The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Shukurani nyingi sana kwa Wazungu. Mungu awabariki sana hadi washangae!!
 
Ndugu Pascal Mayalla, hivi uchaguzi huru na haki huwa huwaje? Sijui kwa Tanzania bara, lakini je hukuona hata clip moja ya zanzibar ambapo kulikuwa na vifaru mjini, watu wanasambaratishwa kwa mabomu ya machozi, maduka kufungwa na mitaa kutokuwa na watu tarehe 27 na 28? Hukuona taarifa yeyote ile ya watu kupigwa, kuuliwa na kukamatwa bila kufunguliwa mashitaka yeyote yale? Uhuru si neno jepesi bwana!
 
Donald Trump anasemaje......

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni mmojawapo unayesambaza 'by virtual of en lighting us, the news is being spread to many Tanzanians like wise I knew nothing
 
Hakuna uwongo hapo, walichoandika ni ukweli mtupu. Kituo nilichopigia kura mimi Wakala wa CHADEMA alizuiwa katakata kuingia ndani, hii nimeona kwa macho yangu kabisa sijaambiwa na mtu! - Sasa Uchaguzi gani huo!
Eti mapolisi wanaenda kwenye vituo vya kupigia kura na mabegi yaliyo jaa, kwenye lindo tu! hawaendi na mabegi
 
Hata uwe mnafiki vipi huwezi kufikia level ya unafiki wa mleta mada.
Njaa tu, anatafuta uteuzi ameshajua huyu mungu (nimetumia herufi ndogo) wa kabudi anapenda sana kusifiwa ( sifa za uongo) ndio akuteue
 
Mtanzania akisoma hii habari lazima ataamini kuwa imeandikwa na mwendawazimu
 
Umesahau gazeti la Uhuru na mzalendo ambayo ni chem chem ya ukweli na uwazi,
Pia Sijawahi kuonaTV ya TBC Media kutoa habari za uzushi.

Lakini kumbuka tuu Ndugu Pascal
MEDIA ZA TANZANIA ZILKUWA ZINATOA HABARI ZA CCM TUU KWA 90% HUKU WAPINZANIA WAKITEGEMEA SOCIAL MEDIA AMBAZO BAADAE INTERNET ILIKUWA SLOW DOWN KAMA ULIVYOSEMA.

Wacha Jiwe asulubiwe na seikali yake.

Si umeona wenzetu USA na Demokrasia yao, Raisi aliye madarakani analalamika kuibiwa kura, hao ndio Mabeberu, sio sisi Africa Watawala kila siku ndio hudulumu wao kura na kuwasweka ndani wapinzani.

Hao ndio Mabeberu
 
Ushasema uwongo hafu unatuuliza. Teuzi zimeisha aisee hamuelewi?

Nileteeni MAyallaaaaa.

Nileteeni Mayallaaaaaaa
Huyu hata ukuu wa kilimo hastahili, Mayalla!!!!? Bure kabisa. Kwani waliuliza swali ili ujibu yes or no? Kwani hata wewe Mayalla ukikanusha, ukweli utabaki pale pale, hata walioko magerezani wanajua kwamba hapakuwepo na uchaguzi..
 
Mpaka sasa nimesoma mara mbili hili andiko na imeniwia vigumu sana kujua aliyeandika ni James Delicious au Paskali wa JF, yule wa awali kabla ya wajumbe wa Kawe hawajafanya yao.
 
Hakuna uwongo hapo, walichoandika ni ukweli mtupu. Kituo nilichopigia kura mimi Wakala wa CHADEMA alizuiwa katakata kuingia ndani, hii nimeona kwa macho yangu kabisa sijaambiwa na mtu! - Sasa Uchaguzi gani huo!
Tukubali kuna ukweli na uongo. Uchaguzi haukuwa wa haki, sawa kabisa. Lakini kuondoka kwa Lissu ni mapenzi yake na haina maana yoyote kama wanavyojaribu kuonesha.
 
