The Most 5 skilled RAPPER in Bongo Hip Hop Of All Time.

The Most 5 skilled RAPPER in Bongo Hip Hop Of All Time.

Hi.. Every one ....?

Before sija-zungumza chochote katika uzi huu please hii thread ni kwa ajili ya fans of HIP HOP MUSIC tu please over please [HASHTAG]#TeamMziwanda[/HASHTAG] LOL, if you don't know any thing about Hip Hop Music its better ukawa msomaji tu acha wenye kuelewa huu mziki kuweza kukosoa na kuchangia kitu katika uzi huu lengo ni kukuza utamaduni huu wa mziki wa HIP HOP..
Pia haya ni mawazo yangu binafsi mimi pia na wewe unaweza kuwa na ya kwako unaweza share na sisi sio dhambi, Pia ruksa kukosa list hii ana kuzungumzia chocho kuhusu uchambuzi huu wa makala hii..

VIGEZO VILIVYOTUMIKA KUAANDA HII LIST HII NI PAMOJA NA;

  1. Uwezo binafsi wa uwasilishaji wa ujumbe kutipia matamshi na mitambao ya mdundo
  2. Utumiaji wa misamiti na lugha ya kiswahili ki ufasaha katika utuzi wa maishairi
  3. Uwezo binafsi wa ku stick katika maada husika wakati wa ku rap
  4. Ujuzi binafsi wa mitambao tofauti tofauti katika midundo
  5. Na mengine mengi..
Sorry nisikuchoshe acha tuanze kuihesabu list yetu ya rapper(Wafokaji) bora wa tano katika mziki wa bongo hip hop wenye uwezo binafsi wa siku zote ;

5. NIKK MBISHI

maxresdefault.jpg


Watu wengi wanaweza niuliza why ?, Nikk Mbishi, Jibu ni dogo tu "UWEZO BINAFSI" Nikk ni moja kati ya rapper wenye confidence na uwezo binafsi katika utunzi na kusimamia kile anacho kiamini katika maisha yake ya mziki pia ni moja kati ya rapper bora wanaozungumziwa sana katika era hii ya Bongo Hip Hop kwa utunzi wake wa kiutofauti, Nikk ni moja kati ya rapper wenye uwezo wa ku stick kwenye maada husika hasa pale anapo rap na kuvaa uhusika kisawia kama alivokwisha fanya kwenye nyimbo mbalimbali kama HISIA na KIJUSI, Moja kati ya nyimbo ambazo nikk alishawahi fanya na kuwa bora kuwahi tokea ni pamoja na KIJUSI, AU, HISIA, KILA SIKU, PLAY BOY, SAUTI YA JOGOO na pia ni rapper mwenye nyimbo nyingi zenye ubora katika misingi ya HIP HOP.



4. JCB MAKALLA

jcbngoma.jpg


Ukisikia Paaa!! Ujue imekukosa...!!!! Jcb makalla moja kati ya rapper wakali tokea Arusha japo kwa sasa kifamilia yupo aboard. Watu wengi wana weza shangazwa na list hii but kwa wafatiliaji wa muda mrefu katika mziki wa bongo hip hop hawawezi bishana na mimi uwezo wa JCB ni mkubwa sana hasa kiuandishi na ku-rap JCB ni moja kati ya rapper pale unapo wapa topic ya kuzungumzia katika wimbo husika hufanya kitu roho inapenda, Pia kitu kinacho mfanya JCB kuwa bora na ni pamoja na flow yake katika nyimbo zake. Kama ilivyo kawaida HIP HOP inatengenezwa na vitu vingi, Pia katika vitu hivyo vingi ndivyo hufanya mapenzi na washabiki kuchangua rapper wanaowapenda na kuwapa kipaumbele katika kusikiliza nyimbo zao moja wapo ni pamoja na kuwa na flow tamu, aina ya uandishi wa mashairi, uwashilishaji wa ujumbe kwa hadhira na mengine mengi vitu hivi JCB anavyo.


3. JAY MOO

Jay_Mchopnga.jpg


Jay moo, mzee wa stori tatu tofauti, hit maker wa PESA MADAFU kwa sasa . Jay moo ni moja ya wasanii wa zamani kwenye mziki wa BONGO HIP HOP, Kutokana na uwezo wake binafsi chini ya usimamizi bora wa producer bora bongo a.k.a father of bongo fleva P-FANK MAJANI amekuwa msanii ambaye hutoma nyimbo zale kwa muda na kufanya vizuri kila baada ya nyimbo zake kuwa hewani.

