yatakua yenye maana kubwa hapa duniani.
Be Humble,Be kind. Life is too short and full of surprises.
-The End...
{comment,like n share}

View attachment 1485282
~Da'Vinci
Uzi mzuri,ngoja nikale kwanza,nikirudi ntaupitia...
 
Nb. Nafsi/Spirit haihusiki juu ya hilo mkuu. Inayohusika ni roho yako, Roho/soul yako ndio kila kitu chako
Roho ipo radhi lakini mwili ni dhaifu. Mambo mengi inayotaka roho ifanye hua yanaukandamiza mwili kwa kiasi fulani hivyo mwili hua haukubali unajitahidi kushindana. Mfano roho itakuataka leo ushinde kwenye maombi na mfungo ila mwili unakataa unataka leo uende kula bata somewhere. Kufunga kunatesa mwili ila kunashibisha roho. Shetani anakamatia huko kwenye mwili sasa.
Mateso ya mwili ni ya kipindi kifupi kwa hapa duniani..ila raha ya mwili yataiteketeza roho yako milele na milele
Excellent here[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Nimekuelewa mate.hope Yatakaa sawa.
Hua ni muumini wa kuwaambia watu utajiri wa ya kweli ni wewe kua wa kweli yaani nikua na amani ya moyo inatosha.
Japo ni ngumu ila huu ndio ukweli.
Ndio ukweli huo. Ilimradi unapata furaha yatosha.
Unavyojishikiza kwenye material things unaijinasua kwenye spiritual things..
Any Question so far.?
 
"Ukijitambua utajua kusudi la maisha yako na maisha yako utayaona yana maana kubwa. Hivyo basi tusikilize sauti ndogo iliyo rohoni mwetu inayotoka kwa Mungu inatuambia kusudi jema la maisha yetu, tukishajua kusudi letu tutajitambua na maisha yetu yatakua yenye maana kubwa hapa duniani"Hapa pamebeba kila kitu,huwa nafurahi sana unapotumia terminology za computer,kama "Shetani kashafunga Firewall na Virus kibao kwenye mwili, mwili unakataa request za kutekeleza yale mema roho inayotaka unakua unaprocess request za kwenda kufanya yale mwili upendayo kama starehe. Cha kufanya ni kuinstall Antivirus za maombi na matumaini kwa muumba wako"Umeniongezea kitu kingine kwenye maombi yangu ya kila siku,kuomba Mungu anijalie nijue kusudi langu hapa duniani,Ubarikiwe sana mkuu Da'Vinci ...
 
"Ukijitambua utajua kusudi la maisha yako na maisha yako utayaona yana maana kubwa. Hivyo basi tusikilize sauti ndogo iliyo rohoni mwetu inayotoka kwa Mungu inatuambia kusudi jema la maisha yetu, tukishajua kusudi letu tutajitambua na maisha yetu yatakua yenye maana kubwa hapa duniani"Hapa pamebeba kila kitu,huwa nafurahi sana unapotumia terminology za computer,kama "Shetani kashafunga Firewall na Virus kibao kwenye mwili, mwili unakataa request za kutekeleza yale mema roho inayotaka unakua unaprocess request za kwenda kufanya yale mwili upendayo kama starehe. Cha kufanya ni kuinstall Antivirus za maombi na matumaini kwa muumba wako"Umeniongezea kitu kingine kwenye maombi yangu ya kila siku,kuomba Mungu anijalie nijue kusudi langu hapa duniani,Ubarikiwe sana mkuu Da'Vinci ...
Ahsante sana mkuu. Stephot hope ww u mtaalamu kwenye masuala haya ya Computer
 
Mimi huwa kuna nyakati huwa inatokea nataka kufanya au kuwaza jambo baya,kunakuwa kama kuna sauti inaniambia acha unafanya jambo baya,sasa unakuta nimelipania kweli nilifanye hilo jambo mpaka unakuta saa nyingine kweli nimelifanya,sasa utakuta kuna hali inaendelea kunisakama sana kuwa unafanya jambo baya ,haitaniachia hata kama ni siku mbili au tatu mpaka napoteza Amani,ila pale nitakapoamua ngoja niache na kutubu na kusema nimeamua kuacha ndio unakuta siisikii tena na pale ndio nakuta ninapata amani kwani muda wote huo inakuwa kama inanizonga kuwa nilichofanya au ninachofanya ni kibaya,nifafanulie hapo mkuu...
 