Hoja yako ni nini? Kwako wewe ulikuwa wa haki ulivyoshughulikiwa na wajumbe. Huo mwingine wa Polisi, Usalama wa Magufuli TISS na Tume ya Mihayo ulikuwa uchafuzi. Ndivyo nilivyoielewa The New York Times
 
Mayala ktk ubora wake.
1.kichwa cha habari umeshasema the new York times lasambaza UONGO.Kimsingi tayari umeshahukumu kwamba ni uongo.Maelezo yaliyofuatia hayana tena maana yoyote.Propaganda za kitoto.
2.Binafsi hata post yako sikusoma tena.Mayalla unafikiri kwa kutumia masaburi siku hizi.unaandika km mtu aliyepaniki.Hujui uandike nn,au uandikeje ili kumfurahisha bwana yule.Pole kaka.
 
Tak Takataka,Uchafu.
 

Pascal unahangaika na Dunia isiyo saizi yako. Unapoteza muda wako labda na waswahili wenzako hapa.

Kama New York Times ni gazeti la 3 kwa ukubwa duniani maana yake linasomwa na linaaminiwa na watu wengi zaidi duniani. Sasa unapojitutumua na wewe hapa na vikaragosi gazeti vyenu vya hapa, tena kwa lugha isiyosomwa na watu zaidi ya 5 Dunia nzima unaona utaleta impact gani?

Uchaguzi wa Tanzania uliomalizika ulivuta interest za watu na nchi nyingi sana duniani. Na japo serikali kwa maksudi mazima walikataa waangalizi wa Kimataifa toka nchi za Magharibi, bado jamaa walipenyeza watu wao mwanzo mwisho. Walishuhudia uhuni na ushenzi wote unaofanywa kwenye chaguzi zetu ambazo kwa akili ya kiswazi bado unaonekana "huru na haki" maana kwa viwango vyetu huo upuuzi wote bado hawakuona kama ni dhuluma na wizi wa haki ya wananchi.

Jamaa wanasambaziana taarifa na muda Si mrefu wanatushukia subirini tulinywe!
 
Kaka Paschalali katika makala yooote pamoja na kujikunja kooote umezungumzia SMS tu kweli Paschal!?? kweli!!.Nani asiyefahamu kuwa Serikali ilizuia BULK SMS wakati wa kipindi chote cha kupiga kura na imekuja kuziruhusu last week!!.achilia mbali kuzuia Internet jambo ambalo linatosha kabisa kudhihirisha kuwa uchaguzu huu haukuwa HURU wala wa HAKI hata bila kuandika mengine ya uchafu yaliyojitokeza. Sie tulitegemea na wewe kama mwanahabari Nguri usiegemee upande mmoja uzungumzie issues kubwa zilizoathiri uchauguzi wetu ,nitaje chache kama (i) kuzagaa kwa karatasi za kupigia kura zilizopigwa tayari kwa Rais JPM hata kabla ya mda wa kupiga kura (iii) Kunyanyaswa kwa mawakala wa upinzani kupitia Jeshi la Polisi na Tume ya Uchaguzi (iii) kuwekwa kwa makada wa CCM kama wasimamizi wa uchaguzi wakuu/wasaidizi na kuwaengua maskini vijana wengi waliokuwa wameomba kazi hizo na wana vigezo na mengine mengi..... Umenishangaza saana na kunivunja moyo wa kutoendelea kusomea hii kada wewe kama Muhandishi nguri tuliyekuwa tunakuamini na kukuheshimu eti leo na wewe unazungumzia "Mabeberu"...Paschal kweli? wewe ni wakuzungumzia Mabeberu kweli!

Kwa kifupi kaka siku hizi hatukuelewi kabisa manake hata basi wangekupa Ukurugenzi au Ukuu wa Wilaya tukaweka VEMA kabisa. Pengine ngoja tusibiri uteuzi ujao manake unajitahidi kusifia hata yasiyosifika lakini bado huonekani (hawakuoni) kama wenzako wakina Shigongo et ela....
 
kasoro ndogondogo kama zip? mmezoea lugha zilezile kudanganya watu. eti madogo ndogondogo "shame on you"
 
Hv ww mtu mzima mbna umekuwa zumbukuku cku hiz?yale maigizo na mauchafuzi hujayaona????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…