Moja sababu ya Jay moo kuwa msanii bora ni pamoja na utunzi wake wa mashairi, Jay moo amewahi kukili kuwa hutumia muda mingi linapokuja swala la utunzi wa mashairi na upangiliaji wa mizani katika nyimbo zake ndio sababu ya nyimbo zake kuwa hit kwa muda mingi na kutochuja ki uharaka kwenye ramani ya mziki wa bongo.


2. FID Q

Fid_Q_lg_lrg.jpg


Fid Q a.k.a Jeshi la mtu mmoja, rapper toka mwanza rapper mwenye uandishi mgumu wa mashairi na utunzi wa hali ya juu kwenye nyimbo zake. Kitu kinacho mtofautisha Fid Q na rapper wengi bongo ni uwezo wa kutumia kiswahili na misamiati migumu kwenye mziki wake kufikisha ujumbe.

Watu wengi wameshasikika wakikili kuwa huwachukua muda kuweza kuelewa nyimbo nzima ya FID Q na nini alikimaanisha katika nyimbo husika.

FID Q ni moja kati ya rapper wa zamani kwenye mziki wa bongo ambao kila siku wamekuwa wakisonga mbele katika mziki wa bongo na kupata mafaniko mengi ya mziki huo.



1. PROFESA JAY

Prof-Jay.jpg


Pro Jay ni moja kati ya rapper waliofanya mziki huu wa bongo hip hop kufika hapa ulipo kutokana na uwezo wake binafsi, Pro Jay ameweza ku washawishi wazazi wa rapper wengi wa sasa katiaka bongo hip hop kuweza kufungua milango kwa watoto wao katika mziki huu wengi wazazi kwa sasa wana amini kuwa mziki wa BONGO HIP HOP sio uhuni, Pia ki uwezo binafsi Prof Jay ni moja kati ya wasanii ambao kila wanapotua nyimbo mpya huwa hit song katika media zote za hapa Bongo na kuwa msanii anae heshimika na rika zote na kwa sasa yupo kwenye ulimwengu wa SIASA napo anafanya vizuri..


Karibu kwa maoni mbali mbali na mapendekezo yako binafsi kuhusu makala hii. Pia unawezi soma makala nyingi kama hivi HAPA na kushare na rafiki zako karibu wote ? 😎

Sugu nae huwezi kumbeza mashairi yake ni ya hit n nail on it na misamiati pia ya kidibaji dibaji inapobidi.

hivi pia hawa vijana waliokuwa wanachana kwenye mashindano enzi zile kama clouds kina godzila ect waliishaaga wapi hata kutoa nyimbo
 
Hivi Afande nae anafanya Hip hop??
Na kua MC mkali ni kua nyimbo nyingi kwani??
Anyway, simpigii chapuo Dogo ila naona pia sio wa kumuondoa.
Mkuu ulinunuaga ile albamu ya "mkuki moyoni?" by afande sele, au ata ushawahi kujipa muda kusikiliza nyimbo zake? He is very good when it comes to deliver a message with exra ordinary rhymes. Yani vina kati na mwisho, that is good and needs a skilled rapper to do that.
Hashim simuondoi ila lets face some facts, can you compare him with fid? Can you compare shadow of dark destiny(the most recognised single ya hashim) with one ( the most recognised single ya one incredible)? Can you compare his freestyle skills with nikki's?
Sikatai ni mkali but not to that extent.
But all in all, kila mtu ana sikio lake.
 
Ni mekuelewa kwa list hyo,ila ukitaka kusikiliza hiphop ya bongo "tune kiss fm any time"
 
Langa Kileo
Albert Mangwea
Afande Sele
Fid Q
Prof Jay
Mr ii Sugu
Langa alikua sana tu, ngwair pia. tunaongelea mashairi , hawa late upcomings pia kama Kala Jeremiah ila sasa sema ku classify hip hop na bongo fleva ya kawaida ndio panagomba. ila all in all mashairi wako vizuri
 
Kazi kazi ni kazi gani ile? Au ule mchiriku wakipindi kile?to plain story, cant be a great hiphop huwezi mcompare na kubanda. Prof unge mpa nafasi ya tano
Huyo kubanda overrated tu.... Na Prof is a better lyricist kuliko huyo jamaa.
 