Uzi umenifanya nipoteze kitu changu nilichokihitaji
Inauma😢😢😢😯
 
Ni kweli mate
Sijajua unataka usahihi wa kiuandishi au kimaana.
●Kama ni kiuandishi basi kwa mujibu wa katekisimu yangu kuna maneno nimeruka..sikuandika sentensi nzima
■Kama ni kimaana/Kimantiki basi kwa mujibu wa holy scriptures zote zinaelwza hiyo ndio Mision ya binaadamu aliyopewa na Mungu. Alileta mwanadamu duniani ili amuabudu yeye Pekee pia afanye maisha yake ya kila siku kama mwanadamu ndio maana akamuwekea Nafsi/Uwezo wa kufanya maamuzi ya maisha yake (Free will)
Usahihi wa kuwepo kwa kusudi kwenye maisha ya mwanadamu ni ili kuleta maana ya maisha ya mwanadamu.
Wewe mwenyewe hapo ulipo una malengo yako qmbayo umejipangia kuyatimiza, kama huna malengo yako binafsi basi unakua kama ni mtu mwenye tatizo sehemu.....
Nitarudi
Hujanielewa bado namaanisha hivi Kama 1+1=2
Usahihi wa hicho unachokiona hapo Ni mantiki zilizosimama hapo.. moja inasimama kama alama ya kuelezea kitu kimoja,jumlisha imesimama kama nyongeza(kuongeza) na sawasawa imesimama kama kiunganishi cha mantiki ya swali na jibu ambalo ni 2..
So hapo ni sawasawa ni nimekuuliza kwanini 1+1 jawabu liwe 2..?!
So inamaana nahitaji usahihi wa jibu lako ambapo itakupasa ueleze mantiki ya 1+1 kuwa 2!!

So nini usahihi au usahihi unatoka wapi wa kuwa lengo letu la sisi kuishi ni kumuabudu Mungu..?????
Ngoja nikuwekee hivi
Lengo la sisi kuishi + Mungu= kumuabudu Mungu..

Naomba usahihi wa hilo jibu..??
 
Mimi naomba nikusaidie wewe katika hili kwa kukuuliza swali moja au mawili au zaidi.

1. Kwanini umeweka ulinganyo wa vitu halisi viwili visivyoshabihiana ?

2. Unapo ona simu wewe au kitu chochote kwacho kipi katika umbile fulani na nidhamu maalumu, unajifunza nini ?

3. Je kuna kitu kimekuwepo kwa bahati mbaya au "from nothing" kama kipo kitaje na utuambie umejuaje hilo ?

4. Je kuna kitu kinaweza kujiumba chenyewe ? Kama kipo ni kipi na utuambie umejuaje ?

Kupitia maswali haya na ukiwa makini, utaona ya kuwa ulicho uliza kipo dhidi yako na kuna sehemu uliruka katika kufikiri kwako.

Ahsante.
Swali lako la kwanza ndio ulilokuwa unatakiwa ulielezee kama njia ya kunijibu Halafu haya yanayofuata yatajibika nitakapo weka mtazamo wangu..
 
Mimi huwa kuna nyakati huwa inatokea nataka kufanya au kuwaza jambo baya,kunakuwa kama kuna sauti inaniambia acha unafanya jambo baya,sasa unakuta nimelipania kweli nilifanye hilo jambo mpaka unakuta saa nyingine kweli nimelifanya,sasa utakuta kuna hali inaendelea kunisakama sana kuwa unafanya jambo baya ,haitaniachia hata kama ni siku mbili au tatu mpaka napoteza Amani,ila pale nitakapoamua ngoja niache na kutubu na kusema nimeamua kuacha ndio unakuta siisikii tena na pale ndio nakuta ninapata amani kwani muda wote huo inakuwa kama inanizonga kuwa nilichofanya au ninachofanya ni kibaya,nifafanulie hapo mkuu...
Mate
Data bank yako inapenda kuhifadhi clear data...Haitaki kuweka Viruses ndani ya server zake.

Pindi Viruses zikiingia kwenye server yako zinafanya Server yako inakua nzito. Inashindwa kuchakata Information ipasavyo.. HHivyo itakua inastuck stuck katika uchakataji. Kinachotakiwa sasa happ ni Kuformat server zako na kuanza upya ikiwa safi.. na ujitahidi kufungua Strong Anti-Viruses software ili viruses wasiweze kuingia kushambulia sever zako

(Server_Roho)
(Anti virus Maombi na kusali)
(Kuformat ni kutubu)
 
nisiwe na maneno mengi sana ila niwaambie kitu maisha hayana maana yeyote endapo utakosa sehemu ya kuyaweka hilo limekua likiwasumbua wengi sana hivyo kujikuta wapo na matabaka ya imani na vitu vingine life ni meaning less hayana maana wala kusudi kama yana kusudi hebu niambie kuhusu maisha ya wanyama kwa maana hiyo hayo makusudi tunajipa sisi ili tupate tu cha kufanya

msomaji ntaanza kua nachangia maada nimechoka kua msomaji tu
 
nisiwe na maneno mengi sana ila niwaambie kitu maisha hayana maana yeyote endapo utakosa sehemu ya kuyaweka hilo limekua likiwasumbua wengi sana hivyo kujikuta wapo na matabaka ya imani na vitu vingine life ni meaning less hayana maana wala kusudi kama yana kusudi hebu niambie kuhusu maisha ya wanyama kwa maana hiyo hayo makusudi tunajipa sisi ili tupate tu cha kufanya

msomaji ntaanza kua nachangia maada nimechoka kua msomaji tu
Unataka kujilinganisha na wanyama.?
Unajua kama unamshimda hadhi malaika.?
 
Back
Top Bottom