The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Uongo katika story ni kufungwa kwa SMS, japo ni kweli wakati wa kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Tanzania, kutokana na Watanzania wengi kuwa na simu janja na kila mwenye simu janja akanunua bundle ili kufuatilia uchaguzi kwa kutumia internet, mtandao wa internet ghafla ukaelemewa hivyo ukawa slow na sometimes ukawa haupatikani, hivyo watumiaji wa WhatsApp, Facebook, Twitter, YouTube etc ikawa haipatikani, lakini SMS zilikuwa zinapatikana kama kawaida kwasababu hazitumii internet hivyo mtu huhitaji kuwa na bundle kutuma au kupokea SMS!. Hawa New York Times ni waongo!

Alifile hii story kutoka Tanzania ni shirika la habari la AP. Kwa vile mimi ni mwandishi, na kwenye uandishi tulifundwa darasani ukipata story from a single source, kabla hujai publish, editor unapaswa kui verify kwa kufanya kitu kinachoitwa double checking na cross checking kwa watu wengine zaidi ya huyo single source wao, and it was as simple as ABC, unampigia mtu mwingine yoyote aliyeko Tanzania, una verify uliyoambiwa na source wako, jee ni kweli internet was down? Je, hata SMS? Wangepata majibu!.

Uongo kuhusu kutopatikana mawasiliano ya SMS ndio samaki mmoja aliyeoza, katika hili tenga la samaki wa story ya The New York Times kuhusu uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

My Take
Kwa kawaida siku zote mimi huwa nashauri uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, siku moja utageuka ukweli, lakini kwa makala hii, sishauri tukanushe uongo huu mdogo kuhusu SMS tuu, huu ni wa kuu puuzia tuu, maana kukanusha uongo wa gazeti kama The New York Times, ni kama kufungua the Pandora Box, kunaweza kufumka mavitu ya ajabu!.

Don't underestimate the powers of media, magazeti ya Marekani!. The Washington Post, limewahi kuandika story ya kashfa ya Watergate, ikampopoa rais wa Marekani toka White House, ikulu akaiona chungu, akabwaga manyanga na kuachia ngazi!.

Hata magazeti yetu, japo mengi ni ya kufungia samaki, lakini kwa mahitaji yetu ya Tanzania na uzalendo!, hakuna gazeti Tanzania linaweza kusema uchaguzi Mkuu haukuwa huru na wa haki, kwa mujibu wa magazeti yetu, uchaguzi mkuu wetu, licha ya kukabiliwa na dosari ndogo ndogo, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, walioshinda wameshinda kwa haki na kihalali, walioshindwa wameshindwa kwa haki na kihalali, wakubali matokeo, uchaguzi sasa umekwisha , kazi iliyo mbele yetu ni kazi moja tuu, kuijenga Tanzania.

Namalizia na lile swali la msingi la bandiko hili kuwa Gazeti la The New York Times, la Marekani, ambalo ni la tatu kwa ukubwa wa kusomwa sana duniani, lasambaza uongo kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki!, Je ni kweli tunyamaze tuu au ni uongo tukanushe?.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
[/QUOTE]
Kwani wanumge wameshinda kwa asilimia ngapi na madiwani kwa asilimia ngapi?
 
Mayala bwana!! Ukada unakufanya unakuwa kipofu kabisa!! Katika kipindi hiki cha 2020-2025 usipoupata ubunge wa zile nafasi 10 basi utapata teuzi ya RC, DC, au balozi.

Kama lengo lako ni kuwinda uteuzi nakuelewa. Ila kama lengo lako ni kutupa habari, nakupongeza pia.
 

Kaka kwa hiyo wewe kwenye article yote hiyo kuhusu uchaguziulichoona uongelee na kuja naconclusion yote hiyo ni SMS tu? Hata hiyo SMS unajua kuwa bundle zote za SMS kwa tigo zilikupa sms 14 tu nomatter umenunua bundle gani hiyo ni kawaida? Filtering ya SMS kuzuia SMS Fulani Fulani hukuiona? Ulisha sema hadharani unajiunga na siasa na ukainisha chama chako haya maoni yako hayashangazi. Subiri uteuzi.
 
Mheshiwa Pascal, tulikushauri bora uendelee na Siasa tu, kwenye siasa huhitaji kufikiri. Kwenye Uandishi kwa sasa utajidhalilisha tu
 
Acha uongo kuwa na aibu eti mitandao ililemewa
Mkuu usishushe hadhi yako kwa mambo ya hovyo jenga msingi imara ukweli utakuweka huru.
Kuwa mzalendo ipende nchi yako
 
Hapo kwenye "Your take" ulipozungumzia internet shutdown aisee umetudharau sana mkuu kama vile unaongea na watu wa vijijini.

Kwamba mtandao ulikuwa slow kisa watu wengi wamenunua bando ili kufuatilia uchaguzi mkuu. Hata ISP wenyewe hawakusema kitu kama hicho bali walikiri kabisa kuwa wamefunga baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii.

Hii ni hoja dhaifu au niseme mfu kabisa kuileta kwa watu wenye uelewa.
 
Wamarekani mpaka dakika hii wanahangaika na Donald Trump, wanajaribu kumshawishi akubaliane na ukweli kwamba ameshindwa uchaguzi mkuu.

Wanachokifanya, kwa bahati nzuri wapo wamarekani wachache wanaelewa kuwa ni siasa za kishenzi za kibeberu.

JPM ni mzalendo ambaye waliompigia kura wanaelewa ni kipi anachoweza kukifanya kama rais na kipi hana uwezo wa kukifanya.
 
Kufungwa kwa sms enye jina la lissu na kutuma sms zaidi ya 10 haikuwezekana
 
Mkuu vita dhidi ya mabeberu hujaielewa na pengine wewe ni mmoja wa mawakala wao. Hakuogopwa Lissu bali mfumo wa nchi ulifahamu ni kina nani walikuwa nyuma ya Lissu na nguvu yao ni ipi.

Lissu mzaliwa wa Singida aliyesomea shule za humu humu nchini hawezi hata siku moja kuogopwa ila Lissu anayevaa udalali wa wazungu anatazamwa kwa umakini kwani keshakubali kuwafanyia kazi watu wenye nia mbaya.

Masuala ya INTERNET hayo ni ya dunia nzima. Ni mapambano ya kitaasisi zaidi yasiyoweza kueleweka kwa mtazamo wa jumla jumla.
 
Hamna kitu
 
nina mashaka kama huyo jamaa ubongo wake haujaoza
 
pile of rubbish
 
Hakuna uwongo hapo, walichoandika ni ukweli mtupu. Kituo nilichopigia kura mimi wakala wa Chadema alizuiwa katakata kuingia ndani, hii nimeona kwa macho yangu kabisa sijaambiwa na mtu! - Sasa uchaguzi gani huo!

Kwa hiyo hayo maneno yako, ndiyo tayari ushahidi wa kutusadikisha kwamba uchaguzi uliibwa???
 
We need not to be told. We saw by our eyes. The election was sham and rigged.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…