TRUE THAT I always wonder why Mr II anapewa heshima sana katika mziki huu wa HIP HOP up to now wakati kipindi chake kilisha pita kitambo sana. To be honest hata kwa STEREO hasimami kuanzia FLOW mpaka Utunzi wa mashairi!
Unamfahamu Chuck D!?!?
 
TRUE THAT I always wonder why Mr II anapewa heshima sana katika mziki huu wa HIP HOP up to now wakati kipindi chake kilisha pita kitambo sana. To be honest hata kwa STEREO hasimami kuanzia FLOW mpaka Utunzi wa mashairi!
Achaneni hao kina Stereo wa Kukariri vina,
Mr II hata sasa ukimwambia achane mistari ya "Ana Miaka Chini ya 18" atakuchania kuanzia Verse mpaka Korasi zote bila kukata sautu wala kuishiwa Pumzi.


Kuna kipande kilikua kikisabaa kwenye whatsapp kikiuonyesha akiwa ana perform wimbo wake wa "Ni Wapi Tunakwenda" iaka hiyo yuko dogo tu, ungekiona hicho kipande angalau ungeelewa.

Binafsi nilishamuona kwenye tamasha moja hivi miaka ya hivi karibuni alichana nyimbo zake kama tatu hivi mfululizo bila playback kuanzia verse mpaka koras na hakutoka nje ya biti. Ni wasanii wachache sana wa Hiphop wenye uwezo huo. Labda tu sababu tu ya ubunge wake tunakua hatuuoni kwenye matamasha ila angekua mtaani hana kazi kauwawa ana njaa njaa pengine tungeuona nae kwenye show mbalimbali akipanda ku perform labda tungemuelewa zaidi.
 
TRUE THAT I always wonder why Mr II anapewa heshima sana katika mziki huu wa HIP HOP up to now wakati kipindi chake kilisha pita kitambo sana. To be honest hata kwa STEREO hasimami kuanzia FLOW mpaka Utunzi wa mashairi!
Hata young killah anamkimbiza
 
Roma na makini joh kwa hizi flow ni so more walitakiwa wawepo
 
kwanini Joh makin hayupo katika list hii?
Hit single za Jcb ni ngapi hadi kuingizwa katika list tena nafasi za juu kabisa?
mara ya mwisho Jcb alitoa hit tanfu lini
Ukiskia paah ft Jaymoe &fid q..Bwii ft jambo squad
 
Unajua what makes this discussion harder, ni difference in generations/era in hip hop kwa apa tanzania.
On my side naona kuna generations kama tatu apa na kila generation had/has its talented and skilled emcees.
Kuna ile generation ya mwanzo( -1999 )kabisa ya akina kwanza unit, WWA, hard blasters(baadae prof jay aliingia kwenye hii crew), kikosi cha mizinga ( akina hashim dogo wakiwemo humo), balozi, de-plow-mats (akina saigon, stiggo, storm-armour shamte etc), sugu etc. Hii era walikuwa skilled, concious and mostly walichana kwa kiingereza( walikuwa wanyamwezi sanaaa)
Generation ya pili(2000 - 2005) ndo akina prof jay(when he started his solo career), jay mo, afande sele, nature, solo thang, fid ( as a late comer on this era), akina east coast team etc. Hii era ilikuwa some how concious, skilled, storytallers, walikuwa na flow nzuri and walipata nguvu kwa kurap in swahili.
Generation ya tatu(2006 -) ndo akina fid (as early comer in this era), chid, langa, joh makini, tamadun music ( akina nikki, stereao baada ya kutoka lunduno, illmatix ). Hii era ndo ina watu wana flow nzuri, very high skills, wanajua mambo mengi, watu wanachana kwa lugha zaidi ya moja(of course ICT inawasaidia sana). And to be honest, kwa upande wangu lunduno na mexicana walibadilisha upepo mzima wa hip hop tanzania. Apa ndo tulipoanza kuona flow kali za kuvutia (simaanishi kuwa zamani flow zilikuwa mbaya, dont get me wrong), skilled lyrics and rhymes.
Sasa tunapofanya comparison lazima tujua pia nyakati za hawa emcees. Leo hii siwezi kulinganisha hashim na one au fid afu niseme hashim mkali, huo utakua na uongo.
NB. Prof jay is exceptional, he has his own ground.

Maoni yangu.
Lunduno, Mexicana siwajui kabisa hebu tupia single zao
 
Back
Top Bottom